Ushauri: X-Girlfriend ananiomba nifunge naye ndoa

Ushauri: X-Girlfriend ananiomba nifunge naye ndoa

Kama ulimshindwa mwanzo na kuweza kumsahau unataka kumrudia wa nini? Mwanaume siku zote ndio kichwa cha familia na kama unaangalia pesa (Marioo) shauri lako ila kwa kusoma tu kidogo nimegundua una shida na dhiki na unataka sehemu ya kuterezea ndio maana unajifanya kama kuna mapenzi kumbe njaa inakusumbua. Ukimuoa huyo ex utakuja juta baadae. Mwanaume simama na msimamo wako achana na huyo single mother. Wewe ulimshindwa, waliomzalisha wamemshindwa halafu unataka kumrudia tena. Sikio la kufa…...
Kweli kabisa njaa inamsumbua huyu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamnyemelea au tayari umeshamvaa maana hapo alipo anaishi kwa hela ya huyo mwanamke
Aibu sana. Na akikubali kuingia kwe ndoa ajue kaolewa yeye. Atafuata maelekezo ya mume tu. Huwezi kuudumiwa halafu usipewe maelekezo. Huyo dada kamtafuta sababu anahitaji heshima ya ndoa tu na inawezekana kakosa option.
 
Mimi si muumini wa single mother lakini kwa huyo wako nakushauri umuoe huyo x-girl. Huyo anakupenda sanaa usimtose kamanda

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi naona hivyo. Kwa sasa simama kama mwanaume, achana kutishwa na uwezo wake wa pesa after all ameshajifunza na amekua anatafuta mme na wewe ndio ameona ni choice wake. Chukua mke huo achana na woga, cha kwanza mchukue mkae naye mpige mimba muwe na mtoto uku ukisoma tabia zake, ukiona katulia funga ndoa rasmi. Wanawake kuwapata ambao mkaelewana ni wachache huyu mmeshajuana kitabia unaweza kucontrol tabia hiz za kiburi cha pesa. After all sasa hivi ameshakuwa mwoga na ataishi na wewe vizuri akiogopa asikuhudhi ukamuacha
 
Kwanini kama humtaki kumuoa uendelee kutafuna pesa zake . Yaani wewe Una matatizo Sana. Bora ungeacha kuchukua pesa zake ili uwe huru
Wapendwa Salaam.

Nilikuwa na mahusiano na binti mmoja hakika tulipendana sana,nilikuwa najivunia kuwa nae hasa kwenye masuala kadhaa akinisapoti sana kiuchumi, kimawazo na kifamilia uhusiano wetu ulidumu miaka 6, badae tulitengana katika harakati za kutafuta maisha.

Kila mtu alisafiri mkoa mbali namwezake kwakuwa kwao wanakipato kizuri alikuwa ananitumia pesa yakujikimu lakini alikuwa anataka aniongoze kama mtoto wake aliyenizaa ilo sikukubali kuwa mtumwa kwa ajili pesa zake huo ndio ulikuwa mwisho wetu tukiwasiliana tulikuwa lazima tugombane shelia zake sikuziweza, kila mtu akaamua kushika njia yake, nikafuta namba zake nikajitaidi kumsahau nikaanza maisha mapya na uhusiano mpya maisha yakaendelea.

Miaka 5 bila mawasiliano ilipita nilishamsahau, ghafla nikapokea simu kutoka kwake anaulizia kuhusu maisha yangu nipo wapi? Nafanya nini? Nimeoa? Nina mtoto? Nikamjibu "hapana" japo sikupenda maswali yake.

Sikupenda kwasababu nilishangaa,nikajiuliza kwanini amenitafuta anataka nini? Ikabidi anisimulie maisha yake tangia tulipo achana mpaka sasa anasema hajawai kufurahia uhusiano wowote baada yangu na anamtoto amezalishwa wamemkimbia hawampi uduma yoyote na mzazi mwenzake japo si tatizo kwake lakini anajuta anatamani turudi kama zamani tufunge ndoa ananiambia yupo tayari kwalolote nitakalo mwambia kwasasa amejifunza vitu vingi amebadilika,ni kama ameotea ivi ninamipango yakuvuta jiko.

Sasa hivi hilo ndio limekuwa ombi lake anaitaji mume wakuishi nae amenichagua anasisitiza nisijali kuhusu mtoto,kipindi hichi cha corona amekuwa msaada sana kwangu ananiwezesha pesa kiasi ata bila kumuomba huwa akiniuliza vitu flani nikimwambia sina nashangaa M-PESA imethibitishwa nimepokea kiasi flani amenitumia.

Binafsi kwasasa yupo niliemchagua kufunga nae ndoa na anamatumaini na mimi tunapendana.

Nipo nawaza nani nimuoe kati yao X-girlfriend au Niliye nae sasaivi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuuh Ila we Jamaa kiboko au unaweza ukawa na tatizo , yaani miaka 6 ya mahusiano bila ndoa kisha miaka 5 huna ndoa huna mtoto , jumla hapo miaka 11 yote unapuyanga na mahusiano tuu, aisee Una tatizo , kuna haja ya kujitafakari mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1][emoji1][emoji1]Eti anapuyanga Hahahahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dini gani mkuu?
Kama ni Muislamu vuta huyo ulonae then toa gap la miezi kadhaa ivi then vuta mzigo wako wa kitambo.
Kama ni dini jirani endelea kupokea ushauri kwa wadau.
 
Chukua karatasi andika majina, kisha kunja karatasi ufumbe macho kisha uzichanganye halafu uokote moja. Utakayebahatika ndo huyohuyo.
Mambo yasiwe mengi.
 
Huyo dada alijua kosa lililofanya ukamuacha mwanzoni?
Na sasa hivi anavyokusaidia tena pesa, huoni kama ni kosa lile lile linaweza kujakutokea?
Je na yeye akiwa amepatq mtihani wa kutokuwa na pesa unahisi mapenzi yenu yatakuwa na uhai?


Alexander The Great
 
Back
Top Bottom