Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 137
- 179
Salaam Wana JF
Nianze andiko hili fupi la uchambuzi kwa kutoa hongera na shukrani kwa Rais Dkt. Pombe Magufuli kuendelea kuonyesha misimamo chanya dhidi ya maslahi ya Watanzania katika mambo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kifya licha ya uwepo wa mashambulizi makali kutoka miongoni mwa Watanzania wenyewe na upande mwingine kutoka kwa wageni kwa maana ya nje ya nchi, Pengine tujiulize kwa nini Magufuli anapingwa sana? Sababu ipo wazi ni kutokana na "Misimamo yake ya utaifa na mali zake" Uadui baina ya Magufuli na mataifa ya magharibi unaanzia kwenye dhana hii, historia inatuonyesha wazi kuwa kila kiongozi wa Kiafrika na mabara mengine kama Asia na hata Amerika ya kusini aliyejaribu kuonyesha " Misimamo ya kizalendo kwa taifa lake amepitia kwenye tanuru la moto na kufitinishwa na wananchi wake kwa mbinu za hila na mfarakano wa kiuchumi".
Je kizazi cha sasa cha vijana wa Kitanzania wanazijua vyema mbinu hizi mfu za Magharibi, Bila shaka jibu ni "Wachache wenye ufahamu wa falsafa hii" Wengi ni wale wanaolishwa matango pori na kujazwa upepo kama puto bila kujua athari zake hapo badae, tunao vijana wengi wanaoendeshwa na kuamini kila tamko la magharibi liko sahihi kimantiki pasipo kuchanganua ukweli wa mambo, Mathalani wakati mataifa ya Magharibi wanaivamia Libya, Walibya waliaminishwa Gaddafi ni Kiongozi muuaji na asiyezingatia utu wa raia wake, wakaamua kuamini hivyo na leo hii libya ni "Machinjio ya binadamu" kwa sababu ya Propaganda za hovyo na za kinafiki Libya si sehemu salama tena wanatamani Gaddafi afufuke kitu ambacho akiwezekani kabisa, Kwa dhana hii, ndipo swali lisilopata jibu hadi sasa uibuka, '' Afrika ni bara la watu wa namna gani" Wenye kuuliza swali hili ni wazungu wanaotutumia katika kufarakana na sisi tunaingia katika mtego huo.
Mantiki kuu ya Andiko hili nikutaka kuwaambia kuwa rais Magufuli ni mwema na kiongozi anayeipenda nchi yake na watu wake na si kama propaganda zinavyoenezwa mitandaoni ndani na nje ya nchi, inawezekana rais ana mapungufu yake kama ilivyo kwa binadamu yoyote yule lakini dhana inayojengwa kwa sasa kuwa rais Magufuli anaizuia chanjo ya corona kuingia nchini ili watu wafe "afurahi", ni dhana potofu na ya hovyo kabisa na wala haikubaliki hata kidogo, Rais ni alama ya utaifa na kivuli cha amani, Kwa Magufuli hilo lipo wazi na amelitimiza kwa asilimia zinazokubalika, bahati mbaya ukweli huu unaposemwa wapo ambao ununa na uamua kurusha matusi badala ya hoja kinzani.
Juhudi za kuijenga Tanzania ya badae zinazofanywa na Rais Magufuli uenda tusizione leo hii lakini tukaja kuziona baada ya kumaliza muda wake hapo mwaka 2025, na ndivyo itakavyokuwa, Wakati wa Rais Mstaafu Kikwete wapo walio mtusi na Kukejeli jitihada zake za ujenzi wa Tanzania, leo hii wanamlilia na kusema "Baba tumekumic", ilikuwa hivyo kwa Nyerere, ikawa hivyo kwa Mwinyi, Mkapa na hata Magufuli itakuwa hivyo, maana historia inao ukweli ndani yake. Myonge myongeni lakini haki yake mpeni, Rais Magufuli anawajibika na anadhubutu kuwakomboa Watanzania, Janga la Corona lisiwe Kigezo cha kufitinishana na kusahau mazuri ndani ya utawala wake, nina imani katika wimbi hili tutavuka salama na maisha yataendelea kama kawaida, Kwa pamoja tuijenge nchi yetu.