Je, ni kweli kutumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa muda mrefu kunasababisha kupata watoto wenye homoni za kike kupita kiasi?

SOVIET UNION

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
455
1,283
IGWEEEE

Wakuu kuna wakati ni kipindi cha nyuma sana nikiwa kidato cha 6 tuliwahi pewa semina haikuwa rasimi sana na ilikuwa inahusu swala la vidonge au Sindano za Uzazi wa Mpango.

Jamaa alituambia Vidonge/ Sindano za uzazi wa mpango zina madhara makubwa sana kuliko Faida zake na hata watawala wanajua hilo sema sasa ndio mambo ya Kwa hisani ya watu wa Marekani.

Sikumbuki kama alisema ni aina zote za sindano au vidonge ila alisema endapo Mama atatumia Vidonge au Sindano kwa muda mrefu sana my be 10 years na baadae akaja kubeba ujauzito kuna tabia hizo sindano na Vidonge vinazalisha Homoni nyingi sana za Kike mwilini mwa mtumiaji.

Sasa endapo mtumiaji akaja kubeba ujauzito na ikitokea kajifungua mtoto wa Kiume, possibility ya mtoto kuwa na homoni nyingi za kike ni kubwa sana na kila mtu anajua kifuatacho endapo mtoto wa kiume anazaliwa na Homoni nyingi za kike.

Na endapo sasa mtoto aliezaliwa ni wa kike, hapo pia ni mtoto kuwa na homoni zaidi za kike na hii hupelekea kibinti miaka 8 matiti yalisha chomoza na yanakaribia kulala kabisa, Binti anakuwa na homoni zaidi za kike ambazo humpelekea kupevuka mapema sana na kuanza utu uzima mapema sana.

Hii habari nilikuja tena kukutana nayo sehemu, inazungumzwa, ingawa sijawahi prove so sijui ukweli ni upi ila humu kuna weza kukawa na wadau wanajua zaidi haya mambo.

========

Taarifa hii imefanyiwa kazi kwenye Jukwaa la Jamii Check. Soma: Matumizi ya Muda mrefu ya Dawa za uzazi wa Mpango husababisha kuzaa watoto wa Kiume wenye homoni za Kike
 
Kitu chochote artificial, kina madhara. Hizo family planning methods ndio sijawahi kuziamini
 
Kibaya zaidi kinachoonekana kwa macho ya kawaida ni wanawake watumia dawa hizo kuwa na unene usio wa lishe, tumbo kuwa na kitambi na kukosa hamu ya kuchakatana. Wengine hizo dawa zikiwakataa wanakonda mpaka matako na matiti yanaishiwa nyama wanakuwa na maumbo ya ajabu.

Kuhusu kuzaa watoto wenye homon nyingi za kike hili ni la kitaalam zaidi, wataalam wa tiba na dawa wanaweza kuthibitisha bila woga wa kusema ukweli
 
kwanza wanawake watumia hizo dawa ni wahuni, wanatumia hizo dawa ili kujamiana na wanaume wengi bila kupata mimba zisizotarajiwa. Mwanamke wa ndoa anazuia nini wakati yuko ndani ya ndoa na ndoa lazima izae watoto?

Kama watoto wengi hawatakiwi ni jukumu la baba kuvaa kondom ili kuzuia hizo mimba zisizotakiwa amlinde mke wake asitumie dawa za uzazi wa mpango ambazo kimsingi zina madhara japo haisemwi waziwazi side effect. Kama vipi wazazi watumie njia salama kukwepa kupata idadi ya watoto wasiowataka.

Mwanamke anawezaje kutumia dawa za uzazi wa mpango wakati akiamua kutofanya mapenzi inawezekana? Mtu hajaolewa lakini anajaza sumu hizo mwilini mwake na kujitakia madhara
 
Yeah niliwahi kusikia kuwa kabla yA kubeba mimba inabid mwanamke kuna dawa atumie ili kubalance hormone..sasa wengi hawalijui hili..maana kama mwanamke alitumia dawa mda mrefu bila kutumia dawa za kubalance hormone,,basi akizAa mtoto wa kiume jua umeleta bomu la baadae..those secret societies are so stratergic...watu hawafikirii kwanini jamaa wanalazimisha nchi ikubali ushoga,ila hawalazimishii watu kua
Mashoga.??!! Wanajua how vitu watawapea ili wanaume wawashwe
 
Back
Top Bottom