Ninadhani yote haya yanasababishwa na umasikini, tamaa ya pesa, kukata tamaa na kutokujiamini. Huduma za hospitali sikuhizi ni gharama sana, kwa mtu mwenye kipato cha kawaida akiwa anaumwa, kufikiria gharama za CT scan, ultrasound, conoloscopy etc, anaona ni heri tu aende kwa wataalamu wa satelight watakaomueleza aliemloga ni nani, mahitaji na makombe, psychologically kwakua anaamini, atajiona anapata nafuu. Bado wengi wetu tunaishi maisha haya ya kubahatisha.
Kuna wale ambao hawana elimu ya uhakika na wanataka kupanda vyeo kazini, hawa nao wako tayari kukopa aende kwenye kamati ya ufundi yule aliyoko pale aondolewe ili yeye apate ulaji. Hii nayo ni pamoja na tamaa na kutokujiamini.
Ninadhani bado tuna safari ndefu ya kuelimishwa na kudumisha huduma za afya. Madaktari na wauguzi wawe pia walimu kwa wagonjwa wao, watumie elimu na ujuzi wao kuelimisha jamii. Kama mtu anaambiwa mke wako ngoma imeitika lakini bahati nzuri wewe haijakupata. Unahitaji kujikinga unapofanya nae mapenzi, jamaa anakazana kuwa mke wangu amelogwa na mimi nitaenda nae hivyo hivyo kwakuwa ni mke wangu.