Ushindi

Ushindi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,085
Mwanafunzi Mtanzania Isaack Ibrahim Emmanuel juzi ameibuka kidedea katika mchezo wa kick boxing baada ya kumpiga KO Mchina Zi xiǎo yún yǔ katika Mjini Jillin.

Isaack ambaye anasomea uhandisi wa Madawa au Pharmaceuticals engineering katika Chuo Kikuu cha Liaoning jijini Shenyang, ameushangaza umati mkubwa wa Wachina kwa kumgaragaza Zi ambaye hajawahi kupigwa hata siku moja.

Mpambano huo wa Kg 60 umempa umaarufu mkubwa Isaack kiasi hata waandaaji wa mapambano wameanza kupigana vikumbo kumtaka acheze mapambano zaidi.

Akiwa na uwezo wa kutumia kwa kasi ya ajabu miguu na mikono yote, wataalamu wa mchezo huo wamemtabiria makubwa kijana huyu wa kutoka mkoani Mwanza.
IMG-20190103-WA0032.jpeg


Jr[emoji769]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom