USHUHUDA : Manabii wanaouza maji na mafuta yaliyoombewa…

USHUHUDA : Manabii wanaouza maji na mafuta yaliyoombewa…

Namuamini Mungu muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyo juu ya nchi ni mali yake.... miti, maji na vingine vyote ni mali yake, yeye ndo nimuombae na nimtegemeaye siku zote lakini kumbuka Mungu ni roho na si mwanadamu ninapomuomba huomba katika roho na kweli nikiamini nitakutana nae katika roho. Haya matendo ya Imani hawajaanza hawa matumishi na wachungaji wa leo hata Yesu alitumia kama ni msomaji wa biblia utakumbuka yule mtu aliyekuwa kipofu Yesu alimpaka matope kwenye macho na mate kama sijakosea na Mungu alimponya. Maji Mungu alijifananisha na maji ndo mana akasema mimi ni maji ya uzima...... Infact yale hayauzwi unachangia garama za kuyaandaa. Mfano TB Joshua kuna vitabu unapewa kama sikosei ni vitatu pachage ya hayo maji yenyewe inavutia vyote ni garama kutengeneza sasa ukipata access kwa nini usichangie garama ili wengine wenye imani na mahitaji wapate? Vitu vingine msijilimit sana. Shetani hawezi kukuonea huruma ya kiasi hicho eti akuponye hahaaaa nikuulize unafikiri wanadamu wa leo kuna anaepata shida akaanzia kwa Mungu? Hatua ya kwanza hata ingekuwa ni wewe ukiumwa utaanza hospitali, ikishindikana wanaanza matambiko sijui familia then inakuja kuna mganga sijui nini nini yakishindikana koooote ndo utasikia kuna mtumishi kule na huku hapo sasa ni muujiza wanatafuta na si Mungu kama unatafuta muujiza kwa nini usiangukie kwa matapeli?

Tumepewa nguvu na mamlaka hatutaki kuzitumia kwa nini wao wasitumie?
Tatizo lako una quote vitu vya muhimu halafu unasema kama sikosei ina maana hujaisoma hiyo biblia ama umeisoma kama kitabu cha juma na rosa. Nimekupatia sura katika biblia kukufahamisha uwezo wa shetani kuwatumia watu. Ile matendo ya mitume sura ya 8 itakusaidia sana kunielewa maana kuna watu kama TB Joshua. Tena anaitwa Petro ambaye alikua anafanya miujizi kama kina John na Petro kasoro tu Petro alitumia Roho mtakatifu. Hivyo alipokutana na kina petro nakuona wenzake wanawawekea mikono watu na wanashukiwa na nguvu za roho mtakatifu wakati yeye kajaribu kashindwa akawaomba wamuuzie hiyo karama na ndipo Petro akamwambia yale nilikuambia katika comment iliyopita. Na hii dhambi inaitwa Simony maana jina lahuyo mtu alikua simon petro. Ukiisoma hii account utagundua nini nilichotaka ukifahamu
 
Masikini ndio huwatajirisha matajiri
 
Mkuu nimesafiri kikazi Mtwara/Ndanda, nimeshuhudia kwa macho yangu sister wa kanisa Katoliki ndiye muhudumu wa bar, yani ni mradi wake na yeye anahudumia.
Ushasema mradi wake Sio Wa Kanisa
 
Juzi mzee wa Upako amesema "kufa maskini Tanzania ni Ufala"
Ndio "" alikuwa ana maanisha utakufa vipi masikini " wakati dunia imejaa wajinga kibao " ambao huwa wanatumiwa kama mtaji wa warevu ""...
 
Watu Wangu Wanaangamia Kwa Kukosa Maarifa

Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Kiatu Cha Muumini Sori Imekwisha
Cha Prophet Sori Soft Anatembea Kwenye Kiyoyozi Na Waumini Wanahaha Juani

*Kanisa Linajengwa Na Waumini Likikamilika Ni Mali Ya Prophet Na Ndiyo Anaamua Lolote
hahahaa hiyo Aya ya mwisho nimecheka Mnooo"" ....kwahiyo waumini huwa wanapanda miti ya matunda kwenye shamba la mchungaji ""....
 
Juzi mzee wa Upako amesema "kufa maskini Tanzania ni Ufala"
Huu msemo nadhani waumini wake hawakuulewa. Yaan anawaambia waumini wake kua wao ni mrad maalumu wa kumtajirisha yeye.. n wao hawaoni.
 
Kuna dada mmoja Namfahamu, Alifanya kazi takriban miaka 18, Na alikuwa kitengo Kizuri, lakini alikuwa ni mtu Wa starehe na kuvionga Vibenten akaja kufukuzwa kazi mwaka 2014 mpk sasa hajapata kazi kapigika kisawasawa ubaya hakujenga Kwa kukaa hana . Sasa anauza mafuta ya upako 15000. Ananunua olive oil 4000 . Anauza 15000 anasema Hayo Mafuta ukipaka Ukiwa unaenda kuomba kazi au interview ushapata.......
Hahahahaha amepata njia ya kutokea.
 
Siku hizi kuna mtindo umezuka mtaani hasa Jijini Dsm !

Kun manabii wanauza maji na mafuta ya kupaka yaliyoombewa kwa waumini wake. Unakuta maji chupa moja inauzwa TZS 15.000 na mafuta ya kupaka huuzwa mpaka TZS 50.000.

Watu wananunua sana hizo products. Na hao watumishi wa MUNGU wanapiga sana biashara mjini.

Mifano halisi ni hawa ambao wana Television zao au wanalipia matangazo yao moja kwa moja.

Kama Mch. Suguye na Mzee Wa Upako.

Mwenye ushuhuda wa maajabu au uponyaji alioupata atupatie tafadhari!

Hizi ni placebos..

Hakuna tofauti na wachawi

Waongo wakubwa!

Niggaz will never learn!
 
Mimi kila siku huwa nasema mambo ya kiroho tujitahidi sana kuyachambua au kutafuta tafakuri yake kiroho, vitu vingine si vya kubeza kama wachangiaji wengine wafanyavyo. Ni ukweli usiopingika kwamba kwenye hivi vitu(faith tools) kuna wengine ambao wamefanya ni biashara(fursa). Nitoe mfano mmoja sigara imaeandikwa ni hatari kwa afya yako tena walioandika ni watengenezaji sasa kama ni hatari kwa afya kwa nini wanatengeneza, kwa sababu wameona kuna fursa ya ambao hawajui au wanajua wanaamua tu kuvuta basi kwa sababu kuna vitu wanapata.

Sasa kwenye maji yaliyoombewa kuuzwa hiyo siwezi kusema kwa nini yanauzwa na wasiyatoe bure kila mtu anafanya kwa kadri alivyoongozwa na Muumba wake. Je imani yako iko wapi? Mana sijui kama kuna mahali wanalazimisha watu wanunue! hiyo ni maamuzi ya mtu binafsi kutokana na imani yake kama vile ambavyo mtu unapoenda kununua bia au wine yako ukanywa, sijawahi kuona mahali wamelalamika ,sasa kama mtu kanunua maji ya upako hayajamsaidia hiyo ni shida yake na imani yake hiyo ni baina yake na Mungu wake sisi ni akina nani kuanza kuingilia mahusiano ya kiroho baina ya mtu na Mungu wake.

Narudi sasa upande wangu binafsi ushuhuda wangu huu Mungu aliyonitendea kupitia Morning water ya TB Joshua , hii naisema wazi na ni baina yangu Mungu wangu na Mungu wa TB Joshua.
Miaka ya nyuma kidogo nilianza kusumbuliwa na ndoto mbaya mbaya za kutisha ambazo zilinifanya nikawa nakosa raha mpk wakati mwingine naogopa kulala, nilikuwa nikilala mara nitaota niko mochwari naosha maiti za watu nisiowajua ninalia sitaki naogopa lakini hakuna wakunihurumia, siku nyingine naota nasugua madro yale ya mochwari mara nadeki mochwari, mara naota naona kaburi niko juu yake nalia sana kiukweli hizi ndoto zilinitesa sana na wakati huo maisha yangu yalikuwa nayashuka kwa mwendo wa hatari kazi sina kwenye kazi hapa ndo usiseme nilisikia kitu kinaniambia acha kazi nikaacha bila sababu mwenyewe sikuelewa ndi stori ndefu sana but siku moja rafiki yangu akaona this is not normal yeye alienda kwa TB Joshua akapewa maji kwa vile aliniona nina hali mbaya akaniuliza kama nina imani kuwa Mungu anaweza yote, nikamjibu ndiyo wakati huo hakuna kanisa ambalo sijakanyaga bila suluhu. Nilifanyiwa maombi yote mpk nikakaribia kukata tamaa sijui nifanye nini tena. Siku hiyo rafiki yangu akanipa hayo maji na vitabu vingi tu alivyopewa huko akaniambia nisome kwanza vitabu alafu nikishajengeka kiimani ndo niyatumie mana aliona nilikuwa nimeshakata tamaa na nikasema sitaenda kwa mganga yoyote kama Mungu umeacha kunisaidia basi nimakubali chochote kinachokuja ni sawa ingawa usiku nikiingia kitandani naanza kulia nawaza nikifa nitawaachaje watoto wangu..........nitaendelea mkiniruhusu
Kaka mm naomba fungua Uzi wako tuta kufollow humu hauta onekana!!!
 
Yesu hadi anaondoka hakujenga kanisa Wala hakuwA Na Biblia yaani gombo la chuo Sasa hivi majengo ya Ibada yanatakiwa Na watu wanatakiwa kuwa Na vitabu vya dini Tajiri gani Tanzania unayemjua anayefanya yote wawili yaani kujenga majengo ya kuabudia nchi nZima Na kugawa vitabu vya Ibada ikiwemo Biblia nchi nZima
SOMA MATENDO YA MITUME 17:24-25
Andiko hilo linatamka wazi kuwa Mungu hakai ktk majengo yaliyojengwa kwa mikono ya wanadam wala haitaji chochote kutoka kwa wanadamu,
Usibadili utaratibu aliouacha Yesu kwa kisingizio cha "wakati huu"...Yesu hana wakati yeye ni yule yule jana leo na kesho,YESU ALISALI POPOTE NA ALIUBIRI POPOTE!
 
Yesu alikuwa ndiye Biblia sababu yeye ndie alikuwa biblia yenyewe ndie neno mwenyewe.Tatizo la Tanzania watu wengi hawajielewi hasa viongozi wa dini.Kla moja akomae kwa kile mungu alichomwitia kakuita uhubiri bila kukusanya sadaka endelea na utaratibu wako usikurupukie kuongelea wa mwingine,umeamriwa ukakusanye pesa kusanya hata kwa mjane SOMA Biblia 1 wafalme 17:7-16 Eliya aliamuriwa akachukue sadaka kwa mjane maskini wa kutupwa ingekuwa leo mtu kama wewe ungebwata kuwa sio sahihi!!!! wewe angalia wito wako.waweza sema wahubiri bure na hutaki sadaka na usipate muumini hata mmoja mwingine anasema mimi bila mtu kunipa laki moja asije kanisani kwangu ukakuta anajaza watu maelfu kuliko wewe mhubiri bure uliyepata bure na unatoa bure ukijaribu kuiga kusema basi mimi nashusha nitatoza elfu kumi tu unakuta hata waumini wachache ulionao wana kukimbia sababu hujaamriwa na Mungu!!! Kila mtu afanye kadri ya alivyoagizwa na Mungu na asihangaike na mwingine kuwa anauza rozali,mafuta au maji ya upako au anabusisha watu misalaba na kuwapaka au kuwauzia kinyesi cha wanyama wa Israel .Maswala ya imani ni mazito shika ulichonacho na hangaika na cha kwako
 
Hakuna mijitu milofa duniani kama myeusi....naunga mkono hoja ya Kanye West kuwa waafrika tulipenda pia kuwa watumwa kwa kukosa fikra...mnawezaje ku'dump akili zenu zote kwa pimbi mmoja?ndio maana ilikuwa rahisi ku-be colonized coz waafrika walijidai kkuijua na kuihusudu bible kama waliiandika wao....idiots!!!!
Aliyekudanganya wanaopigwa kwa staili hyo ni watu weusi pekee nani ?.hii style ya upigaji imeanzia kwa wazungu,tembea uone.no research no right to speak coon.
 
Mimi kila siku huwa nasema mambo ya kiroho tujitahidi sana kuyachambua au kutafuta tafakuri yake kiroho, vitu vingine si vya kubeza kama wachangiaji wengine wafanyavyo. Ni ukweli usiopingika kwamba kwenye hivi vitu(faith tools) kuna wengine ambao wamefanya ni biashara(fursa). Nitoe mfano mmoja sigara imaeandikwa ni hatari kwa afya yako tena walioandika ni watengenezaji sasa kama ni hatari kwa afya kwa nini wanatengeneza, kwa sababu wameona kuna fursa ya ambao hawajui au wanajua wanaamua tu kuvuta basi kwa sababu kuna vitu wanapata.

Sasa kwenye maji yaliyoombewa kuuzwa hiyo siwezi kusema kwa nini yanauzwa na wasiyatoe bure kila mtu anafanya kwa kadri alivyoongozwa na Muumba wake. Je imani yako iko wapi? Mana sijui kama kuna mahali wanalazimisha watu wanunue! hiyo ni maamuzi ya mtu binafsi kutokana na imani yake kama vile ambavyo mtu unapoenda kununua bia au wine yako ukanywa, sijawahi kuona mahali wamelalamika ,sasa kama mtu kanunua maji ya upako hayajamsaidia hiyo ni shida yake na imani yake hiyo ni baina yake na Mungu wake sisi ni akina nani kuanza kuingilia mahusiano ya kiroho baina ya mtu na Mungu wake.

Narudi sasa upande wangu binafsi ushuhuda wangu huu Mungu aliyonitendea kupitia Morning water ya TB Joshua , hii naisema wazi na ni baina yangu Mungu wangu na Mungu wa TB Joshua.
Miaka ya nyuma kidogo nilianza kusumbuliwa na ndoto mbaya mbaya za kutisha ambazo zilinifanya nikawa nakosa raha mpk wakati mwingine naogopa kulala, nilikuwa nikilala mara nitaota niko mochwari naosha maiti za watu nisiowajua ninalia sitaki naogopa lakini hakuna wakunihurumia, siku nyingine naota nasugua madro yale ya mochwari mara nadeki mochwari, mara naota naona kaburi niko juu yake nalia sana kiukweli hizi ndoto zilinitesa sana na wakati huo maisha yangu yalikuwa nayashuka kwa mwendo wa hatari kazi sina kwenye kazi hapa ndo usiseme nilisikia kitu kinaniambia acha kazi nikaacha bila sababu mwenyewe sikuelewa ndi stori ndefu sana but siku moja rafiki yangu akaona this is not normal yeye alienda kwa TB Joshua akapewa maji kwa vile aliniona nina hali mbaya akaniuliza kama nina imani kuwa Mungu anaweza yote, nikamjibu ndiyo wakati huo hakuna kanisa ambalo sijakanyaga bila suluhu. Nilifanyiwa maombi yote mpk nikakaribia kukata tamaa sijui nifanye nini tena. Siku hiyo rafiki yangu akanipa hayo maji na vitabu vingi tu alivyopewa huko akaniambia nisome kwanza vitabu alafu nikishajengeka kiimani ndo niyatumie mana aliona nilikuwa nimeshakata tamaa na nikasema sitaenda kwa mganga yoyote kama Mungu umeacha kunisaidia basi nimakubali chochote kinachokuja ni sawa ingawa usiku nikiingia kitandani naanza kulia nawaza nikifa nitawaachaje watoto wangu..........nitaendelea mkiniruhusu
Mkuu acha hadithi nyingi ktk ukristo hakuna kitu kama maji ya BARAKA, Faith Bracelet au matunda yaliombewa, mafuta ya mzaituni whatsoever... huo ni utapeli na upotevu haijalishi ataufanya papa, kadinari, padiri, Mchungani ,askof Mchungani kiongozi, mtume, nabii au mtume na nabii au mpumbavu yyte huo ni ushetani kama ushetani mwingine.........stop lying to these good pipo humu....

eti kuna watu wanajiita mitume....hahaaa mtume watu wanakufa na ukimwi, kansa, kisukari etc mpigeni barabara....
 
Kama Mch. Suguye na Mzee Wa Upako.

Mwenye ushuhuda wa maajabu au uponyaji alioupata atupatie tafadhari!

Raisi Magufuli alishinhttps://www.eatv.tv/news/current-affairs/jpm-afunguka-kuhusu-rozali-iliyompa-uraisda uraisi kwa kutumia Rozali
Mkuu acha hadithi nyingi ktk ukristo hakuna kitu kama maji ya BARAKA, Faith Bracelet au matunda yaliombewa, mafuta ya mzaituni whatsoever... huo ni utapeli na upotevu haijalishi ataufanya papa, kadinari, padiri, Mchungani ,askof Mchungani kiongozi, mtume, nabii au mtume na nabii au mpumbavu yyte huo ni ushetani kama ushetani mwingine.........stop lying to these good pipo humu....

eti kuna watu wanajiita mitume....hahaaa mtume watu wanakufa na ukimwi, kansa, kisukari etc mpigeni barabara....
 
Hakuna kitu kama hicho Mungu anaombwa direct au kupitia Jesus hakuna substitute object
 
Back
Top Bottom