USHUHUDA : Manabii wanaouza maji na mafuta yaliyoombewa…

USHUHUDA : Manabii wanaouza maji na mafuta yaliyoombewa…

Mzee wa upako alishasema.
Kufa masikini ni UFALA.
maana wajinga wajinga wapo.unashindwa kubuni kitu upate hela.?
Jiongeze
 
Kuna sehemu nilienda nikakuta wanatangaza birthday ya prophet(nabii) imekaribia kama unataka kujiunga nae kusherekea birthday yake sharti utoe mchango shilingi elfu hamsini
 
Mambo yao waachie wenyewe...

Cha muhimu wawe na EFD machine na walipe kodi kwa sababu wanafanya biashara...


Cc: mahondaw
 
Siku hizi kuna mtindo umezuka mtaani hasa Jijini Dsm !

Kun manabii wanauza maji na mafuta ya kupaka yaliyoombewa kwa waumini wake. Unakuta maji chupa moja inauzwa TZS 15.000 na mafuta ya kupaka huuzwa mpaka TZS 50.000.

Watu wananunua sana hizo products. Na hao watumishi wa MUNGU wanapiga sana biashara mjini.

Mifano halisi ni hawa ambao wana Television zao au wanalipia matangazo yao moja kwa moja.

Kama Mch. Suguye na Mzee Wa Upako.

Mwenye ushuhuda wa maajabu au uponyaji alioupata atupatie tafadhari!

Wajinga ndiyo waliwao. Serikali isajili upya madhehebu ya dini na viwekwe vigezo vya elimu ya Mungu( Theology) na siyo miujiza ya bandia na ushirikina. Watu wanaumia na wana shida nyingi na kwa ujinga wao wanawaamini hao matapeli. Yabaki madhehebu machache na yanayoongozwa
 
na viongozi wenye elimu ya dini. Huu ushirikina ni biashara isiyolipiwa kodi. Uhuru wa kuabudu uwe na masharti na mipaka.
 
Shikamoo Kagame kwa kuyafuta 6000. Wakitaka usajili wawe na shahada ya elimu ya Mungu( Theology) vinginevyo wajiajiri wawe wamachinga. Huku kwetu sijui msajili naye ana kanisa lake? Mbona anaendelea kuwasajili?
 
Mimi ni mkristo lkn siku zote naona dini ya kiislam ndio imekaa kiutu
kwa nini umuuzie mtu wa Mungu kitu cha kujitibia ama baraka ya Mungu????
baraka za Mungu haziuzwi it is for free.....for every one
Yaani watu wanataka kuwa ma agent wa kuuza baraka za Mungu??
This is absurd
 
"Aliyesema waumini ni kondoo hajakosea". Acha wagongwe kitaifa.
 
kipindi cha mitume wa kale, pesa haikuchukua nafasi kubwa katika kueneza neno la mungu kwakua kila kitu kilikua kinapatikana pasipo hitaji la pesa, mitume walikua wanatembelea punda, ngamia au kwa miguu.
kwa sasa mambo yamebadilika wachungaji, mapadre wanatembelea magari, zamani kulikua hakuna huduma ya maji ya kulipia wala umeme, shughuli zote kwenye masingagogi na makanisa watu walikua wanajitolea lakini sasa makanisa yanaajili na wanalipa mishahara, ata mwanakwaya haimbi bila kupewa pesa.
usafiri, chakula, maji, umeme huduma za television na matangazo vyote vinahitaji pesa. lazima wenye makanisa watumie njia iyo kupata pesa ili makanisa yao yaendelee.
KWA DUNIA YA LEO HAKUNA DINI YOYOTE ISIYOHITAJI PESA KUJIENDESHA.
Anhaa kwa hivyo na wewe ni mpigwaji?
 
Ukiona mtu mzima analia machozi hovyo tu kisa kaokoka huyu ni kichaa...wanawake wanasikiza sana hawa wahubiri njaa waongo na wezi kama vile kweli ndio yanaokoa..

Maisha ni wewe kupambana..mtu anasema kama wewe masikin fala sasa bado unaamini atakuombea huyo?
 
Huu ni uganga wa kienyeji tu hakuna tofauti..
Nenda wema, usiwe mnafiki, usiwe mwizi, usiwe mchawi, amini Mungu yupo na ndio maana upo..muombe Mungu kwa kinywa chako na nafsi yako, jutia uovu kwa nafsi yako na umuombe Mungu msamaha.. Hiyo ndio dini ya haki...
 
Yesu aliwaambia wafuasi wake:-
Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure (Mt 10:8).

Maana ya mstari huu ni kwamba Yesu aliwapa wanafunzi wake uwezo wa kuponya wagonjwa na kufufua hata wafu. Lakini akasema hicho kipawa:-mmepata bure, toeni bure

Kwa hiyo mtu yeyote anayetoza hela kwa kuuza maji au mafuta n.k. ni mwizi. Lakini hii haina maana kwamba mtumishi wa Mungu wa kweli hawezi kutumia mafuta au maji wakati anamwombea mtu maana Biblia kwenye Marko 6:13 inasema mitume walipoenda kuombea watu"-Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza

Na wewe mwananchi usimhukumu mtumishi yeyote maana Mungu atawatandika viboko anavyojua. Wewe cha kufanya ni kuwashauri wale wanaoangamia kwa kukosa maarifa kwa kukubali kununua maji na mafuta na vitu vingine wasiendelee kufanya hivyo. Badala yake, wamwombe Mungu. Yesu alisema:-Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.


 
Anointed Water

Kuna Yule
Holy Man
Anointed Man Rugemarila 😀
Hakuwa Na Mafuta Wa Maji Ila Cash
Kwasasa Yupo Segerea 😡
 
Kama wewe ni Mkatoliki maji ya baraka yapo bure kanisani.
 
Ongeeni yote mpendavyo ila Suguye niacheni mwenyewe bora niitwe mjinga tena jinga ila hamjaniambia lolote kwa Suguye toeni povuu mpendavyo maji yake tutanunua na mafuta na kila atakachokisema kitanisaidia nabeba nimekubali kuwa mjinga povuu ruksa
Halafu wanajua sana kuwatageti wanawake, sijui wanawake akili zenu huwa ziko vipi. Mnarubuniwa kirahisi mno.
 
Mimi ni mkristo lkn siku zote naona dini ya kiislam ndio imekaa kiutu
kwa nini umuuzie mtu wa Mungu kitu cha kujitibia ama baraka ya Mungu????
baraka za Mungu haziuzwi it is for free.....for every one
Yaani watu wanataka kuwa ma agent wa kuuza baraka za Mungu??
This is absurd
Hakuna wauzaji wa spiritual products kama waisalam?Nenda misikiti kibao utawakuta wanauza hasa siku za ijumaa.Mafuta ya kuingia nuksi nk wewe acha uongo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom