Ushuhuda wenye kuumiza mno

Ushuhuda wenye kuumiza mno

Hii ni simulizi ya dereva wa boda boda aliyenusurika kifo cha kuteketea na moto kwenye ajali ya Moro
Anasumulia kwamba asubuhi ile alipata abiria wa kumpeleka Nane nane... Walipofika eneo la ajali ndio kwanza ajali ilkuwa imetokea na hakuna aliyeshunghulika na majeruhi kwenye cabin ya gari... Hivyo yule abiria alimuomba dereva wa boda boda watoe msaada... Wakapanda kwenye cabin na kukuta abiria mmoja mwanamke na dereva ambao wote walikuwa wamevunjika miguu ila walikuwa hai bado
Walipojaribu kuwanasua wakakuta wamebanwa na mikanda (safety belts) hivyo yule abiria wa boda boda akamuomba bodaboda wakatafute kisu ili waje wakate ile mikanda wawatoe majeruhi... Boda boda akataka kugoma lakini yule abiria wake akamsihi wakatafute kisu wawasaidie wale majeruhi kwakuwa hata yeye boda boda hajui atakuja kusaidiwa na nani maishani...

Maneno yale yalimuingia bodaboda na kukubali huku wengine wakiendelea na harakati za kuchota mafuta yanayomwagika.... Basi ni wakati wanaiendea boda boda yao, ndipo moto ulipolipuka
Dereva wa bodaboda alinusurika ila bodaboda yake iliteketea palepale pamoja na yule abiria wake aliyetaka kutoa msaada
Maisha ni kitu gani? Maisha yamebeba siri gani? Kusudi la Mungu ninini?
Abiria mpita njia aliyekuta ajali na kutaka kutoa msaada anapoteza maisha kwenye harakati za kusaidia... Boda boda ambaye hakuwa tayari kutoa msaada pengine akuwaza muda atakaopoteza pale.. Ananusurika...!!!
Abiria yule angepita na zake pengine yasingemkuta yaliyomkuta... Utu wema wake ndio umekuwa kiama chake

Dereva wa Lori na abiria wake nao waliteketea ndani ya ile cabin... Pengine moto usingewaka wangenusurika..... Lakini anayeacha simanzi ni yule aliyejitoa kuwasaidia hawa majeruhi naye anaishia kuungua mpaka kufa.... Maisha ni kitu gani?

Inahuzunisha ndio ila kuokoa mtu kwenye mazingira hayo sio wazo zuri kabisa.

Binafsi ningefanya hivyo kama tu pasingelikua na watu wengine pembeni.
 
Angalau abiria wa bodaboda amekutwa na kifo wakati wa kutenda mema. Kufa kwake ni faida...maandiko yanasema.

Wengine sijui tutakutwa na vifo vyetu katika mazingira gani!
Wizi, utapeli ugoni ugomvi... [emoji144][emoji848]
 
Turejee maandiko ya biblia wakati Musa anamuomba Farao awaruhusu wana wa Israel waondoke Misri. Mungu akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu.

Ndicho kilichotokea Morogoro kweli unataka kuniambia watu zaidi ya 500 walikuwa wanachota mafuta na kirandaranda eneo la tukio zaidi ya nusu saa bila kumuona na kumsaidia kumuokoa dereva? Sidhani watanzania tumekuwa na moyo mgumu hivyo

Labda yametokeo hayo ili kazi ya Mungu aliyopanga itimie.
Duuuh kwaiyo aliwapa hao watu mioyo migumu ili itokee kilichotokea?
 
Bado naendelea kuangalia video ya raia kuchota mafuta na kuacha kuwaokoa dereva na mwenzie.

Raia tunakuwa na roho ngumu za kutotoa msaada hatimaye maangamizi yanàtukumba.

Nina imani yule aliyetaka kumukoa dereva amerejea kwa Muumba wake salama kutokana na nia yake ya kuokoa maisha ya wenzio ila bahati mbaya kateketea pamoja na wale waliotaka kuadhibiwa kutokana na roho zao za kukosa utu na kujali vipato/mali(mafuta)
Hata Mimi hii imenishangaza.
Yaani watu wapo busy kuchota mafuta badala ya kuwasaidia waliokuwa ndani ya gari.

Ni kukosa ubinadamu na utu .
 
Inahuzunisha ndio ila kuokoa mtu kwenye mazingira hayo sio wazo zuri kabisa.

Binafsi ningefanya hivyo kama tu pasingelikua na watu wengine pembeni.
Unapotoa msaada ,usiangalie wengine wanatoa au hawatoi.
As long as unafanya Jambo jema,wewe fanya tu..bila kujali Ni wangapi hawajafanya..na kila mmoja atatoa hesabu zake kwa nafasi yake aliyopewa.
 
Turejee maandiko ya biblia wakati Musa anamuomba Farao awaruhusu wana wa Israel waondoke Misri. Mungu akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu.

Ndicho kilichotokea Morogoro kweli unataka kuniambia watu zaidi ya 500 walikuwa wanachota mafuta na kirandaranda eneo la tukio zaidi ya nusu saa bila kumuona na kumsaidia kumuokoa dereva? Sidhani watanzania tumekuwa na moyo mgumu hivyo

Labda yametokeo hayo ili kazi ya Mungu aliyopanga itimie.
Ndicho kilichotokea Morogoro kweli unataka kuniambia watu zaidi ya 500 walikuwa wanachota mafuta na kirandaranda eneo la tukio zaidi ya nusu saa bila kumuona na kumsaidia kumuokoa dereva?
 
""Death has never been busy, He is the enemy who has no respect for people and their privacy;He will come knocking at your door anytime" African Literature.
.
death-quotes-we-all-die-the-goal-isnt-to-live-forever-the-goal-is-to-create-something-that-wi...jpeg
 
Hii ni simulizi ya dereva wa boda boda aliyenusurika kifo cha kuteketea na moto kwenye ajali ya Moro
Anasumulia kwamba asubuhi ile alipata abiria wa kumpeleka Nane nane... Walipofika eneo la ajali ndio kwanza ajali ilkuwa imetokea na hakuna aliyeshunghulika na majeruhi kwenye cabin ya gari... Hivyo yule abiria alimuomba dereva wa boda boda watoe msaada... Wakapanda kwenye cabin na kukuta abiria mmoja mwanamke na dereva ambao wote walikuwa wamevunjika miguu ila walikuwa hai bado
Walipojaribu kuwanasua wakakuta wamebanwa na mikanda (safety belts) hivyo yule abiria wa boda boda akamuomba bodaboda wakatafute kisu ili waje wakate ile mikanda wawatoe majeruhi... Boda boda akataka kugoma lakini yule abiria wake akamsihi wakatafute kisu wawasaidie wale majeruhi kwakuwa hata yeye boda boda hajui atakuja kusaidiwa na nani maishani...

Maneno yale yalimuingia bodaboda na kukubali huku wengine wakiendelea na harakati za kuchota mafuta yanayomwagika.... Basi ni wakati wanaiendea boda boda yao, ndipo moto ulipolipuka
Dereva wa bodaboda alinusurika ila bodaboda yake iliteketea palepale pamoja na yule abiria wake aliyetaka kutoa msaada
Maisha ni kitu gani? Maisha yamebeba siri gani? Kusudi la Mungu ninini?
Abiria mpita njia aliyekuta ajali na kutaka kutoa msaada anapoteza maisha kwenye harakati za kusaidia... Boda boda ambaye hakuwa tayari kutoa msaada pengine akuwaza muda atakaopoteza pale.. Ananusurika...!!!
Abiria yule angepita na zake pengine yasingemkuta yaliyomkuta... Utu wema wake ndio umekuwa kiama chake

Dereva wa Lori na abiria wake nao waliteketea ndani ya ile cabin... Pengine moto usingewaka wangenusurika..... Lakini anayeacha simanzi ni yule aliyejitoa kuwasaidia hawa majeruhi naye anaishia kuungua mpaka kufa.... Maisha ni kitu gani?

Premature death, untimely death, death caused by ignorance and negligence..

Kwa kuwa tunajifanya watu wa imani basi tunamsingizia Mungu kuwa amepanga au sijui shetani ndo kafanya yake na tunasahau kuna mahali hatujatimiza wajibu.

Fikiria police wangewahi na kuweka ulinzi hakuna mtu angelazimisha kuiba mafuta, wangesimama mbali wanaangalia.

Ukiacha Hayo chukulia mgonjwa aliye wodini anamwita nurse kwa kuwa amebanwa pumzi nesi anamu ignore baada ya mda anafariki, kumbe nesi angemuwahi kwa sindano au oxygen yule mgonjwa angepona, sisi tunasema mapenzi ya Mungu.

Kufa ni lazima lakini wakati mwingine tunakufa kabla ya muda, bado hatujui kuthamini uhai...
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji115][emoji115][emoji115][emoji109][emoji109][emoji109][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mungu mwenye upendo wote anaachaje watoto wake wanateketea?
Kwani amewaacha wateketee bila sababu ? Hujajiuliza swali hili ?

Pili, yeye ndio ametaka wateketee sababu kifo ni haki na muda ukifikia Mola huwa hacheleweshi hata sekunde.

Tatu,upendo wa Mola wetu ni upendo kamili ambao una ambatana na mambo kadha wa kadha,kama kutupa akili ya kujua lipi jema na lipi zuri,na kutupa muda wa kujirekebisha na mfano wake.
 
Inasikitisha na kushangaza kweli! mtu anashindwa kumuokoa mwenzake kwa kuchelewa kutafuta kisu kukata mkanda, wakati huo huo anakimbia haraka kutafuta dumu, ndoo, sufuria kuchota mafuta.[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Inauma sana ila hakika dunia ni mapito tu kwani hakuna ajuaye siku yake ya mwisho,mungu ilaze roho ya marehemu mahali pema amiin
 
Mungu mwenye uwezo wote kashindwaje kubadilisha io fate wanae wapendwa wasiteketee na moto?
Hili ni swali la uongo kwake,yaani umekosea kuuliza swali bila shaka kwa kutomjua Mola ana sifa gani na tabia gani.

Vipi ashindwe kuzuia wakati yeye ndio ametaka litokee na akaruhusu litokee ?

Mlitakiwa mumjue kwanza Mola ndio mumjadili,ila sababu hamumjui basi mnauliza maswali ya kitoto sana kumuhusu yeye.
 
Back
Top Bottom