Ushuhuda wenye kuumiza mno

Ushuhuda wenye kuumiza mno

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,517
Reaction score
860,567
Hii ni simulizi ya dereva wa boda boda aliyenusurika kifo cha kuteketea na moto kwenye ajali ya Moro
Anasumulia kwamba asubuhi ile alipata abiria wa kumpeleka Nane nane... Walipofika eneo la ajali ndio kwanza ajali ilkuwa imetokea na hakuna aliyeshunghulika na majeruhi kwenye cabin ya gari... Hivyo yule abiria alimuomba dereva wa boda boda watoe msaada... Wakapanda kwenye cabin na kukuta abiria mmoja mwanamke na dereva ambao wote walikuwa wamevunjika miguu ila walikuwa hai bado
Walipojaribu kuwanasua wakakuta wamebanwa na mikanda (safety belts) hivyo yule abiria wa boda boda akamuomba bodaboda wakatafute kisu ili waje wakate ile mikanda wawatoe majeruhi... Boda boda akataka kugoma lakini yule abiria wake akamsihi wakatafute kisu wawasaidie wale majeruhi kwakuwa hata yeye boda boda hajui atakuja kusaidiwa na nani maishani...

Maneno yale yalimuingia bodaboda na kukubali huku wengine wakiendelea na harakati za kuchota mafuta yanayomwagika.... Basi ni wakati wanaiendea boda boda yao, ndipo moto ulipolipuka
Dereva wa bodaboda alinusurika ila bodaboda yake iliteketea palepale pamoja na yule abiria wake aliyetaka kutoa msaada
Maisha ni kitu gani? Maisha yamebeba siri gani? Kusudi la Mungu ninini?
Abiria mpita njia aliyekuta ajali na kutaka kutoa msaada anapoteza maisha kwenye harakati za kusaidia... Boda boda ambaye hakuwa tayari kutoa msaada pengine akuwaza muda atakaopoteza pale.. Ananusurika...!!!
Abiria yule angepita na zake pengine yasingemkuta yaliyomkuta... Utu wema wake ndio umekuwa kiama chake

Dereva wa Lori na abiria wake nao waliteketea ndani ya ile cabin... Pengine moto usingewaka wangenusurika..... Lakini anayeacha simanzi ni yule aliyejitoa kuwasaidia hawa majeruhi naye anaishia kuungua mpaka kufa.... Maisha ni kitu gani?
 
So sad,
Maisha yana siri kubwa sana.
MshanaJr life is priceless
Dah maisha ni kujifunza kila leo naamini tunaendelea kujifunza, Mungu awalaze mahali pema wote waliotangulia mbele za haki.
Left to tell.... Bila huyu bodaboda assumptions zingekuwa nyingi mno kuhusu dereva wa roli... Zingetengenezwa hadithi za kila namna kumhusu... BTW kuna kitu kitabaki kuwa siri ya wafu...!!! MWANAMKE ALIYEKUWA NAYE NI NANI?
Ni abiria wa kawaida au alikuwa mtu wake?
Kwa hali ilivyo ina maana Dar alitoka jana yake na hapo ndio siku ya pili barabarani... Je alilala wapi? Na nani? [emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]
 
Bado naendelea kuangalia video ya raia kuchota mafuta na kuacha kuwaokoa dereva na mwenzie.

Raia tunakuwa na roho ngumu za kutotoa msaada hatimaye maangamizi yanàtukumba.

Nina imani yule aliyetaka kumukoa dereva amerejea kwa Muumba wake salama kutokana na nia yake ya kuokoa maisha ya wenzio ila bahati mbaya kateketea pamoja na wale waliotaka kuadhibiwa kutokana na roho zao za kukosa utu na kujali vipato/mali(mafuta)
 
Hii ni simulizi ya dereva wa boda boda aliyenusurika kifo cha kuteketea na moto kwenye ajali ya Moro
Anasumulia kwamba asubuhi ile alipata abiria wa kumpeleka Nane nane... Walipofika eneo la ajali ndio kwanza ajali ilkuwa imetokea na hakuna aliyeshunghulika na majeruhi kwenye cabin ya gari... Hivyo yule abiria alimuomba dereva wa boda boda watoe msaada... Wakapanda kwenye cabin na kukuta abiria mmoja mwanamke na dereva ambao wote walikuwa wamevunjika miguu ila walikuwa hai bado
Walipojaribu kuwanasua wakakuta wamebanwa na mikanda (safety belts) hivyo yule abiria wa boda boda akamuomba bodaboda wakatafute kisu ili waje wakate ile mikanda wawatoe majeruhi... Boda boda akataka kugoma lakini yule abiria wake akamsihi wakatafute kisu wawasaidie wale majeruhi kwakuwa hata yeye boda boda hajui atakuja kusaidiwa na nani maishani...

Maneno yale yalimuingia bodaboda na kukubali huku wengine wakiendelea na harakati za kuchota mafuta yanayomwagika.... Basi ni wakati wanaiendea boda boda yao, ndipo moto ulipolipuka
Dereva wa bodaboda alinusurika ila bodaboda yake iliteketea palepale pamoja na yule abiria wake aliyetaka kutoa msaada
Maisha ni kitu gani? Maisha yamebeba siri gani? Kusudi la Mungu ninini?
Abiria mpita njia aliyekuta ajali na kutaka kutoa msaada anapoteza maisha kwenye harakati za kusaidia... Boda boda ambaye hakuwa tayari kutoa msaada pengine akuwaza muda atakaopoteza pale.. Ananusurika...!!!
Abiria yule angepita na zake pengine yasingemkuta yaliyomkuta... Utu wema wake ndio umekuwa kiama chake

Dereva wa Lori na abiria wake nao waliteketea ndani ya ile cabin... Pengine moto usingewaka wangenusurika..... Lakini anayeacha simanzi ni yule aliyejitoa kuwasaidia hawa majeruhi naye anaishia kuungua mpaka kufa.... Maisha ni kitu gani?

LIVE IT OR SUCK IT, UKIONA BINADAMU WANAFIKIA KIWANGO CHA KUTOKUOKOA BINADAMU WENZAO WANAPOPATA AJALI KAMA HIZI NA NYINGINE KWA KIGEZO CHA KUCHUKUA MALI KWANZA KTK AJALI NA KUACHA KUMUOKOA BINADAMU MWENZIE ELEWA KIWANGO CHA ROHO MBAYA NA USHETANI KIMEFIKIA KWA KIWANGO CHA JUU, TUSITUMIE SABABU KUWA TUNA UMASKINI SANA NDIO MAENEO KAMA HAYA TUTUMIE KUJITATUA.

THIS IS MADNESS OF HIGHEST ORDER WATU KUWAZA MALI KULIKO UHAI WA BINADAMU WENZIE, SOMEONE HAS RISKED HIS LIFE SAVING OTHER PERSON LIFE BUT WENGINE WALIANGALIA MAFUTA ZAIDI KULIKO UHAI, MWENYEZI MUNGU AMJALIE TUNU YA MILELE KATIKA UFALME WAKE, KHERI WENYE MOYO SAFI NA WASAIDIAO WENGINE🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Back
Top Bottom