Ushauri: X-Girlfriend ananiomba nifunge naye ndoa

Ushauri: X-Girlfriend ananiomba nifunge naye ndoa

Umasikini na tamaa ya hela ndo itakufanya umuumize Dada wa watu ulienae sasa, usikubali mtu atumie udhaifu wako kwa faida yake...

Imeisha hio

F@nnยฅ[emoji769]
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Yule mwanamke kwenye tangazo la Vodacom anajua kudekeza mume aiseee..Hadi nimeshtuka! Nilikuwa sijawai ona hili tangazo.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Duuuuh Ila we Jamaa kiboko au unaweza ukawa na tatizo , yaani miaka 6 ya mahusiano bila ndoa kisha miaka 5 huna ndoa huna mtoto , jumla hapo miaka 11 yote unapuyanga na mahusiano tuu, aisee Una tatizo , kuna haja ya kujitafakari mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa na ndoa kuwa na mtoto ni malengo na mamuzi ya mtu na sio kama mtu ana matatizo

121.
 
Kwani wewe ni una clinic ya kulea wenye stress na wapweke ,sema nini demu anajua kabisa your not financial stable ameshajua udhaifu wako unapenda kiyonga,sasa huo mtelezo wa ganda landizi uta ku cost utakuna na thread nyingne humu ya kufanywa mtumwa na mkeo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msimamo wetu kuhusu single mother haujabadirika.. ukioa single mother uwe na uvumilivu siku baba mtoto akitaka kumuona mtoto wake (most likely watatafuta eneo tulivu ili akutane na mtoto wake). Siku baba mtoto akitaka kupasha kiporo ni kama kusukuma mlevi tu.

Mpaka sasa hivi matokeo ya wewe na huyo ex wako ni 3-0 sababu kwanza ana mtoto (mapemzi yote yako kwa mtoto wake kwako anatafuta umsitiri tu) , pili ana pesa.

Halafu weww ni mwanaume pambana upate pesa zako na kama michongo imegoma basi ridhika na unachopata huku ukiongeza juhudi.. hizo pigo za kupokea miamala za maex wako utakuja liwa kiboga siku moja.
 
Hata mimi naona hivyo. Kwa sasa simama kama mwanaume, achana kutishwa na uwezo wake wa pesa after all ameshajifunza na amekua anatafuta mme na wewe ndio ameona ni choice wake. Chukua mke huo achana na woga, cha kwanza mchukue mkae naye mpige mimba muwe na mtoto uku ukisoma tabia zake, ukiona katulia funga ndoa rasmi. Wanawake kuwapata ambao mkaelewana ni wachache huyu mmeshajuana kitabia unaweza kucontrol tabia hiz za kiburi cha pesa. After all sasa hivi ameshakuwa mwoga na ataishi na wewe vizuri akiogopa asikuhudhi ukamuacha

Huyo ex anataka ndoa tu ile afiche aibu yake. Akipata ndoa na pesa zake atakua hashikiki. Huwezi control tabia ya mwenye hela wakati wewe huna kitu.. kama tabia yake ni kuvimba sababu ya hela sasa hivi kaficha makucha tu.. akimuoa show inaanza kama kawaida
 
Wapendwa Salaam.

Nilikuwa na mahusiano na binti mmoja hakika tulipendana sana,nilikuwa najivunia kuwa nae hasa kwenye masuala kadhaa akinisapoti sana kiuchumi, kimawazo na kifamilia uhusiano wetu ulidumu miaka 6, badae tulitengana katika harakati za kutafuta maisha.

Kila mtu alisafiri mkoa mbali namwezake kwakuwa kwao wanakipato kizuri alikuwa ananitumia pesa yakujikimu lakini alikuwa anataka aniongoze kama mtoto wake aliyenizaa ilo sikukubali kuwa mtumwa kwa ajili pesa zake huo ndio ulikuwa mwisho wetu tukiwasiliana tulikuwa lazima tugombane shelia zake sikuziweza, kila mtu akaamua kushika njia yake, nikafuta namba zake nikajitaidi kumsahau nikaanza maisha mapya na uhusiano mpya maisha yakaendelea.

Miaka 5 bila mawasiliano ilipita nilishamsahau, ghafla nikapokea simu kutoka kwake anaulizia kuhusu maisha yangu nipo wapi? Nafanya nini? Nimeoa? Nina mtoto? Nikamjibu "hapana" japo sikupenda maswali yake.

Sikupenda kwasababu nilishangaa,nikajiuliza kwanini amenitafuta anataka nini? Ikabidi anisimulie maisha yake tangia tulipo achana mpaka sasa anasema hajawai kufurahia uhusiano wowote baada yangu na anamtoto amezalishwa wamemkimbia hawampi uduma yoyote na mzazi mwenzake japo si tatizo kwake lakini anajuta anatamani turudi kama zamani tufunge ndoa ananiambia yupo tayari kwalolote nitakalo mwambia kwasasa amejifunza vitu vingi amebadilika,ni kama ameotea ivi ninamipango yakuvuta jiko.

Sasa hivi hilo ndio limekuwa ombi lake anaitaji mume wakuishi nae amenichagua anasisitiza nisijali kuhusu mtoto,kipindi hichi cha corona amekuwa msaada sana kwangu ananiwezesha pesa kiasi ata bila kumuomba huwa akiniuliza vitu flani nikimwambia sina nashangaa M-PESA imethibitishwa nimepokea kiasi flani amenitumia.

Binafsi kwasasa yupo niliemchagua kufunga nae ndoa na anamatumaini na mimi tunapendana.

Nipo nawaza nani nimuoe kati yao X-girlfriend au Niliye nae sasaivi?

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Povu Ruksa Naona watu roho inawatoka baada ya kutaja miamala
Vitu vingine sio za kuleta huku
 
Back
Top Bottom