Wapendwa Salaam.
Nilikuwa na mahusiano na binti mmoja hakika tulipendana sana,nilikuwa najivunia kuwa nae hasa kwenye masuala kadhaa akinisapoti sana kiuchumi, kimawazo na kifamilia uhusiano wetu ulidumu miaka 6, badae tulitengana katika harakati za kutafuta maisha.
Kila mtu alisafiri mkoa mbali namwezake kwakuwa kwao wanakipato kizuri alikuwa ananitumia pesa yakujikimu lakini alikuwa anataka aniongoze kama mtoto wake aliyenizaa ilo sikukubali kuwa mtumwa kwa ajili pesa zake huo ndio ulikuwa mwisho wetu tukiwasiliana tulikuwa lazima tugombane shelia zake sikuziweza, kila mtu akaamua kushika njia yake, nikafuta namba zake nikajitaidi kumsahau nikaanza maisha mapya na uhusiano mpya maisha yakaendelea.
Miaka 5 bila mawasiliano ilipita nilishamsahau, ghafla nikapokea simu kutoka kwake anaulizia kuhusu maisha yangu nipo wapi? Nafanya nini? Nimeoa? Nina mtoto? Nikamjibu "hapana" japo sikupenda maswali yake.
Sikupenda kwasababu nilishangaa,nikajiuliza kwanini amenitafuta anataka nini? Ikabidi anisimulie maisha yake tangia tulipo achana mpaka sasa anasema hajawai kufurahia uhusiano wowote baada yangu na anamtoto amezalishwa wamemkimbia hawampi uduma yoyote na mzazi mwenzake japo si tatizo kwake lakini anajuta anatamani turudi kama zamani tufunge ndoa ananiambia yupo tayari kwalolote nitakalo mwambia kwasasa amejifunza vitu vingi amebadilika,ni kama ameotea ivi ninamipango yakuvuta jiko.
Sasa hivi hilo ndio limekuwa ombi lake anaitaji mume wakuishi nae amenichagua anasisitiza nisijali kuhusu mtoto,kipindi hichi cha corona amekuwa msaada sana kwangu ananiwezesha pesa kiasi ata bila kumuomba huwa akiniuliza vitu flani nikimwambia sina nashangaa M-PESA imethibitishwa nimepokea kiasi flani amenitumia.
Binafsi kwasasa yupo niliemchagua kufunga nae ndoa na anamatumaini na mimi tunapendana.
Nipo nawaza nani nimuoe kati yao X-girlfriend au Niliye nae sasaivi?