Ushauri: X-Girlfriend ananiomba nifunge naye ndoa

Ushauri: X-Girlfriend ananiomba nifunge naye ndoa

Ukiona mtanzania anakuomba ushauri jua kaisha hamua tayar hapo anakuwa anataka umuunge mkono juu ya uhamuzi wake kama ikitokea kumshauri tofauti na maamuzi yake atakuona ww ufai na umpendi.

Ushauri oa ulie hamua kumuoa
 
Angekuwa hana pesa wala usingemsikiliza mara mbili
 
Wapendwa Salaam.

Nilikuwa na mahusiano na binti mmoja hakika tulipendana sana,nilikuwa najivunia kuwa nae hasa kwenye masuala kadhaa akinisapoti sana kiuchumi, kimawazo na kifamilia uhusiano wetu ulidumu miaka 6, badae tulitengana katika harakati za kutafuta maisha.

Kila mtu alisafiri mkoa mbali namwezake kwakuwa kwao wanakipato kizuri alikuwa ananitumia pesa yakujikimu lakini alikuwa anataka aniongoze kama mtoto wake aliyenizaa ilo sikukubali kuwa mtumwa kwa ajili pesa zake huo ndio ulikuwa mwisho wetu tukiwasiliana tulikuwa lazima tugombane shelia zake sikuziweza, kila mtu akaamua kushika njia yake, nikafuta namba zake nikajitaidi kumsahau nikaanza maisha mapya na uhusiano mpya maisha yakaendelea.

Miaka 5 bila mawasiliano ilipita nilishamsahau, ghafla nikapokea simu kutoka kwake anaulizia kuhusu maisha yangu nipo wapi? Nafanya nini? Nimeoa? Nina mtoto? Nikamjibu "hapana" japo sikupenda maswali yake.

Sikupenda kwasababu nilishangaa,nikajiuliza kwanini amenitafuta anataka nini? Ikabidi anisimulie maisha yake tangia tulipo achana mpaka sasa anasema hajawai kufurahia uhusiano wowote baada yangu na anamtoto amezalishwa wamemkimbia hawampi uduma yoyote na mzazi mwenzake japo si tatizo kwake lakini anajuta anatamani turudi kama zamani tufunge ndoa ananiambia yupo tayari kwalolote nitakalo mwambia kwasasa amejifunza vitu vingi amebadilika,ni kama ameotea ivi ninamipango yakuvuta jiko.

Sasa hivi hilo ndio limekuwa ombi lake anaitaji mume wakuishi nae amenichagua anasisitiza nisijali kuhusu mtoto,kipindi hichi cha corona amekuwa msaada sana kwangu ananiwezesha pesa kiasi ata bila kumuomba huwa akiniuliza vitu flani nikimwambia sina nashangaa M-PESA imethibitishwa nimepokea kiasi flani amenitumia.

Binafsi kwasasa yupo niliemchagua kufunga nae ndoa na anamatumaini na mimi tunapendana.

Nipo nawaza nani nimuoe kati yao X-girlfriend au Niliye nae sasaivi?
sasa ushaanza kupokea pesa zake alafu unaleta swaga za kuwa una mwingine wa kufunga nae ndoa, nendakwa huyo x ukaolewe ukawe chini ya sheria
 
Bado naendelea kusoma coments zenu za mawazo yenu wachangiaji povu ruksa!
 
Nikuulize kwanza mkuu, wewe unampenda? Na uko tayari kuvumilia na kumnyoosha pindi atakaporudia uchizi wake wa kuku control?

Nijibu ilo alafu nikushauri

In Vino Veritas (In Wine Lies the Truth)
 
Usifanye kosa la kurudia matapishi, kuwa makini usijekujuta baadae.

Angalia hizo pesa zake zisigeuke mtego kwako.
 
Yule mwanamke kwenye tangazo la Vodacom anajua kudekeza mume aiseee..Hadi nimeshtuka! Nilikuwa sijawai ona hili tangazo.
 
Umasikini na tamaa ya hela ndo itakufanya umuumize Dada wa watu ulienae sasa, usikubali mtu atumie udhaifu wako kwa faida yake...

Imeisha hio

F@nn¥[emoji769]
 
Back
Top Bottom