Usichokijua kuhusu filamu ya The God Father

Mkuu Al Capone alikuwa kwenye The Scarface na ni muuza unga.
Vito Corleone ni Frank Castello ambaye alikuwa hapendi kabisa biashara ya unga.
Vito Corleone kama Frank Castello alikuwa amewanunua wanasiasa kibao Marekani.
Vito Corleone kama Frank Castello alianzisha vita kwenye familia za kimafia.
Vito Corelone kama Frank Castello alikuwa ana akali na anapenda kutumia diplomasia.
Vito Corleone kama Frank Castello alipgwa risasi hadharani lakini akapona.
F.B.I wanasema alikuwa na familia ndogo lakini ina ushawishi mkubwa balaa.

Al Capone alikuwa in Scarface???
Are you referring to Al Pacino?
If my memory serves me right najua Al Pacino ndie aliact as Tony Montana in Scarface
 
Al Capone alikuwa in Scarface???
Are you referring to Al Pacino?
If my memory serves me right najua Al Pacino ndie aliact as Tony Montana in Scarface

Mkuu hujanielewa vizuri,
Nimesema kwenye filamu ya Scarface tabia nyingi za Tony Montana zinamuigiza Al Capone.
Ndiyo Al Pacino ameigiza kama Tony Montana. Sasa mkuu wetu Finyango alihisi kwamba Don Corleone ndiye Al Capone, nikamwambia Al Copone yupo kwenye Scarface.
 
Inasemekana hii ndiyo moja filamu nzuri iliyowahi kupendwa hapa duniani. Imetengenezwa mwaka 1972 na mara ya kwanza ilikuwa riwaya lilioandikwa na mwanafasihi wa Kiitalia Mario Puzo.
Hii filamu inaelezea jinsi gani familia za kimafia kutoka kisiwa cha Sicily nchini Italy zilikuwa zinafanya umafia mjini New York.

Ile filamu inapendwa sana na watu lakini wanasahau kwamba yale matukio mengi ya mle ndani yalikuwa ni ya Ukweli na yalifanyika. Japo Mamafia tofatuti tofauti ndiyo waliyowahi kuyafanya. Hata utengenezwaji wa ile filamu ulipigwa marufuku na mabosi wa mafia kama Joseph Colombo ambaye aliapa kwamba ile filamu haitatengenezwa.

Mfano tu kwenye filamu inaonyesha ambavyo mzee Vito Corleone anamsaidia Mwanamuziki Johhny Fontaine kupata mkataba kutoka kwa mmiliki wa kampuni Jack Woltz. Jack Woltz anakataa na Don Corleone anatuma mamafia wanaenda kukata kichwa cha farasi wake anayempenda na kumuwekea kitandani.

Kwenye maisha ya kweli Mwanmuziki Johnny Fontaine ni Frank Sinatra na Jack Woltz ni Bilionea wa Kimarekani mwenye asili ya Kiyahudi marehemu Walt Disney. Sinatra amefanya kazi na kampuni la Disney japo mara ya kwanza alinyimwa mkataba na Disney. Akaamua kwenda kwa bosi wa kimafia na wakakata kichwa cha farasi wa Walt Disney a wakamwekea kitandani. Baada ya filamu kutoka Sinatra alimtukana sana Mario Puzo na hadi baadhi ya mabosi wa kimafia walimdaka na kuanza kumuuliza yale mambo amejulia wapi.

Sehemu ya Michael Corleone nayo ni ya kweli. Na mambo yako vile vile kabisa ndiyo maana hadi waitalia wanaoshi Marekani chini ya mwamvuli wa Italian-American Civil Rights League waliamua kupambana na hiyo filamu kwasababu walisema kwamba inawachafua watu wa Italia. Ukweli ulikuja kuvuja kutoka F.B.I kwamba Italian-American Civil Rights League ilikuwa inawfdhiliwa na mamafia hasasa Familia ya Colombo ambaye alikuwa anamtafuta sana Mario Puzo.

Ukisoma hizo Riwaya za The God Father na ufuatilie matukio ya kihistoria nchini Marekani na hadi mapinduzi ya Cuba utakuja kujua ile filamu ina ukweli mwingi: Na hii ndiyo inafanya ipendwe sana na watu wengi duniani. Japo Wakatoliki wengi hawaipendi The God Father 3 kwasababu walisema inalichafua kanisa lakini ukweli ni kwamba mengi ya mle yalifanyika sana miaka ya 70's. Hadi The New York Post walisema "Hating The God Father 3 is hard as defending Sinatra"

Mpelelezi kutoka F.B.I anayeitwa John Miller aliwahi kufanya Interview na kituo cha CBS NEWS cha Marekani akasema kwamba "FRANK CASTELLO WAS THE GODFATHER" kwamba kwenye ile filamu VITO CORLEONE anafanana kile kitu na Castello. Na anasema baba yake alikuwa na urafiki na baba yake Frank Castello.

HUYU NDIYE GODFATHER MWENYEWE FRANK CASTELLO au VITO CORLEONE.
View attachment 430157

CC: Daudi Mchambuzi , MSEZA MKULU , Consigliere , Red Giant
Mengine kuhusu sinema hiyo ni; 1.Baada ya Producer Paul Rudi kutumia connection zake kuwasomesha Mafia bosses kwamba the godfather haitawa-potray Waitalia vibaya walisema lazima waipitie script. Walitaka kuhakikisha kuwa maneno "mafia" na "la cosa nostra" hayatumiki hata mara moja.
2. Luca Brasi (jina halisi Lenny Montana) alikuwa ni real life mafia. Alikuwa enforcer wa Colombo crime family.
3. Baada ya The Godfather kutolewa, Mafia walitaka waione. Wakafanyiwa special screening ya peke yao. Sinema ilipoisha wafanyakazi wa Theatre walipata tip nene kwani wiseguys (mafioso)waliifurahia sana na walikuwa wanata-tip hela ndefu sana.
 
Mkuu hujanielewa vizuri,
Nimesema kwenye filamu ya Scarface tabia nyingi za Tony Montana zinamuigiza Al Capone.
Ndiyo Al Pacino ameigiza kama Tony Montana. Sasa mkuu wetu Finyango alihisi kwamba Don Corleone ndiye Al Capone, nikamwambia Al Copone yupo kwenye Scarface.
mkuu ila scarface ni Miami na Al Capone Chicago!? au ni mambo ya sanaa tu, kubadilisha hiki na kile?
 
mkuu ila scarface ni Miami na Al Capone Chicago!? au ni mambo ya sanaa tu, kubadilisha hiki na kile?

Ni mambo ya sanaa mkuu huwezi kumzungumzia mtu moja kwa moja,
Tony Montana alikuwa siyo Marekani kabisa,
Japo wanasema alitumika kuwawakilisha mamafia wengi akiwemo Al Capone.
Mfano mzuri Vito Corleone na tabia nyingi za Frank Castello lakini pia alikuwa na tabia za mamafia kama Carlo Gambino na Joseph Profaci.
 
napendaga movie za wamafia. unapata Joe Pesci?
 
Sasa sijui kipindi hiki atawazungumzia wakina nani?
Miaka ya nyuma walisema Di Carprio anaweza akawekwa kwenye filamu ya nne sijajua kama bado wana huo mpango.

Kumbuka Vincent Corleone, the illegitimate son of Sony Corleone ndio alimrithi Michael na akawa Don
So people are interested to know how he was able to protect the Corleone family after the death of Michael
Mtoto wa Michael hakuwa na interest yoyote na his father's organization
Yule binti yake ndio huyo aliuwawa
Isitoshe kuna fununu kuwa hata Al Capone alichimbiwa mkwara kabla Michael hajafa kuwa asijaribu kugusa interest za Corleone family popote pale na akawa mdogo
 
Mengine kuhusu sinema hiyo ni; 1.Baada ya Producer Paul Rudi kutumia connection zake kuwasomesha Mafia bosses kwamba the godfather haitawa-potray Waitalia vibaya walisema lazima waipitie script. Walitaka kuhakikisha kuwa maneno "mafia" na "la cosa nostra" hayatumiki hata mara moja.
2. Luca Brasi (jina halisi Lenny Montana) alikuwa ni real life mafia. Alikuwa enforcer wa Colombo crime family.
3. Baada ya The Godfather kutolewa, Mafia walitaka waione. Wakafanyiwa special screening ya peke yao. Sinema ilipoisha wafanyakazi wa Theatre walipata tip nene kwani wiseguys (mafioso)waliifurahia sana na walikuwa wanata-tip hela ndefu sana.

Haaaahaaaa cheers mkuu.
Ndiyo maana nimesema tabia za kupenda fujo ni za familia ya Colombo.
Ndiyo maana alipinga sana filamu isitoke ila wenzake wakasema aipotezee.
 
Back
Top Bottom