Ushuhuda: Madhara mbalimbali ya Vidonge vya Uzazi Wa Mpango

Yanamadhara sana, tulitumia vijiti lkn du, vidamu damu havikomi almost wiki 2 hadi 3, tukaachana navyo, mpango ni kalenda tu.
 
nilipojifungua mtoto wangu wa kwanza niliweka loop nikakaa nayo kwa muda wa mwaka na miezi 8 nikaitoa, ilinifanya niwe na bleed sana takribani siku 7 wakati mwingine damu mbichi kabisa, mume wangu akamuuliza Doctor kwanini inakuwa hivyo doctor akamwambia loop inatoa mimba yaani mimba inaingia lakini haiwezi kukua kwenye mazingira machafu ndiyo sababu ya mimi kubleed kiasi kile nikaitoa, nikanasa mimba baada ya wiki . nikajifungua mwanangu wa 2 akawa anamwaga nje lakini akawa anachoka sana nikaona yanini kutesana!! nikaweka njiti nilishauriwa vizuri na doctor na madhara yake pia ikiwemo kuumwa kichwa kwa siku za kwanza na kukosa kubleed kwa muda wa miezi hata 3 inategemea na mtu kwani inazuia yai kupevuka, nikaweka nashukuru Mungu haikunidhuru na nilipotoa nikanasa tena ujauzito wa 3 mwezi uliofuatia,, na sasa ndiyo ninayotumia. vidonge na sindano sijawahi kutumia Shangazi yangu Doctor aliniambia siyo vizuri haswa Sindano kwani sindano imewadhuru wengi na wengine walichukukua muda mrefu kupata tena ujauzito. so mi naona inategemea na mtu. na aina ya njia anayotumia.
 
Contraceptives, by their nature, encourage unhealthy attitudes about sexuality.
They encourage COMPROMISE on responsibility, commitment, respect: in short, on REAL LOVE
Mfano tu, they encourage promiscuity.
To everyone I speak, liberal or conservative, these facts are obvious.
Yet this viewpoint is never presented in the media.
Never.
Maybe kuna sera ya kukaa kimya?
Au Viongozi wanashindwa kutofautisha udhaifu binafsi kama tayari ameshatumbukia, na anaona uvivu kubadilika, VS sera bora za kujenga taifa?
 
duuuh kweli aya mavidonge na sindano ni hatari me nina rafki yangu kachoma sindano tkea mwezi wa tatu mpka leo ajaona ck sake anataka arudi tena hospitali akacheki tatizo nn
 
Huo ndo ukweli na sio kutishana....Sidhani kama hao wazungu wanatumia hayo makitu..Na kama wanatumia basi zao sio kama hizi tunapewa huku dunia ya 3. Turudi tu kwenye asili na tuache ujuaji mwingi.

Dear ZD, wazungu ndo watumizi wakubwa hii kitu na wao wanaanza katika umri mdogo zaidi, though madhara wanayoyapata ni makubwa maana kwa nchi ya holland wana tatizo la kukosa watoto hivyo kujikuta wazee wengi ukilinganisha na young generation... Kwa sisi ambao tunaweza kuona athari inayokuja mbele yetu ni bora kuepukana nayo kabla mambo hayajaaribika maana ni uaribifu wa mfumo mzima wa maisha na haileti amani katika jamii. Poleni kwa mliowahi kupata madhara, mi sijawahi hata kufikiria kutumia njia hizi za kisasa ni kalenda mwendo mdundo
 
Members wa JF, natoa salaam zangu kwenu na nafurahi kujiunga nanyi katika kuhabarishana habari mbalimbali. nikichangia kwenye njia za uzazi wa mpango nawasihi dada/wadogo na mama zangu kuwa makini sana kabla ya kutoa uamuzi ni njia gani watumie. Mi mwenyewe niliwahi kutumia sindano ndani ya kipindi cha miezi mitatu sikupata shida sana, ila nilivyochoma ya pili ilikua balaa tupu! kila kukicha maradhi ya kichwa na tumbo haviishi, nikienda hospital hakuna ugonjwa naambiwa niside effect lakini baada ya dawa kuzoea mwilini vitaisha. ila nilivyoona miezi sita imeisha sikurudia tena! nikaamua kutumia kalenda sasa mambo yako murua!
 
Nimegundua wengi humu ni wauwaji (Aborter). Hiyo kitu ya kufuata kalenda ambayo wadau wengi wameelezea kua wanatumia ni wizi mtupu. Mizunguko ya kina mama wengi haiko uniform. akipata stress kidogo tu teyari tarehe zishajichanganya. Na huwezijua kama zimepalaganyika mpaka aone haingii tena mwezini. yaani kusema ishanasia. Enhe unategemea solution yake ni nini kama sio kwenda kuabort?
Daaah dunia hii!
 
duh,inaonekana watu wanaumia sana na haya madubwana!!tumieni calendar jamani,is the best way ever
 
Nimegundua wengi humu ni wauwaji (Aborter). Hiyo kitu ya kufuata kalenda ambayo wadau wengi wameelezea kua wanatumia ni wizi mtupu. Mizunguko ya kina mama wengi haiko uniform. akipata stress kidogo tu teyari tarehe zishajichanganya. Na huwezijua kama zimepalaganyika mpaka aone haingii tena mwezini. yaani kusema ishanasia. Enhe unategemea solution yake ni nini kama sio kwenda kuabort?
Daaah dunia hii!

We ndo muuaji ambaye umezoea ku abort wenzio kama we huwezi tumia kalenda bora unyamaze.gfsonwin hebu njoo uone watu wanavyotia kichefuchefu
 
Ili la kufuata technolojia limenifanya nikumbuke ile debate ya kutahiri vitoto vichanga...ukimuuliza mtu sababu hana hata reference ya mkubwa alowahi fanyiwa hivyo bila madhara haipo...ni mwendo wa liwalo na liwe;

Ikija kwenye masuala ya mwili na afya...sifanyi majaribio aise..never.

kikubwa mie naona ni watu tusipende kuifanyia majaribio miili yetu.

Kuna watu wanakimbizana na teknolojia kama inavyokuja bila kujipa muda wa kupima madhara.

Bora nizae watoto 50 kuliko kutumia njia za uzazi hizi za kisasa.
 
Back
Top Bottom