MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Inasemekana hii ndiyo moja filamu nzuri iliyowahi kupendwa hapa duniani. Imetengenezwa mwaka 1972 na mara ya kwanza ilikuwa riwaya lilioandikwa na mwanafasihi wa Kiitalia Mario Puzo.
Hii filamu inaelezea jinsi gani familia za kimafia kutoka kisiwa cha Sicily nchini Italy zilikuwa zinafanya umafia mjini New York.
Ile filamu inapendwa sana na watu lakini wanasahau kwamba yale matukio mengi ya mle ndani yalikuwa ni ya Ukweli na yalifanyika. Japo Mamafia tofatuti tofauti ndiyo waliyowahi kuyafanya. Hata utengenezwaji wa ile filamu ulipigwa marufuku na mabosi wa mafia kama Joseph Colombo ambaye aliapa kwamba ile filamu haitatengenezwa.
Mfano tu kwenye filamu inaonyesha ambavyo mzee Vito Corleone anamsaidia Mwanamuziki Johhny Fontaine kupata mkataba kutoka kwa mmiliki wa kampuni Jack Woltz. Jack Woltz anakataa na Don Corleone anatuma mamafia wanaenda kukata kichwa cha farasi wake anayempenda na kumuwekea kitandani.
Kwenye maisha ya kweli Mwanmuziki Johnny Fontaine ni Frank Sinatra na Jack Woltz ni Bilionea wa Kimarekani mwenye asili ya Kiyahudi marehemu Walt Disney. Sinatra amefanya kazi na kampuni la Disney japo mara ya kwanza alinyimwa mkataba na Disney. Akaamua kwenda kwa bosi wa kimafia na wakakata kichwa cha farasi wa Walt Disney a wakamwekea kitandani. Baada ya filamu kutoka Sinatra alimtukana sana Mario Puzo na hadi baadhi ya mabosi wa kimafia walimdaka na kuanza kumuuliza yale mambo amejulia wapi.
Sehemu ya Michael Corleone nayo ni ya kweli. Na mambo yako vile vile kabisa ndiyo maana hadi waitalia wanaoshi Marekani chini ya mwamvuli wa Italian-American Civil Rights League waliamua kupambana na hiyo filamu kwasababu walisema kwamba inawachafua watu wa Italia. Ukweli ulikuja kuvuja kutoka F.B.I kwamba Italian-American Civil Rights League ilikuwa inawfdhiliwa na mamafia hasasa Familia ya Colombo ambaye alikuwa anamtafuta sana Mario Puzo.
Ukisoma hizo Riwaya za The God Father na ufuatilie matukio ya kihistoria nchini Marekani na hadi mapinduzi ya Cuba utakuja kujua ile filamu ina ukweli mwingi: Na hii ndiyo inafanya ipendwe sana na watu wengi duniani. Japo Wakatoliki wengi hawaipendi The God Father 3 kwasababu walisema inalichafua kanisa lakini ukweli ni kwamba mengi ya mle yalifanyika sana miaka ya 70's. Hadi The New York Post walisema "Hating The God Father 3 is hard as defending Sinatra"
Mpelelezi kutoka F.B.I anayeitwa John Miller aliwahi kufanya Interview na kituo cha CBS NEWS cha Marekani akasema kwamba "FRANK CASTELLO WAS THE GODFATHER" kwamba kwenye ile filamu VITO CORLEONE anafanana kile kitu na Castello. Na anasema baba yake alikuwa na urafiki na baba yake Frank Castello.
HUYU NDIYE GODFATHER MWENYEWE FRANK CASTELLO au VITO CORLEONE.
CC: Daudi Mchambuzi , MSEZA MKULU , Consigliere , Red Giant , UncleBen , FisadiKuu , mchambawima1 , werrason , eden kimario , big gift