FULL FIGHT: Pambano kati ya Francis Ngannou vs Tyson Fury

mkushite

JF-Expert Member
Sep 2, 2021
622
1,467
Wanajf, leo kuna pambano kubwa duniani kati ya Mweusi Ngannou na Mzungu Fury. Ni pambano kubwa na la kusisimua.

Wewe kama mpenzi wa ngumi, ushindi unampa nani?

=====

Muktasari:
Leo Oktoba 28, 2023, Mwanamasumbwi Francis Ngannou maarufu "The Predator" anapanda ulingoni kuzichapa na bingwa wa ndondi wa uzito wa juu, Tyson Fury, huko Riyadh, Saudi Arabia.

Dar es Salaam. Leo Oktoba 28, 2023, Mwanamasumbwi Francis Ngannou maarufu "The Predator" anapanda ulingoni kuzichapa na bingwa wa ndondi wa uzito wa juu, Tyson Fury, huko Riyadh, Saudi Arabia.

BBC imeripoti kuwa pambano hilo linaelezewa na mashabiki wa michezo kama moja ya mapambano makubwa ya ndondi ya karne hii, na ni mtihani mkubwa kwa Ngannou.

Hata hivyo, swali ambalo mashabiki wengi wa michezo huu wanajiuliza ni Je, Ngannou ataweza kumshinda Tyson Fury ambaye hajawahi shindwa katika mapambano yake?

Wakati Ngannou ameibuka kutoka katika mchezo unaojumuisha aina zote za mapigano kama vile ndondi, mateke, mieleka, ngumi (MMA); kwa upande wa Fury ni tofauti kwani mwanamasumbwi huyo yeye tangu mwanzo anatumia mikono pekee.

"Kitaalamu itakuwa ngumu kwa Francis Ngannou ambaye amezoea MMA - kukabiliana na bondia bora zaidi duniani," ameeleza Léandre Nzie, mwandishi wa habari wa Cameroon.

Francis Ngannou alizaliwa katika familia masikini. Akiwa mdogo alikutana na changamoto kadhaa katika maisha ambazo zilimfanya kuchukua majukumu ambayo watoto wa umri wake, wasingeweza kuyabeba.

“Nilikuwa na umri wa miaka 10....Baada ya kuondoka nyumbani kwetu, nilienda kwa bibi yangu, Iinibidi kufanya kazi ili kuchangia huduma za nyumbani; kununua mafuta, chakula na kwa masomo kununua vitabu,” ameeleza Ngannou katika kipindi cha mtandaoni cha Joe Rogan.

"Lazima ufanye kazi na hivyo ndivyo nilivyoanza, ingawa kazi hii ilikuwa ya watu wazima, lakini sikukuwa na chaguo jingine," anaelezea bingwa huyo wa zamani wa Ultimate Fighting Championship (UFC).

Francis Ngannou alifanya kazi katika migodi ya mchanga hadi alipokuwa na umri wa miaka 17.

Kadiri umri ulivyosonga, matatizo yaliendelea kurundikana kwenye mabega ya Francis ambaye anataka jambo moja tu: kutimiza ndoto ya kuwa bingwa wa ndondi.

Kwa hiyo aliamua kuhamia Ulaya kwa kusafiri njia inayotumiwa na maelfu ya wahamiaji kwa kuvuka Jangwa la Sahara kisha Bahari ya Mediterania hadi Ufaransa, ambako hakuacha wazo la kujihusisha na ndondi.

Ambapo katika jitihada hizo, alifanikiwa kuingia katika mashindano ya MMA na kuwa bingwa.

BBC imeendelea kuripoti kuwa Ngannou alifaulu kuonyesha ustadi wake wa mieleka wakati wa pambano dhidi ya Mfaransa Cyril Gane na kuubakisha mkanda wake wa ubingwa wa UFC wa uzito wa juu.

Licha ya mafanikio yake, baadaye aliamua kuondoka. "Unajua kwamba mkataba wa UFC unaweza kuwa na vikwazo na huna la kusema." Francis Ngannou alisema wakati anatoa tangazo la kuachana na UFC.

Baada ya kuondoka UFC, alifanikiwa kutia saini Ligi ya Wapiganaji (PFL), shirika jingine la MMA, ingawa ni la hadhi ya chini kuliko UFC.

2015, pambano lake la kwanza UFC: Francis Ngannou alipigana katika pambano lake la kwanza dhidi ya Mbrazili Luis Henrique baada ya kusaini UFC. Alishinda kwa kumpiga KO mpinzani wake katika raundi ya pili.

Kipigo cha kwanza akiwa UFC: Baada ya mfululizo wa ushindi, Francis Ngannou alipigana na Stipe Miocic aliyekuwa akitetea mkanda wake. Ngannou alipigwa katika pambano hilo.

Bingwa wa UFC uzito wa juu: Miaka mitatu baada ya pambano lao la kwanza, Miocic alitaka kutetea taji lake tena dhidi ya Mcameroon huyo. Francis Ngannou alifaulu kumshinda Miocic na kushikilia ukanda wa uzito wa juu.

Pambano lake dhidi ya UFC: Wakati Francis Ngannou alipotangaza kuondoka UFC, baadhi ya watu walishuku kwamba atarudi kwenye ulimwengu wa MMA. Hata hivyo, aliweza kuwanyamazisha baada ya kutia saini mkataba wa kihistoria na PFL.

Akiwa na PFL, Francis Ngannou alipata uhuru aliokuwa ameutaka kutoka kwa UFC. Kuanzia sasa, ataweza kupigana kwenye ndondi - ndoto yake ya utotoni.

Pia atapata sehemu ya faida inayotokana na PFL kwenye hafla anazoshiriki. Mnyama huyo pia ameteuliwa kuwa balozi wa shirika hilo katika bara la Afrika.

Kwa mwandishi wa habari, Francis Ngannou ni nembo kwa vijana wa nchi yake.

"Francis ni kielelezo cha ustahimilivu, ni ishara ya ndoto iliyotimizwa kwa nguvu na mikono yake."

Oktoba 28, Francis Ngannou atatimiza ndoto yake ya utotoni. Anasaidiwa katika maandalizi na lejendari Mike Tyson ambaye pia atakuwa pembeni yake huko Riyadh.

Chanzo BBC
20231029_105335.jpg


Tyson Fury vs. Francis Ngannou | Fight Highlights​

 
Francis anaweza bahatisha knok out ksma atamuotea ngumi nzuri furry.

Kiufundi furry ana nafasi ya kushinda kwa namna anataka yeye, kosa kubwa kama ataruhusu ngumi ya ushundi kutoka kwa predator

Mwisho nasema lolote linaweza kutokea 50/50
 
Francis anaweza bahatisha knok out ksma atamuotea ngumi nzuri furry.

Kiufundi furry ana nafasi ya kushinda kwa namna anataka yeye, kosa kubwa kama ataruhusu ngumi ya ushundi kutoka kwa predator

Mwisho nasema lolote linaweza kutokea 50/50
Mkuu, Tyson Fury huyu huyu ambaye alitwangwa kinu na Wilder na akainuka?
 
What a fight. Hats off kwa Ngannou. Kwenda 10 rounds vs Fury si masikhara.
 
What a fight. Hats off kwa Ngannou. Kwenda 10 rounds vs Fury si masikhara.
Mbali na round ya 3,8,9 na 10 hizo round zingine angekuwa makini angemshinda. Jamaa inaonekana mzuri kuliko hata Wilder
 
Hakika mkuu
Tyson Furry ni sugu
Jamaa alipewa kinu kizito sana lile pambano lake la kwanza na Wilder na akainuka nilishangaa sana na hata wilder hakuamini kama jamaa atainuka huyu Furry ni mvumilivu wa makonde ,mabondia wengi wa sasa wanakosa uvumilivu
 
Sikupata wasaa wa kucheki huu mtanange. Ila naona hapa Tyson Fury kala kiasi kinachokaribiana na $50 million kwa kuingia ulingoni jana!!!!!

Wakati huo, Francis Ngannou amekula zaidi ya $10 million kwa kuingia ulingoni pia. Hapo bado maokoto mengine ya PPV na kadhalika.


Fun fact, Ngannou pambano lake la mwisho UFC mwaka 2018, akitetea mkanda wake dhidi ya Cyril Gane, alikula kama $ 600,000 tuuuuu!!!!! Pia mpunga alokula jana, ni zaidi ya kipunga alokula katika mechi zake 20 za mwisho akiwa UFC.
 
Tyson Fury ameshindikana kabisa. Japo nae Nganou anastahili pongezi maana kuanzia round ya 7 alikua anaonesha kachoka ila bado aliweza kurusha ngumi zilizomtetemesha Fury mpaka wengi tuliamini Fury anaweza kaa
 
Hakika mkuu

Jamaa alipewa kinu kizito sana lile pambano lake la kwanza na Wilder na akainuka nilishangaa sana na hata wilder hakuamini kama jamaa atainuka huyu Furry ni mvumilivu wa makonde ,mabondia wengi wa sasa wanakosa uvumilivu
LIle bomber alilopewa na Wilder lilifanya mpaka familia ya Wilder ikaanza kushangilia wakiamini sasa Fury ndio kwisha habari lakini mwamba aliamka. Fury ni chuma haswaa
 
Back
Top Bottom