Full Blood Picture
JF-Expert Member
- Jan 7, 2021
- 4,470
- 9,569
Serikali ya Tanzania ilitangaza katika hotuba ya Bajeti ya mwaka 2026/2027 kuwa imependekeza kupunguza ushuru wa forodha kwa baadhi ya magari ya umeme kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10. Aidha, ilitangaza pendekezo la kusamehe VAT kwa baadhi ya vifaa vya kuchajia magari ya umeme ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi, kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuharakisha mpito kuelekea matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira.
Hata hivyo, mwaka wa fedha tayari umeanza lakini bado utekelezaji wa mapendekezo hayo haujaonekana kwa vitendo. Badala yake, kwa baadhi ya magari ya MHEV (Mild Hybrid Electric Vehicles), gharama zimeongezeka kutokana na ushuru unaotozwa, jambo linalozua mkanganyiko kwa wananchi na wadau waliokuwa wakitarajia kunufaika na mabadiliko yaliyotangazwa.
Je, ni sababu zipi zinazosababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa mapendekezo haya? Je, kuna taratibu za kisheria au kiutawala ambazo bado hazijakamilika, au serikali imeshindwa kutekeleza ahadi iliyotolewa bungeni? Wananchi wanastahili kupata ufafanuzi wa wazi kuhusu hali halisi na muda ambao mabadiliko hayo yataanza kutumika.
TRA, tunahitaji maelezo ya kina kuhusu suala hili. Si vyema kuona pongezi na vyeti vya ukusanyaji ushuru vikigawiwa wakati utekelezaji wa mabadiriko ya kodi zilizotolewa kwa wananchi unaonekana kutokwenda sambamba na matarajio. Ahadi zinazotolewa bungeni zinapaswa kutekelezwa kwa wakati ili kujenga imani ya wananchi kwa taasisi za serikali na sera zake.
Hili si suala dogo; ni kero inayowagusa wananchi wengi wanaotaka kuwekeza katika magari yanayotumia nishati safi na kuchangia juhudi za kulinda mazingira. Tunatarajia majibu ya wazi na hatua za haraka ili kuondoa sintofahamu iliyopo.