Ushawahi Kuwa In Love Lakini Ukashindwa Kusema?

Ushawahi Kuwa In Love Lakini Ukashindwa Kusema?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
19,408
Reaction score
45,799
Umewahi kuwa in love na mtu lakini ukashindwa kabisa kumwambia? ❤️

Ni nini kilikufanya ushindwe kufunguka?

Kwa sisi baby girls, mara nyingi tunaamini ni bora kubaki kimya kuliko kuonekana tunajishusha au kukosa maadili

Au kuhofia tutaonekanaje kwa muhusika na watu wengine

Ndiyo maana wengi huchagua kuficha hisia zao, wakibaki kuonyesha ishara tu huku wakigugumia moyoni

Kama mwanaume hajajiongeza, basi ndiyo hivyo tena🤭

Kwa wanaume, huonekana ni rahisi zaidi kutupia ndoano, ingawa wapo pia ambao ni madomo zege

Na hawa madomo zege hua wananishangaza hivi nyie wanaume kuna ugumu gani kwenye ku tongoza 🤣🤣


Je, umewahi kumpenda mtu kiasi cha falling deeply in love, lakini ukashindwa kumwambia? Uoga wako ulikuwa ni nini?

Kulombana sio anasa

ShesRise_1 ✋️
 
Back
Top Bottom