Ushuhuda: Freeman Mbowe ni kiongozi dhaifu

So what? Wewe uko CCM bado unajitetea dhidi ya Ufukuzwaji wako CHADEMA? Mbowe ni dhaifu. Sawa Tunakubaliana na wewe Mbowe ni dhaifu. Naomba nijibu maswali yafuatayo:
1. Kwanini udhaifu wa Mbowe unaifanya CHADEMA inaendelea kuka kwa kasi kwa kupata idadi ya KURA za Urais, idadi ya wabunge, madiwani na mameya.
2. Kwanini udhaifu wa Mbowe unamyima usingizi Mh.Rais wa Tanzania mpaka anawafungia Mbowe na wenzake kufanya mikutano? anamuhofia dhaifu?
3. Kwanini udhaifu wa Mbowe unawafanya watu shupavu kama wewe Shonza, Zito na wenzako kuondoka CHADEMA?
4. Kwanini ninyi mashupavu mliofukuzwa CHADEMA mlishindwa kumuondoa Mbowe kwenye uenyekiti wa Chama cha CDM?
5. Kwanini ninyi mlio mashupavu msianzishe chama chenu cha Upinzani na kuonyesha udahaifu wa Mbowe kwa kuipiku CHADEMA?
Majibu Tafadhali
 
Mi huwa nasema hakuna chama hovyo kama sisimu, inawezekana kbs kukitoa madarakani ila wapinzani haswa chadema wanajichanganya wenyewe. Natoa changamoto moja tuu kwamba pamoja na mazuri anayofanya sasa hivi rais ktk uongozi wake bado mapungufu ni mengi sana ambayo na uhakika mpk 2020 upinzani watakuwa wana point za kuombea kura. Ila binafsi ninachofikiria kwa sasa ni wkt wa upinzani kuacha kwanza kukosoa utendaji wa mhe wala kuugomea na kushinikiza operation UKUTA, ila tuu wanachotakiwa kwa sasa ni kuhimiza upatikanaji wa KATIBA mpya ile ya warioba na nguvu zaidi ilekezwe kwenye kuwa na tume huru ya uchaguzi kbl ya 2020. Mbali na hivyo tunacheza makidamakida
 
Jina: JULIANA SHONZA

Kabila: Mnyiha wa Mbozi

Elimu: Shahada ya Uzamili (Masters on Sociology) – Shahada ya Uzamivu ( Phd – UDSM) on progress.

Ndoa: Nimeolewa

Umri: Miaka 30

Dini: Mkristo wa Dhehebu la Pentekoste

Kazi: Mbunge wa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
====================================================

Kama ilivyoelekeza Sheria, na kwa Matakwa ya Kikatiba ninaanza Andiko langu kwa “Kiapo” ili itakapolazimu maneno yangu ya leo yatumike katika mabaraza ya Sheria na Mahakama kama rejea rasmi.

Maana ya neno “kiapo” kama nilivyolitumia linamaanisha kuwa ni maelezo anayotoa mtu ambayo mtu huyo anaamini kuwa ni sahihi na ya kweli. Na kwa kuwa inakubalika katika Sheria (Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 ya Sheria za Tanzania, kifungu cha 231) kutoa kiapo kwa njia ya maandishi, kama ifuatavyo;

’’Mimi, JULIANA SHONZA, Mtu mzima, Mkristo, Mama wa familia, Mkazi wa Songwe, nikiwa ninaelewa vya kutosha juu ya jambo ninalotaka kulitolea kiapo na hivyo NAAPA kuwa;

NIKIWA NA AKILI TIMAMU BILA KUSHAWISHIWA NA MTU AU KIKUNDI CHA WATU, NAAPA KUWA MAELEZO NITAKAYOYATOA HAPA KUHUSU MHE. FREEMAN AIKAELI MBOWE, (Mb) MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO NI SAHIHI, NA YA KWELI”

Ndugu wana jamvi wenzangu, nikiwa ndani ya kiapo naomba nieleze yafuatayo kuhusu UDHAIFU na UDHALIMU wa NDG. MBOWE, nitajitahidi nielekeze kwa ushahidi wa matukio na kwa ufupi kadri itakavyowezekana.

Nianze kwa kueleza kuwa wengi katika watu wanafahamu (ingawa kuna upotoshaji mkubwa ktk ufahamu huo) kuwa niliondoka / kuondolewa CHADEMA kwa sababu moja tu, nilidiriki kumnyooshea kidole MWENYEKITI MBOWE. Nikikosoa namna ya utendaji wake, nilitia shaka juu ya uwezo, maono, ufundi na maarifa yake katika kumudu aina ya siasa za sasa na hatma ya CHADEMA..nilifanya hivyo kwa maslahi mapana ya CHAMA hicho na NCHI yetu kwa ujumla.

Lakini kama ilivyo kwa viongozi WAOGA (cowards), mkuu wangu huyo (ambae hakuzoea kunyooshewa kidole) aliona nimemtusi, nimemkebehi na nimefanya jambo la kumvua nguo na kumshushia heshima na hakuwa tayari kuvumilia DHIHAKA hiyo..hakuwa tayari kukiri MAKOSA, hakuwa TAYARI kuruhusu UHURU wa kikatiba ulio kwa kila mwanachama wa CHADEMA kutumika, hakuwa tayari kuuona UKWELI, kwa kuwa tu UKWELI huo ulisemwa na JULIANA.

Nitaeleza matukio mawili (kati ya mengi) ambayo nilimkosoa MBOWE na ikawa mwanzo wa mtafaruku baina yetu na baina yangu na CHADEMA.

(a) Mnamo tarehe 16 Mei, 2012; (Kwa maelekezo ya MBOWE) Aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Mhe John Heche alitoa tamko la kumtuhumu Ndg John Magale Shibuda kuwa ni MSALITI kwa kitendo chake cha kutangaza hadharani kuwa atagombea URAIS kupitia CHADEMA mwaka 2015.

Baada ya TAMKO hilo, (nikiwa Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA) nilijitokeza hadharani kumpinga HECHE, na kumkosoa kuwa TAMKO lake halina Baraka za BAVICHA kwani hajamshirikisha Kiongozi yeyote wa BAVICHA na halikupitia vikao rasmi vya kikatiba, hivyo nikasema kuwa TAMKO hilo ni la HECHE na wala sio la BAVICHA, na nikasema kuwa hatuko tayari BAVICHA kutumika na MTU ndani ya Chama kupambana na MTU mwingine.

Mnamo tarehe 26/5/2012, Mnadhimu na Mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA Mhe Tundu Lissu (kwa maelekezo ya Mbowe) akajitokeza hadharani na kusema HECHE yuko sahihi, na kwamba SHIBUDA ni pandikizi na msaliti. Kwa mara nyingine nikapinga hoja ya Lissu iliyonukuliwa kwenye Gazeti la Mwananchi la tarehe 27/5/2012 ukurasa wa 7. Nilisema Mwenyekiti HANA Absolute Mandate ya kuitumia BAVICHA anavyopenda.

(b) Mnamo tarehe 2, february 2013 katika vuguvugu la Mhe Zitto Kabwe kutangaza kuwania UENYEKITI wa CHADEMA na mimi kuhisiwa kuwa ni miongoni mwa wanaomuunga mkono, niliitwa na kutakiwa kujieleza hasa kutokana na hekaya iliyoitwa Ripoti ya Siri ya Mwenendo wa Kisiasa wa Zitto Z. Kabwe ndani na nje ya CHADEMA.

Kwa kuwa niliamini katika kweli, sikushindwa kutamka mbele ya kikao kile ambacho Mhe Baregu alikuwepo, Mbowe mwenyewe alikuwepo na Dr Kitila (akiwa bado CHADEMA) alikuwepo kuwa sina IMANI na uwezo na maarifa ya Mwenyekiti kukivusha Chama katika wakati huu, ni vyema na ni kutokana na utaratibu wa kidemokrasia ndani ya Chama uliokuwepo kikatiba watu wengine waruhusiwe kugombea na ikiwa wanachama wengi watakubali kufanya mabadiliko ya Mwenyekiti, UAMUZI wao uheshimiwe, miongoni mwa wanaotaka mabadiliko hayo ni pamoja na Mimi.

Baada ya Mjadala mrefu, nilijiengua/kuenguliwa CHADEMA kwa jina maarufu la wakati huo la MSALITI, maana kila aliyempinga MBOWE wakati huo na hata sasa aliitwa hivyo.

Baada ya kueleza kwa ufupi matukio hayo mawili yaliyothibitisha udhalimu wa Mbowe wa kutumia mabavu kuendesha Chama na kufanya maamuzi na kuonyesha alivyo Kiongozi Dhaifu, mwenye Woga na asiyejiamini (maana siku zote amekuwa akituma watu badala ya kujitokeza yeye mwenyewe), nirudi katika kadhia ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokutana Juzi na kuunda UKUTA.

Kwanza ieleweke kuwa sio mara ya kwanza CHADEMA kuunda opresheni zisizo na mbele wala nyuma, ila mwaka huu operesheni hii imezidi kuwa ya hovyo kuwahi kufanywa ndani ya CHADEMA..eti ya kuzuia UDIKTETA..Hivi baada ya yoooote aliyoyafanya MBOWE ndani ya CHADEMA anapata wapi authority, ama legitimacy ya kukemea Udikteta..?

Mimi najua kuwa CHADEMA ya sasa sio ile niliyokuwa mimi miongoni mwa Viongozi, maana sisi tulikuwa tunahoji na wakati mwingine kupinga UJINGA na UONEVU ndani ya Chama, hii ni CHADEMA ya ma-ZOMBIE yanayofuata kama WAFU wasio na roho wala maono. Chadema yenye Katibu Mkuu aliyefungwa hatamu, akivutwa kulia anakwenda na akivutwa kushoto ndio unakuwa muelekeo wake, yenye Viongozi wa BAVICHA waoga, wajinga, wasiofikiri, wasiojiuliza, wenye njaa na wanaojali maslahi ya matumbo yao na matumbo ya waliowaweka madarakani.

Ili nifanye thread hii kuwa fupi naomba nifanye marejeo ya Thread yangu ya tarehe 24 february, 2016 yenye anuani Ushauri kwa Jirani: Mbowe must be disposed! na nyingine ni hii Waraka kwa vijana wa UKAWA: Ni wakati wa Mabadiliko hizo nyuzi mbili zinawatosha kabisa kuwa ni hadidu za rejea juu ya mwenendo na tabia zinazoonyesha udhaifu mkubwa wa MBOWE na matendo yake.

Kimsingi, operesheni hii nayo itakufa kifo cha kimya kimya kama ilivyo zingine zilizowahi kutangazwa huko nyuma bila kuacha mafanikio ya aina yeyote, ila kitu cha kipekee sana ambacho nikiri kuwa huko nyuma hakikuwahi kujitokeza ni jina lenyewe la operesheni, inaitwa Operesheni UKUTA...woow, what a brand name..!!!
JULIANA SHONZA PAMOJA NA PhD yako akili zako ni kidogo sana.

1.badala ya kuandika ni jinsi gani serikali itatatua kero za wananchi na wewe utatatua vipi kero za wanasongwe wewe unatuletea upuuzi wako kuhusu kina Mbowe?

2.kama unafahamu kuwa mbowe ni dhaifu na dhalimu kuna haja gani ya wewe kuanza kupoteza muda wako kupambana na mtu dhaifu kwako?

3.kama mbowe ni dhaifu ana madhara gani kwa wananchi mpaka upoteze muda mwingi na akili yako kupambana na mtu dhaifu?

4. Mbowe ni mwenyekiti wa Chadema na wewe ni mwana ccm kwanini usishangilie udhaifu wa mwenyekiti wa CHADEMA ili CCM iendelee kutusua kila uchaguzi kwa kutumia udhaifu wa upinzani?

5. wewe ulishatoka CHADEMA unapata wapi moral authority ya kuongelea masuala ya CHADEMA wakati hayakuhusu?

6. kuna haja gani ya mbunge kupoteza muda kuongelea CHADEMA inayoongozwa na mwenyekiti dhaifu asiye na madhara yoyote kwa chama tawala.?

7 . PhD holder unapata wapi muda wa kufikiria vitu vya kijinga namna hii na kuvileta mbele ya kadamnasi tena kwa kiapo bila hata aibu?

8. pamoja na PhD yako hapo ndiyo level yako ya kufikiri ?

9. madhumuni ya bandiko lako ni nini? kumtukana mbowe ? kujaza saver za jf au ni kupoteza muda?
NYINYI WABUNGE WA SIKU HIZI MNAFIKIRIA KWA KUTUMIA NINI? TUWAAMINI KWA KIPI? UPI MSAADA WENU KWENYE KUTATUA MATATIZO YA WATANZANIA WANAOTESEKA NA UGUMU WA MAISHA HUKO VIJIJINI?
TUMIA KICHWA CHAKO KUFIKIRI SIYO KUBEBA WIG TU
 
Udikteta wa kuwatumbua majizi na wahujumu uchumi leo mnauita udikteta kweli tunaiona rangi halisi ya upinzani tz yaani leo magufuli dikteta kwa aya anayoyafanya tunaitaji kufikili zaidi ya hapa, go go magufuli umewashika mahala pake
 
Kwa hiyo kama Mbowe ni Dikteta na sisi unataka kutuhalalishia Udikteta wa Magufuli?
Sisi tunataka demokrasia kwa mujibu wa Katiba. Kama Katiba inavunjwa hatuna budi kukemea bila kujali ni Magufuli au Mbowe.

Kosa moja halihalishi kosa jingine.
Wewe Shonza ndio weak na unaonesha una personal conflict na Mbowe.
 
Kama mpentekoste! Sikubaliani na kauli za kuita watu zombie na wajinga.Shoza katubu siasa isikupeleke jehanamu.Mimi ni ccm damu hapo umepotoka.
Huyu ndiye aliwafananisha nani na Herode?
 
Jina: JULIANA SHONZA

Kabila: Mnyiha wa Mbozi

Elimu: Shahada ya Uzamili (Masters on Sociology) – Shahada ya Uzamivu ( Phd – UDSM) on progress.

Ndoa: Nimeolewa

Umri: Miaka 30

Dini: Mkristo wa Dhehebu la Pentekoste

Kazi: Mbunge wa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
====================================================

Kama ilivyoelekeza Sheria, na kwa Matakwa ya Kikatiba ninaanza Andiko langu kwa “Kiapo” ili itakapolazimu maneno yangu ya leo yatumike katika mabaraza ya Sheria na Mahakama kama rejea rasmi.

Maana ya neno “kiapo” kama nilivyolitumia linamaanisha kuwa ni maelezo anayotoa mtu ambayo mtu huyo anaamini kuwa ni sahihi na ya kweli. Na kwa kuwa inakubalika katika Sheria (Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 ya Sheria za Tanzania, kifungu cha 231) kutoa kiapo kwa njia ya maandishi, kama ifuatavyo;

’’Mimi, JULIANA SHONZA, Mtu mzima, Mkristo, Mama wa familia, Mkazi wa Songwe, nikiwa ninaelewa vya kutosha juu ya jambo ninalotaka kulitolea kiapo na hivyo NAAPA kuwa;

NIKIWA NA AKILI TIMAMU BILA KUSHAWISHIWA NA MTU AU KIKUNDI CHA WATU, NAAPA KUWA MAELEZO NITAKAYOYATOA HAPA KUHUSU MHE. FREEMAN AIKAELI MBOWE, (Mb) MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO NI SAHIHI, NA YA KWELI”

Ndugu wana jamvi wenzangu, nikiwa ndani ya kiapo naomba nieleze yafuatayo kuhusu UDHAIFU na UDHALIMU wa NDG. MBOWE, nitajitahidi nielekeze kwa ushahidi wa matukio na kwa ufupi kadri itakavyowezekana.

Nianze kwa kueleza kuwa wengi katika watu wanafahamu (ingawa kuna upotoshaji mkubwa ktk ufahamu huo) kuwa niliondoka / kuondolewa CHADEMA kwa sababu moja tu, nilidiriki kumnyooshea kidole MWENYEKITI MBOWE. Nikikosoa namna ya utendaji wake, nilitia shaka juu ya uwezo, maono, ufundi na maarifa yake katika kumudu aina ya siasa za sasa na hatma ya CHADEMA..nilifanya hivyo kwa maslahi mapana ya CHAMA hicho na NCHI yetu kwa ujumla.

Lakini kama ilivyo kwa viongozi WAOGA (cowards), mkuu wangu huyo (ambae hakuzoea kunyooshewa kidole) aliona nimemtusi, nimemkebehi na nimefanya jambo la kumvua nguo na kumshushia heshima na hakuwa tayari kuvumilia DHIHAKA hiyo..hakuwa tayari kukiri MAKOSA, hakuwa TAYARI kuruhusu UHURU wa kikatiba ulio kwa kila mwanachama wa CHADEMA kutumika, hakuwa tayari kuuona UKWELI, kwa kuwa tu UKWELI huo ulisemwa na JULIANA.

Nitaeleza matukio mawili (kati ya mengi) ambayo nilimkosoa MBOWE na ikawa mwanzo wa mtafaruku baina yetu na baina yangu na CHADEMA.

(a) Mnamo tarehe 16 Mei, 2012; (Kwa maelekezo ya MBOWE) Aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Mhe John Heche alitoa tamko la kumtuhumu Ndg John Magale Shibuda kuwa ni MSALITI kwa kitendo chake cha kutangaza hadharani kuwa atagombea URAIS kupitia CHADEMA mwaka 2015.

Baada ya TAMKO hilo, (nikiwa Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA) nilijitokeza hadharani kumpinga HECHE, na kumkosoa kuwa TAMKO lake halina Baraka za BAVICHA kwani hajamshirikisha Kiongozi yeyote wa BAVICHA na halikupitia vikao rasmi vya kikatiba, hivyo nikasema kuwa TAMKO hilo ni la HECHE na wala sio la BAVICHA, na nikasema kuwa hatuko tayari BAVICHA kutumika na MTU ndani ya Chama kupambana na MTU mwingine.

Mnamo tarehe 26/5/2012, Mnadhimu na Mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA Mhe Tundu Lissu (kwa maelekezo ya Mbowe) akajitokeza hadharani na kusema HECHE yuko sahihi, na kwamba SHIBUDA ni pandikizi na msaliti. Kwa mara nyingine nikapinga hoja ya Lissu iliyonukuliwa kwenye Gazeti la Mwananchi la tarehe 27/5/2012 ukurasa wa 7. Nilisema Mwenyekiti HANA Absolute Mandate ya kuitumia BAVICHA anavyopenda.

(b) Mnamo tarehe 2, february 2013 katika vuguvugu la Mhe Zitto Kabwe kutangaza kuwania UENYEKITI wa CHADEMA na mimi kuhisiwa kuwa ni miongoni mwa wanaomuunga mkono, niliitwa na kutakiwa kujieleza hasa kutokana na hekaya iliyoitwa Ripoti ya Siri ya Mwenendo wa Kisiasa wa Zitto Z. Kabwe ndani na nje ya CHADEMA.

Kwa kuwa niliamini katika kweli, sikushindwa kutamka mbele ya kikao kile ambacho Mhe Baregu alikuwepo, Mbowe mwenyewe alikuwepo na Dr Kitila (akiwa bado CHADEMA) alikuwepo kuwa sina IMANI na uwezo na maarifa ya Mwenyekiti kukivusha Chama katika wakati huu, ni vyema na ni kutokana na utaratibu wa kidemokrasia ndani ya Chama uliokuwepo kikatiba watu wengine waruhusiwe kugombea na ikiwa wanachama wengi watakubali kufanya mabadiliko ya Mwenyekiti, UAMUZI wao uheshimiwe, miongoni mwa wanaotaka mabadiliko hayo ni pamoja na Mimi.

Baada ya Mjadala mrefu, nilijiengua/kuenguliwa CHADEMA kwa jina maarufu la wakati huo la MSALITI, maana kila aliyempinga MBOWE wakati huo na hata sasa aliitwa hivyo.

Baada ya kueleza kwa ufupi matukio hayo mawili yaliyothibitisha udhalimu wa Mbowe wa kutumia mabavu kuendesha Chama na kufanya maamuzi na kuonyesha alivyo Kiongozi Dhaifu, mwenye Woga na asiyejiamini (maana siku zote amekuwa akituma watu badala ya kujitokeza yeye mwenyewe), nirudi katika kadhia ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokutana Juzi na kuunda UKUTA.

Kwanza ieleweke kuwa sio mara ya kwanza CHADEMA kuunda opresheni zisizo na mbele wala nyuma, ila mwaka huu operesheni hii imezidi kuwa ya hovyo kuwahi kufanywa ndani ya CHADEMA..eti ya kuzuia UDIKTETA..Hivi baada ya yoooote aliyoyafanya MBOWE ndani ya CHADEMA anapata wapi authority, ama legitimacy ya kukemea Udikteta..?

Mimi najua kuwa CHADEMA ya sasa sio ile niliyokuwa mimi miongoni mwa Viongozi, maana sisi tulikuwa tunahoji na wakati mwingine kupinga UJINGA na UONEVU ndani ya Chama, hii ni CHADEMA ya ma-ZOMBIE yanayofuata kama WAFU wasio na roho wala maono. Chadema yenye Katibu Mkuu aliyefungwa hatamu, akivutwa kulia anakwenda na akivutwa kushoto ndio unakuwa muelekeo wake, yenye Viongozi wa BAVICHA waoga, wajinga, wasiofikiri, wasiojiuliza, wenye njaa na wanaojali maslahi ya matumbo yao na matumbo ya waliowaweka madarakani.

Ili nifanye thread hii kuwa fupi naomba nifanye marejeo ya Thread yangu ya tarehe 24 february, 2016 yenye anuani Ushauri kwa Jirani: Mbowe must be disposed! na nyingine ni hii Waraka kwa vijana wa UKAWA: Ni wakati wa Mabadiliko hizo nyuzi mbili zinawatosha kabisa kuwa ni hadidu za rejea juu ya mwenendo na tabia zinazoonyesha udhaifu mkubwa wa MBOWE na matendo yake.

Kimsingi, operesheni hii nayo itakufa kifo cha kimya kimya kama ilivyo zingine zilizowahi kutangazwa huko nyuma bila kuacha mafanikio ya aina yeyote, ila kitu cha kipekee sana ambacho nikiri kuwa huko nyuma hakikuwahi kujitokeza ni jina lenyewe la operesheni, inaitwa Operesheni UKUTA...woow, what a brand name..!!!

Unaweza ukawa sahihi kwenye allegations zako zote Juliana, lakini wakati mwingine timing ya kuzitoa kwenye public inaweza kuzipa credit au discount allegations kama hizi.
 
Umesema kweli, lakini naendelea kujiuliza wana nini watu hata mioyo yao ikubali kufungwa, wakubali kuwa watumwa na manamba wa fikra na mitazamo. maana watu hawa wamekuwa kama Nanga ya Merikebu, wanasubiri kuzingwa kwa kamba na kuzamishwa majini.

waliwaamini viongozi wa chadema
wakawapa mioyo yao,
wakaamini watawafikisha katika mabadiliko
walipokuwa upande wao waliwatukana sana CCM

walipogundua wamesalitiwa na walichoamini au waliowaamini ni matapeli, wanaogopo kugeuka na kukiri hayo,

wana uchungu na wanaona, bora abaki CDM akiwa na matusi, kelele na kusema kwa nguvu hata katika maneno ya kipuuzi, eti kuwa wa vyama vingine ni muongo na msaliti

wengi wana madonda ya mioyo, wametahiriwa kisaikolojia ( cult)
CDM imekuwa cult
ni sawa na yale makanisa ambayo yanajua kabisa kiongozi wao wa dini 'SIO' ila wanawapenda balaa
wameathirika, kuwaita wafuata upepo ni kuwapendelea, mazombie sawa
 
Udikteta wa kuwatumbua majizi na wahujumu uchumi leo mnauita udikteta kweli tunaiona rangi halisi ya upinzani tz yaani leo magufuli dikteta kwa aya anayoyafanya tunaitaji kufikili zaidi ya hapa, go go magufuli umewashika mahala pake
Udikteta wake ni dhidi ya kuminya deomkrasia. Udikteta wake ni wa kuvunja sheria hata mtuhumiwa ana haki ya kutetewa kabla hajatiwa hatiani. Mhakama pekee ndio iliyopewa mamlaka kikatiba ya kumuhukumu mtu kwamba huyu ni fiasadi sio Rais wala mwenyekiti wa chama chochote.
By the way ni watuhumiwa gani wakubwa wa uhujumu Uchumi nchini wamekamtwa? Ikiwa akina Riz,Chenge, EL, Rostam,Tiba, kalamagi,yona,mramba, mkulo, Mkono, bakheresa,manji mpaka leo wanadunda uraiani
 
Hapa ndio mwisho wa fikra zako, no wonder ni miongoni mwa waliolishwa ule unga wa ndele. Ipo siku zitakujia fikra sahihi na utajikomboa katika minyonyoro iliyokuzunguka ya utumwa wa fikra.

Nitajaribu kwa staha sana kama nilivyojaliwa na Mungu kujibu matusi yako kwa Chadema unayoiita ya Mazombie na wajinga pamoja na Mbowe.
Kwanza kuweka sawa kumbukumbu usitumie neno kujiondoa /kufukuzwa, tumia neno kufukuzwa tuu kwani hukuwahi kujiondoa.

Pili maamuzi ya operation UKUTA nani kakwambia ni ya Mbowe? yale kayatangaza Mbowe kwa niaba ya Kamati kuu na mbele ya Kamati kuu.
Kwa hiyo kwa hicho kiapo chako cha kisanii wale wazee wote wa KK ni wajinga na ma zombie? Unaelewa maana ya neno zombie ulilotumia kuwaita wazee kama Pro Baregu, Lowasa, Pro Safari, Sumaye na wengineo ambao wengi uko nao Bungeni? Pia wapo kina mama watu wazima katika list hiyo ambao uko nao Bungeni, jee unao ujasiri wa kuwa face na kuwaambia nyie ni mazombie?

Heshima inapaswa kutolewa kwa kila mtu, neno ZOMBIE ni tusi kubwa kuliko BWEGE maana zombie ni maiti inayotembea lakini bwege nafuu yake ni mtu hai........Jee hudhani kwa matusi yako wewe ambaye ni verified user kwa watu ulio wataja kwa kiapo unastahili kuchukuliwa hatua za kisheria ili kurudisha heshima ya Jamiiforum?

OMBI:
Wale wanaohusika na sheria hebu oneni ni jinsi gani kuna weza kuwa na kesi ya kimtandao ili kupata rejea nzuri kwa ile kesi ya Arusha ambayo hata Bungeni iliombewa mwongozo. Litakuwa jambo jema kama kesi ya aina ile itaangukia kwa mbunge wakupewa wa CCM
 
Pole mdada, Mbowe alikufanyaje mbona malalamiko hayaishi hapa Jamvini??
 
Back
Top Bottom