Ushuhuda: Freeman Mbowe ni kiongozi dhaifu

Ushuhuda: Freeman Mbowe ni kiongozi dhaifu

Kama mpentekoste! Sikubaliani na kauli za kuita watu zombie na wajinga.Shoza katubu siasa isikupeleke jehanamu.Mimi ni ccm damu hapo umepotoka.


Siku hizi wachawi nao wanajinasibu kama walokole ili waaminike kwenye jamii .
Ni chui wanaojivika vazi la kondoo.
Siamini kwamba huyo dada kwa sasa ana amani kweli moyoni kama sio kufurahia pesa na posho za ubunge.

Hakuna chama hapa Tanzania ambacho Mwenyekiti ananyooshewa kidole.
Vyama vyote vinaendeshwa kibabe.
Siasa za Kiafrika zinahitaji mara nyingine ubabe mana watu wanakimbilia siasa kama ajira ya kupata fedha hivyo ukicheka na kila mwanachama anavyotaka kimtizamo wake basi unaangamiza chama.
 
So what? Wewe uko CCM bado unajitetea dhidi ya Ufukuzwaji wako CHADEMA? Mbowe ni dhaifu. Sawa Tunakubaliana na wewe Mbowe ni dhaifu. Naomba nijibu maswali yafuatayo:
1. Kwanini udhaifu wa Mbowe unaifanya CHADEMA inaendelea kuka kwa kasi kwa kupata idadi ya KURA za Urais, idadi ya wabunge, madiwani na mameya.
2. Kwanini udhaifu wa Mbowe unamyima usingizi Mh.Rais wa Tanzania mpaka anawafungia Mbowe na wenzake kufanya mikutano? anamuhofia dhaifu?
3. Kwanini udhaifu wa Mbowe unawafanya watu shupavu kama wewe Shonza, Zito na wenzako kuondoka CHADEMA?
4. Kwanini ninyi mashupavu mliofukuzwa CHADEMA mlishindwa kumuondoa Mbowe kwenye uenyekiti wa Chama cha CDM?
5. Kwanini ninyi mlio mashupavu msianzishe chama chenu cha Upinzani na kuonyesha udahaifu wa Mbowe kwa kuipiku CHADEMA?
Majibu Tafadhali


Hivi ubunge wake ni wa mezani au wa jimboni?

Huko aliko anaweza kumkosoa mwenyekiti wake hata wa kijiji kweli.


Anafikiri kuwa tumesahau kuwa wasomi ndio waliotumika kuua NCCR Mageuzi.
Wamejaribu sana Chadema lakini kwa Mbowe wamegonga mwamba.

Huyo dada kwa kweli anadhalilisha sana wasomi wa dunia hii.

Anashindwa kujua tu kuwa kama JK angeminya demokrasia kama anavyofanya JPM hata yeye leo asingefahamika popote.

Demokrasia na uhuru wa mawazo wakati wa JK ungeminywa tusingewapata watu kama akina Zito, Kitilya ,Mnyika,Mtatiro na wengine wengi. Sasa yeye anahangaika na Mbowe wakati hakuna fursa ya kuibua vijana na wazee wenye uwezo zaidi. Yani anataka Mbowe naye ahamie CCM ili akaelekezwe cha kusema.

Ajifunze kwa Ester Bulaya aliyekataa kuburuzwa kule CCM.
 
Hapa ndio mwisho wa fikra zako, no wonder ni miongoni mwa waliolishwa ule unga wa ndele. Ipo siku zitakujia fikra sahihi na utajikomboa katika minyonyoro iliyokuzunguka ya utumwa wa fikra.
Juliana Shonza nakupenda sana love sana kipenzi wangu.... Any way niyaache ya nyuma bali mama jiepushe na manen kama Mazombie... Sijuwi nini hapa baado tuna maisha baada ya hapa duniani baada kifo.. Kumbuka aliyetuumba alituita watu wangu.. Binadamu .... Tafakari love

FE.
 
Hivi hii mada iliishaje. .?
Maana sijajua conclusion, mbowe amekiri au ameamua kufungua kesi dhidi ya shonza.
 
Jina: JULIANA SHONZA

Kabila: Mnyiha wa Mbozi

Elimu: Shahada ya Uzamili (Masters on Sociology) – Shahada ya Uzamivu ( Phd – UDSM) on progress.



U must feel sorry for what u have as a leaders huko kwenu opposition, maana kama isingelikuwa kwa juhudi za watawala Tanzania would stink and sink..!!
....hakika hii masters ON sociology ni ya Dar rapid transit
 
Tumejua sasa ya kuwa:
1.Umeolewa na una umri wa miaka 30
2.Ni mbunge wa viti maalumu na mkazi wa Songwe.
3.Una masters,na unaendelea na masomo ya Phd(Japo usomi wako,hauendani na kiwango chako cha akili na ufahamu)
Wale wasomi wa vyuo vikuu wanajua,kuna GPA za ........kama sura inalipa.
4.Wewe ni mu FPCT usiye na nidhamu wala roho ya kusamehe(umejaza chuki ndani yako)
5.Mwisho,jibu maswali uliyoulizwa:
--Kama Mbowe ni dhaifu,ninyi watu shupavu ilikuwaje mkashindwa kumn'goa?
--Kama Mbowe si kiongozi mzuri,mbona upinzani na chama chake vinazidi kuimarika chini ya uongozi wake?
--Wabunge wenzako wa CCM na wazee wa CCM,walimsifu sana Mbowe,kwamba ni kiongozi shupavu na mwenye busara katika bunge lililopita la Makinda,je wao ni wanafiki?
YAJIBU KWANZA HAYO,NITARUDI NIONGEZEE MENGINE MAZITO.
 
Hivi ubunge wake ni wa mezani au wa jimboni?

Huko aliko anaweza kumkosoa mwenyekiti wake hata wa kijiji kweli.


Anafikiri kuwa tumesahau kuwa wasomi ndio waliotumika kuua NCCR Mageuzi.
Wamejaribu sana Chadema lakini kwa Mbowe wamegonga mwamba.

Huyo dada kwa kweli anadhalilisha sana wasomi wa dunia hii.

Anashindwa kujua tu kuwa kama JK angeminya demokrasia kama anavyofanya JPM hata yeye leo asingefahamika popote.

Demokrasia na uhuru wa mawazo wakati wa JK ungeminywa tusingewapata watu kama akina Zito, Kitilya ,Mnyika,Mtatiro na wengine wengi. Sasa yeye anahangaika na Mbowe wakati hakuna fursa ya kuibua vijana na wazee wenye uwezo zaidi. Yani anataka Mbowe naye ahamie CCM ili akaelekezwe cha kusema.

Ajifunze kwa Ester Bulaya aliyekataa kuburuzwa kule CCM.
Unamuita Msomi huyu dada? Huyu ni mwana taaluma. Msomi ni yule anayeweza kujenga hoja za kisomi na si hisia au umbeya na propaganda. Kama yeye ni msomi angekujna fact au findings detail zikiwa na sample evidence na analysis inayoendana na phenomena yake. Ana masters halafu hajui maana ya research. Aibu!
 
Mkuu umemsahau na Lowasa, tena huyo ushahidi wake anao Mnyika...na Mbowe.....
Nimeandika EL maana yake ni hiyo Edward Lowasa
Ushahidi wa kwanza unatoka kwa kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Mwaikembe na Mh.Sita
Hawa wengine walishadadia tu.
Wana CCM wengi wanapotosha sana tuhuma za Lowasa kwa kusema CHADEMA ndio waanzilishi wa Tuhuma dhidi ya Lowasa wakati sio kweli, waanzilishi wa Tuhuma ni Spika mstaafu Sitta na kamati teule ya bunge ya kipindi hicho
 
Mh Mbowe kapoteza dira na anabaki kufukuza kivuli chake:
1) Hoja zilizomjenga kisiasa km ufisadi zinatekelezwa kwa vitendo na serikali ya sasa.
2) Hana "utashi wa kisiasa" ambapo ni mwananchi kwanza mwanasiasa baadaye, kwa kuogopa kupoteza umaarufu unaoporomoka kwa kasi
3) Umimi unamtawala zaidi ya maslahi ya wanachama na wafuaso wake na Watanzania kwa ujumla wao - Tamko la UKUTA limejaa umimi tu (asikike, aonekane, akwezwe, asifiwe, nk)

Wananchi anaodhani anawawakilisha ati hakuna demokrasia (bungeni, mikutano ya kisiasa) watamwazibu kwa kukinyima kura 2020 chama CHAKE ( kwa kuwa kinakosa sifa ya kuwa cha kisiasa)?
 
dada hongera kwa kusoma PHD..... ila tambua vyama vya siasa vipo na kila mtu anavutiwa namtu au mambo anayosimamia. Pia tambua kuna haki ya mtu kuchagua na kuchagulia ,hivyo basi kwa kuwa watu wameamua kumchagua mbowe kuwa kiongozi wao basi nakushauri utulie ili ikifika wakati wa uchaguzi ni vyema ukamshauri unayetaka awe kiongozi achukue fomu ila isije ikatokea kama yule aliyetangaza atachukua fomu then akakimbia.Kwa kuwa chadema wanamwamini Mbowe waache waishi kwenye nyumba yao. wewe uliyopo nje timiza majukumu yako na pili tunahitaji fikra mbadala kwa ajili ya ukuwaji wa demokrasia.Natutakia masomo mema na Mungu akubariki daima.Kwa imani yako na imani nyingine tunafundishwa kusamehe na kusahau.
Labda utufahamishe ni watu gani hao waliomchagua Mbowe kuwa kiongozi wao, huo uchaguzi ulifanyika lini, na alikuwa anacompete na akina nani?
 
Mpaka huyu mama wa Mbeya kaibuka kweli watakuwa wamepigiana simu wa Lumumba au sasa watakuwa wa Dodoma kuwa mambo magumu njoo msaidie, " Because if u argue with the fool and your knowledge tells that she/he is the fool then your also a fool"
 
Maana naona mbwembwe nyingi za taaluma ndoa ila kwenye ubunge hajasema wakuchaguliwa, viti maalum au kuteuliwa kama muheshimiwa naibu spika
 
Jina: JULIANA SHONZA

Kabila: Mnyiha wa Mbozi

Elimu: Shahada ya Uzamili (Masters on Sociology) – Shahada ya Uzamivu ( Phd – UDSM) on progress.

Ndoa: Nimeolewa

Umri: Miaka 30

Dini: Mkristo wa Dhehebu la Pentekoste

Kazi: Mbunge wa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
====================================================


Kama ilivyoelekeza Sheria, na kwa Matakwa ya Kikatiba ninaanza Andiko langu kwa “Kiapo” ili itakapolazimu maneno yangu ya leo yatumike katika mabaraza ya Sheria na Mahakama kama rejea rasmi.

Maana ya neno “kiapo” kama nilivyolitumia linamaanisha kuwa ni maelezo anayotoa mtu ambayo mtu huyo anaamini kuwa ni sahihi na ya kweli. Na kwa kuwa inakubalika katika Sheria (Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 ya Sheria za Tanzania, kifungu cha 231) kutoa kiapo kwa njia ya maandishi, kama ifuatavyo;

’’Mimi, JULIANA SHONZA, Mtu mzima, Mkristo, Mama wa familia, Mkazi wa Songwe, nikiwa ninaelewa vya kutosha juu ya jambo ninalotaka kulitolea kiapo na hivyo NAAPA kuwa;

NIKIWA NA AKILI TIMAMU BILA KUSHAWISHIWA NA MTU AU KIKUNDI CHA WATU, NAAPA KUWA MAELEZO NITAKAYOYATOA HAPA KUHUSU MHE. FREEMAN AIKAELI MBOWE, (Mb) MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO NI SAHIHI, NA YA KWELI”

Ndugu wana jamvi wenzangu, nikiwa ndani ya kiapo naomba nieleze yafuatayo kuhusu UDHAIFU na UDHALIMU wa NDG. MBOWE, nitajitahidi nielekeze kwa ushahidi wa matukio na kwa ufupi kadri itakavyowezekana.

Nianze kwa kueleza kuwa wengi katika watu wanafahamu (ingawa kuna upotoshaji mkubwa ktk ufahamu huo) kuwa niliondoka / kuondolewa CHADEMA kwa sababu moja tu, nilidiriki kumnyooshea kidole MWENYEKITI MBOWE. Nikikosoa namna ya utendaji wake, nilitia shaka juu ya uwezo, maono, ufundi na maarifa yake katika kumudu aina ya siasa za sasa na hatma ya CHADEMA..nilifanya hivyo kwa maslahi mapana ya CHAMA hicho na NCHI yetu kwa ujumla.

Lakini kama ilivyo kwa viongozi WAOGA (cowards), mkuu wangu huyo (ambae hakuzoea kunyooshewa kidole) aliona nimemtusi, nimemkebehi na nimefanya jambo la kumvua nguo na kumshushia heshima na hakuwa tayari kuvumilia DHIHAKA hiyo..hakuwa tayari kukiri MAKOSA, hakuwa TAYARI kuruhusu UHURU wa kikatiba ulio kwa kila mwanachama wa CHADEMA kutumika, hakuwa tayari kuuona UKWELI, kwa kuwa tu UKWELI huo ulisemwa na JULIANA.

Nitaeleza matukio mawili (kati ya mengi) ambayo nilimkosoa MBOWE na ikawa mwanzo wa mtafaruku baina yetu na baina yangu na CHADEMA.

(a) Mnamo tarehe 16 Mei, 2012; (Kwa maelekezo ya MBOWE) Aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Mhe John Heche alitoa tamko la kumtuhumu Ndg John Magale Shibuda kuwa ni MSALITI kwa kitendo chake cha kutangaza hadharani kuwa atagombea URAIS kupitia CHADEMA mwaka 2015.


Baada ya TAMKO hilo, (nikiwa Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA) nilijitokeza hadharani kumpinga HECHE, na kumkosoa kuwa TAMKO lake halina Baraka za BAVICHA kwani hajamshirikisha Kiongozi yeyote wa BAVICHA na halikupitia vikao rasmi vya kikatiba, hivyo nikasema kuwa TAMKO hilo ni la HECHE na wala sio la BAVICHA, na nikasema kuwa hatuko tayari BAVICHA kutumika na MTU ndani ya Chama kupambana na MTU mwingine.


Mnamo tarehe 26/5/2012, Mnadhimu na Mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA Mhe Tundu Lissu (kwa maelekezo ya Mbowe) akajitokeza hadharani na kusema HECHE yuko sahihi, na kwamba SHIBUDA ni pandikizi na msaliti. Kwa mara nyingine nikapinga hoja ya Lissu iliyonukuliwa kwenye Gazeti la Mwananchi la tarehe 27/5/2012 ukurasa wa 7. Nilisema Mwenyekiti HANA Absolute Mandate ya kuitumia BAVICHA anavyopenda.


(b) Mnamo tarehe 2, february 2013 katika vuguvugu la Mhe Zitto Kabwe kutangaza kuwania UENYEKITI wa CHADEMA na mimi kuhisiwa kuwa ni miongoni mwa wanaomuunga mkono, niliitwa na kutakiwa kujieleza hasa kutokana na hekaya iliyoitwa Ripoti ya Siri ya Mwenendo wa Kisiasa wa Zitto Z. Kabwe ndani na nje ya CHADEMA.


Kwa kuwa niliamini katika kweli, sikushindwa kutamka mbele ya kikao kile ambacho Mhe Baregu alikuwepo, Mbowe mwenyewe alikuwepo na Dr Kitila (akiwa bado CHADEMA) alikuwepo kuwa sina IMANI na uwezo na maarifa ya Mwenyekiti kukivusha Chama katika wakati huu, ni vyema na ni kutokana na utaratibu wa kidemokrasia ndani ya Chama uliokuwepo kikatiba watu wengine waruhusiwe kugombea na ikiwa wanachama wengi watakubali kufanya mabadiliko ya Mwenyekiti, UAMUZI wao uheshimiwe, miongoni mwa wanaotaka mabadiliko hayo ni pamoja na Mimi.

Baada ya Mjadala mrefu, nilijiengua/kuenguliwa CHADEMA kwa jina maarufu la wakati huo la MSALITI, maana kila aliyempinga MBOWE wakati huo na hata sasa aliitwa hivyo.

Baada ya kueleza kwa ufupi matukio hayo mawili yaliyothibitisha udhalimu wa Mbowe wa kutumia mabavu kuendesha Chama na kufanya maamuzi na kuonyesha alivyo Kiongozi Dhaifu, mwenye Woga na asiyejiamini (maana siku zote amekuwa akituma watu badala ya kujitokeza yeye mwenyewe), nirudi katika kadhia ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokutana Juzi na kuunda UKUTA.

Kwanza ieleweke kuwa sio mara ya kwanza CHADEMA kuunda opresheni zisizo na mbele wala nyuma, ila mwaka huu operesheni hii imezidi kuwa ya hovyo kuwahi kufanywa ndani ya CHADEMA..eti ya kuzuia UDIKTETA..Hivi baada ya yoooote aliyoyafanya MBOWE ndani ya CHADEMA anapata wapi authority, ama legitimacy ya kukemea Udikteta..?

Mimi najua kuwa CHADEMA ya sasa sio ile niliyokuwa mimi miongoni mwa Viongozi, maana sisi tulikuwa tunahoji na wakati mwingine kupinga UJINGA na UONEVU ndani ya Chama, hii ni CHADEMA ya ma-ZOMBIE yanayofuata kama WAFU wasio na roho wala maono. Chadema yenye Katibu Mkuu aliyefungwa hatamu, akivutwa kulia anakwenda na akivutwa kushoto ndio unakuwa muelekeo wake, yenye Viongozi wa BAVICHA waoga, wajinga, wasiofikiri, wasiojiuliza, wenye njaa na wanaojali maslahi ya matumbo yao na matumbo ya waliowaweka madarakani.

Ili nifanye thread hii kuwa fupi naomba nifanye marejeo ya Thread yangu ya tarehe 24 february, 2016 yenye anuani Ushauri kwa Jirani: Mbowe must be disposed! na nyingine ni hii Waraka kwa vijana wa UKAWA: Ni wakati wa Mabadiliko hizo nyuzi mbili zinawatosha kabisa kuwa ni hadidu za rejea juu ya mwenendo na tabia zinazoonyesha udhaifu mkubwa wa MBOWE na matendo yake.

Kimsingi, operesheni hii nayo itakufa kifo cha kimya kimya kama ilivyo zingine zilizowahi kutangazwa huko nyuma bila kuacha mafanikio ya aina yeyote, ila kitu cha kipekee sana ambacho nikiri kuwa huko nyuma hakikuwahi kujitokeza ni jina lenyewe la operesheni, inaitwa Operesheni UKUTA...woow, what a brand name..!!!
elimu yetu ilishakufa siku nyingi na huu ndio ushahidi,, abbysuss abbysum invocat!!! shonza
 
Back
Top Bottom