Ushuhuda: Freeman Mbowe ni kiongozi dhaifu

Ushuhuda: Freeman Mbowe ni kiongozi dhaifu

Kwa hiyo dada shonza, Heche akimkosoa Shibuda, ni maelekezo ya Mbowe. Ila wewe ukimpinga Heche, siyo maelekezo ya shibuda wala mwingine yeyote?! Lisu akimpinga shibuda, ni maelekezo ya Mbowe, ila wewe tena ukimpinga Mbowe hujatumwa na wapinzani wa Mbowe!!!

Kama wewe kweli ni mtu usiyeelekezwa kama hao unaowatukana hapa, ni wapi umepinga dhuluma na maonevu yanayofanywa na serikali hii dhidi ya wanaoipinga?!

Sikujua na wala sikudhania kuwa kuna mpentecoste anaweza kuwa upande wa watu wale waliozunguka nchi nzima wakiwazushia wenzao magonjwa na vifo!
 
UKUTA inawapa kiwewe magu na ng'ombe zake. Moto wa nchi nzima hawatoweza kuuzima.
 
Jina: JULIANA SHONZA

Kabila: Mnyiha wa Mbozi

Elimu: Shahada ya Uzamili (Masters on Sociology) – Shahada ya Uzamivu ( Phd – UDSM) on progress.

Ndoa: Nimeolewa

Umri: Miaka 30

Dini: Mkristo wa Dhehebu la Pentekoste

Kazi: Mbunge wa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
====================================================


Kama ilivyoelekeza Sheria, na kwa Matakwa ya Kikatiba ninaanza Andiko langu kwa “Kiapo” ili itakapolazimu maneno yangu ya leo yatumike katika mabaraza ya Sheria na Mahakama kama rejea rasmi.

Maana ya neno “kiapo” kama nilivyolitumia linamaanisha kuwa ni maelezo anayotoa mtu ambayo mtu huyo anaamini kuwa ni sahihi na ya kweli. Na kwa kuwa inakubalika katika Sheria (Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 ya Sheria za Tanzania, kifungu cha 231) kutoa kiapo kwa njia ya maandishi, kama ifuatavyo;

’’Mimi, JULIANA SHONZA, Mtu mzima, Mkristo, Mama wa familia, Mkazi wa Songwe, nikiwa ninaelewa vya kutosha juu ya jambo ninalotaka kulitolea kiapo na hivyo NAAPA kuwa;

NIKIWA NA AKILI TIMAMU BILA KUSHAWISHIWA NA MTU AU KIKUNDI CHA WATU, NAAPA KUWA MAELEZO NITAKAYOYATOA HAPA KUHUSU MHE. FREEMAN AIKAELI MBOWE, (Mb) MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO NI SAHIHI, NA YA KWELI”

Ndugu wana jamvi wenzangu, nikiwa ndani ya kiapo naomba nieleze yafuatayo kuhusu UDHAIFU na UDHALIMU wa NDG. MBOWE, nitajitahidi nielekeze kwa ushahidi wa matukio na kwa ufupi kadri itakavyowezekana.

Nianze kwa kueleza kuwa wengi katika watu wanafahamu (ingawa kuna upotoshaji mkubwa ktk ufahamu huo) kuwa niliondoka / kuondolewa CHADEMA kwa sababu moja tu, nilidiriki kumnyooshea kidole MWENYEKITI MBOWE. Nikikosoa namna ya utendaji wake, nilitia shaka juu ya uwezo, maono, ufundi na maarifa yake katika kumudu aina ya siasa za sasa na hatma ya CHADEMA..nilifanya hivyo kwa maslahi mapana ya CHAMA hicho na NCHI yetu kwa ujumla.

Lakini kama ilivyo kwa viongozi WAOGA (cowards), mkuu wangu huyo (ambae hakuzoea kunyooshewa kidole) aliona nimemtusi, nimemkebehi na nimefanya jambo la kumvua nguo na kumshushia heshima na hakuwa tayari kuvumilia DHIHAKA hiyo..hakuwa tayari kukiri MAKOSA, hakuwa TAYARI kuruhusu UHURU wa kikatiba ulio kwa kila mwanachama wa CHADEMA kutumika, hakuwa tayari kuuona UKWELI, kwa kuwa tu UKWELI huo ulisemwa na JULIANA.

Nitaeleza matukio mawili (kati ya mengi) ambayo nilimkosoa MBOWE na ikawa mwanzo wa mtafaruku baina yetu na baina yangu na CHADEMA.

(a) Mnamo tarehe 16 Mei, 2012; (Kwa maelekezo ya MBOWE) Aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Mhe John Heche alitoa tamko la kumtuhumu Ndg John Magale Shibuda kuwa ni MSALITI kwa kitendo chake cha kutangaza hadharani kuwa atagombea URAIS kupitia CHADEMA mwaka 2015.


Baada ya TAMKO hilo, (nikiwa Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA) nilijitokeza hadharani kumpinga HECHE, na kumkosoa kuwa TAMKO lake halina Baraka za BAVICHA kwani hajamshirikisha Kiongozi yeyote wa BAVICHA na halikupitia vikao rasmi vya kikatiba, hivyo nikasema kuwa TAMKO hilo ni la HECHE na wala sio la BAVICHA, na nikasema kuwa hatuko tayari BAVICHA kutumika na MTU ndani ya Chama kupambana na MTU mwingine.


Mnamo tarehe 26/5/2012, Mnadhimu na Mjumbe wa Kamati Kuu wa CHADEMA Mhe Tundu Lissu (kwa maelekezo ya Mbowe) akajitokeza hadharani na kusema HECHE yuko sahihi, na kwamba SHIBUDA ni pandikizi na msaliti. Kwa mara nyingine nikapinga hoja ya Lissu iliyonukuliwa kwenye Gazeti la Mwananchi la tarehe 27/5/2012 ukurasa wa 7. Nilisema Mwenyekiti HANA Absolute Mandate ya kuitumia BAVICHA anavyopenda.


(b) Mnamo tarehe 2, february 2013 katika vuguvugu la Mhe Zitto Kabwe kutangaza kuwania UENYEKITI wa CHADEMA na mimi kuhisiwa kuwa ni miongoni mwa wanaomuunga mkono, niliitwa na kutakiwa kujieleza hasa kutokana na hekaya iliyoitwa Ripoti ya Siri ya Mwenendo wa Kisiasa wa Zitto Z. Kabwe ndani na nje ya CHADEMA.


Kwa kuwa niliamini katika kweli, sikushindwa kutamka mbele ya kikao kile ambacho Mhe Baregu alikuwepo, Mbowe mwenyewe alikuwepo na Dr Kitila (akiwa bado CHADEMA) alikuwepo kuwa sina IMANI na uwezo na maarifa ya Mwenyekiti kukivusha Chama katika wakati huu, ni vyema na ni kutokana na utaratibu wa kidemokrasia ndani ya Chama uliokuwepo kikatiba watu wengine waruhusiwe kugombea na ikiwa wanachama wengi watakubali kufanya mabadiliko ya Mwenyekiti, UAMUZI wao uheshimiwe, miongoni mwa wanaotaka mabadiliko hayo ni pamoja na Mimi.

Baada ya Mjadala mrefu, nilijiengua/kuenguliwa CHADEMA kwa jina maarufu la wakati huo la MSALITI, maana kila aliyempinga MBOWE wakati huo na hata sasa aliitwa hivyo.

Baada ya kueleza kwa ufupi matukio hayo mawili yaliyothibitisha udhalimu wa Mbowe wa kutumia mabavu kuendesha Chama na kufanya maamuzi na kuonyesha alivyo Kiongozi Dhaifu, mwenye Woga na asiyejiamini (maana siku zote amekuwa akituma watu badala ya kujitokeza yeye mwenyewe), nirudi katika kadhia ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokutana Juzi na kuunda UKUTA.

Kwanza ieleweke kuwa sio mara ya kwanza CHADEMA kuunda opresheni zisizo na mbele wala nyuma, ila mwaka huu operesheni hii imezidi kuwa ya hovyo kuwahi kufanywa ndani ya CHADEMA..eti ya kuzuia UDIKTETA..Hivi baada ya yoooote aliyoyafanya MBOWE ndani ya CHADEMA anapata wapi authority, ama legitimacy ya kukemea Udikteta..?

Mimi najua kuwa CHADEMA ya sasa sio ile niliyokuwa mimi miongoni mwa Viongozi, maana sisi tulikuwa tunahoji na wakati mwingine kupinga UJINGA na UONEVU ndani ya Chama, hii ni CHADEMA ya ma-ZOMBIE yanayofuata kama WAFU wasio na roho wala maono. Chadema yenye Katibu Mkuu aliyefungwa hatamu, akivutwa kulia anakwenda na akivutwa kushoto ndio unakuwa muelekeo wake, yenye Viongozi wa BAVICHA waoga, wajinga, wasiofikiri, wasiojiuliza, wenye njaa na wanaojali maslahi ya matumbo yao na matumbo ya waliowaweka madarakani.

Ili nifanye thread hii kuwa fupi naomba nifanye marejeo ya Thread yangu ya tarehe 24 february, 2016 yenye anuani Ushauri kwa Jirani: Mbowe must be disposed! na nyingine ni hii Waraka kwa vijana wa UKAWA: Ni wakati wa Mabadiliko hizo nyuzi mbili zinawatosha kabisa kuwa ni hadidu za rejea juu ya mwenendo na tabia zinazoonyesha udhaifu mkubwa wa MBOWE na matendo yake.

Kimsingi, operesheni hii nayo itakufa kifo cha kimya kimya kama ilivyo zingine zilizowahi kutangazwa huko nyuma bila kuacha mafanikio ya aina yeyote, ila kitu cha kipekee sana ambacho nikiri kuwa huko nyuma hakikuwahi kujitokeza ni jina lenyewe la operesheni, inaitwa Operesheni UKUTA...woow, what a brand name..!!!
Umeeeleza meengi na kueleweka vizuri sana, ila umesahau machache ulivyokutana na Mwigulu hotel moja sinza na kukabidhiwa pesa kwenye bahasha ,
Baadae mkawa mnakuta mara kwa mara hotel mkijifungia ndani zaidi ya masaa sita , sijui mlikuwa mpanga nini chumbani
 
Umesema kweli, lakini naendelea kujiuliza wana nini watu hata mioyo yao ikubali kufungwa, wakubali kuwa watumwa na manamba wa fikra na mitazamo. maana watu hawa wamekuwa kama Nanga ya Merikebu, wanasubiri kuzingwa kwa kamba na kuzamishwa majini.
Juliana

Sitaki kuingia ndani sana kwenye mada yako. Ila nataka nikuombe ufafanue/ujibu yafuatayo:-

Naomba umpinge na mkiti wako wa sasa wazi wazi, kama ulivyofanya huko ulikotoka. Halafu utupatie mrejesho

Pili, naomba nikuulize, hivi ni kwa nn shibuda alitoka ccm, na je unakumbuka kwamba alitangaza pia kugombea urais na kikwete 2010. Na kama unakumbuka, unaoanisha vipi matukio hayo miwili

Tatu unazungumziaje michakato ya Kupata wenye viti wa ccm, na je, ni kwa nn viongozi tu wa ccm ndio wenye kuamua nani awe mkiti kinyume cha matakwa ya wana ccm wenyewe

Mwisho, unaona mbowe hafai kwa sababu na yeye ni dikteta, sawa, je unazungumziaje mchakato wa zanzibar uliompora waziwazi urais maalim seif.
 
naziona kiki za kisiasa kuelekea uchaguzi Wa 2020,
binafs saiz nachek michongo ya pesa tu , na pesa saiz ztakuwa Dodoma , c magu kasema
 
Cdm imeingiliwa na mdudu unaitwa
Fuata mkumbo
Zidumu fikra za Mbowe hatakama ni Ugoro mtupu.
Mtu kama prof.Baregu kuongozwa na

Vijana wengi CHADEMA hawatumii akili kitafakari anayo yaropoka Mwenyekiti wao.

Mbowe Hana uwezo kuiongoza cdm ya sasa
Anatumia ubabe

"Akili ndogo kuongoza Akili kubwa"
Mtu kama profesa Baregu kuongozwa na matamko ya mtu wa form6,inatia mashaka sana
 
Kama umeamua kuandika kiingereza
Anza na malizia kwa lugha hiyo hiyo

Gwajima nani kwanza!!!?




WATANZANIA WANAHITAJI MAENDELEO SIO "UKUTA"
HAWAPAKANI NA SOMALIA
Na Watanzania watapataje Maendeleo Kati Kuna Udikteta? Ebooo!
 
Kama umeamua kuandika kiingereza
Anza na malizia kwa lugha hiyo hiyo

Gwajima nani kwanza!!!?




WATANZANIA WANAHITAJI MAENDELEO SIO "UKUTA"
HAWAPAKANI NA SOMALIA
Kuondoa Udkteta Nayo Ni Hatua Mojawapo Katika Maendeleo, rudi shule ww
 
Mbunge Wa viti maalum Juliana pole sana Dada kama wewe ni mkristo na unasali dhehebu la pentekoste na pia umeolewa kuna haja ya kumrudia Mungu maana andiko lako linaonyesha shetani kakufunga kweli kweli umekuwa MTU Wa kwanini Na chuki shetani amejitahidi sana upate ubunge hili uendelee kufanya dhambi maana umesahau yote mafundisho ya dini Na kuanza kutukana mpaka waliokufundisha siasa na kukufanya ukafika hapo ulipi fika ccm wakauona kwa kuwa unaweza kutumika kuchafua watu kutukana watu kama ulivyowaita wana chadema mazombi ukapata viti maalum nakuombea Mungu akufungue macho uache kutumiwa Na shetani najua ipo siku utatubu ameni Mungu ni mwema
 
Juliana

Sitaki kuingia ndani sana kwenye mada yako. Ila nataka nikuombe ufafanue/ujibu yafuatayo:-

Naomba umpinge na mkiti wako wa sasa wazi wazi, kama ulivyofanya huko ulikotoka. Halafu utupatie mrejesho

Pili, naomba nikuulize, hivi ni kwa nn shibuda alitoka ccm, na je unakumbuka kwamba alitangaza pia kugombea urais na kikwete 2010. Na kama unakumbuka, unaoanisha vipi matukio hayo miwili

Tatu unazungumziaje michakato ya Kupata wenye viti wa ccm, na je, ni kwa nn viongozi tu wa ccm ndio wenye kuamua nani awe mkiti kinyume cha matakwa ya wana ccm wenyewe

Mwisho, unaona mbowe hafai kwa sababu na yeye ni dikteta, sawa, je unazungumziaje mchakato wa zanzibar uliompora waziwazi urais maalim seif.
Thank youu[emoji106]
Nasubiri jibu la PHD holder[emoji2]
 
Ile hali tu ya Mbowe kuwa mwenyekiti wa kudumu dhama hizi ni ishara kwamba Chadema na Mbowe mwenyewe wana matatizo.

Kama wanachadema wanaamini hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuwa mwenyekiti wa chama tofauti na Mbowe basi kelele zao hizi za kila siku ni kazi bure.
Watu ambao chama kinawandaa kuja kuwa viongozi wa juu serikalini iwapo Chadema itashinda uchaguzi wataonekana vipi na wananchi ikiwa watu wameng'ang'ania vyeo? Wanapatikana Vijana wakionyesha uwezo wao wanapewa majina mabaya na kisha kufukuzwa Chadema anabaki Mbowe na vijana wa kuchongwa na yeye.

Chadema kuna matatizo mengi ila tatizo la kwanza na liko wazi ni Mbowe, huyu lazima aondoke ndipo mabadiliko yataanza kuonekana.
Hivi,ukiwa na mpinzani wako anaharibu,au jirani yako usiempenda akiharibu nyumba yake,wewe utafurahia au kusikitika?
Adui muombee njaa,sasa kama CDM ni adui yenu na kwa mujibu wenu ana njaa,kelele yote ya kumuonyeshea chakula kilipo ni ya nini?
 
LKazi ya kuongoza upinzani nchi hii sio lelemama! Kushindana na Ccm kwa nguvu kwa miaka zaidi ya 15 si rahisi. Tujue Ccm wanakila kitu kuweza kumwangusha mpinzani Wake,tumewaona kina Lamwai,Mrema,Cheyo nk. waliojaribu kidogo na kushindwa kikubwa.
Kuna sababu kumpongeza mbowe kwa jitihada kubwa anazofanya kuinua welewa wa wananchi na kuipigania nchi kwa mambo kadhaa. Hatusemi kwamba hakosei lakini impact ya makosa yake haikaribii robo ya impact ya mazuri afanyayo. Pengine huwa anakuwashapu kureact kwakuhofia hila za chama tawala na serikali yenye mkono mrefu.
Mpumbavu Funza hawezi kuona umahiri Huu kwani amepewa kula kutokana na kuwatukana watu wamrengo mwingine. Hana adabu wala chembe ya hekima kuwatusi vibaya wazee,vijana,wamama na wengine walopoteza maisha wakitaka kujenga ushindani Wa kisera nchini.
Msomi uchwara asojua kuitumia elimu yake zaidi ya kujipendekeza kwa kutusi wasiomuunga mkono. Ni aibu kwa taifa kuwa na mtu anayejitanabaisha kuwa msomi lakini anashindwa kutumia usomi huo kuleta mabadiliko chanya kwa taifa,Tena anayetaka kudhihaki na kuziba mawazo ya washindani Wake katika kutafuta mustakhabali wa Taifa letu.
NINAHAKIKA FUNZA UKIMPA CHAMA AKIENDESHE ATASHINDWA KABLA HAKUJAPAMBAZUKA...(funza-mtu apendaye uchafu na hupenda kuishi chooni)
 
Kwa maneno yenu na matendo yenu inaonyesha wazi kuna kitu kinawauma sana huko chadema ,maana waswahili wanasema.

Ukiona unasemwa sana ujue kabisa wewe ni star na matendo uyafanyanyo yanawachoma.

Maana ccm kila siku ni lowasa na mbowe sasa wamewakosea nini?

Kama ni chama chenu mmeachiwa endeleeni na majipu yenu

Ukiona unasemwa sana ujue kuwa wamekukubali
Wahubiri wanamsema sana shetani karibu kila nyumba ya Ibada je shetani ni bora sana?
 
Haha aisee hivi hawa ng'ombe wasiokuwa na mikia wanapata wapi ujasiri wa kufukuza nzi ? Angalia bana huko kuna wenyewe usije ukatolewa jicho pia na kugeuka zombie kama ulivyowaita wengine ,
 
Sasa juli si unatakiwa ufurahi kwa mbowe kua dhaifu kwanini unaumia kiasi ichi? ebu muulize mwenzio yule mtt wa meneja kampeni
 
PhD UDSM anaandika kingereza cha kuunga. Hahaha uzuri si wewe peke yako na wengine nimewashuhudia.UDSM mmapoteza sifa mliyokuwa nayo hapo awali.
 
Back
Top Bottom