Ushauri wenu

Habari zenu wanajamvi....Nnampenzi wangu almost 3yrs tangu tuwepamoja..bt hajawai kunipeleka anapoishi hata mara mja na nnapomuuliza ananijibu kuwa"pale ni kwako na ipo cku utaenda na kufulahia na jua kwamba nakupenda na wewe ni kama mke wangu"!!na nnajua kila kitu kuhusu maisha yake ya nyuma kuwa anamtoto na anaishi na mama ake na anapokaa hyo mwanamke wake wa mwanzo na mtot napafahamu...bt tatizo ni kwamba kila nnapomwaleza kuhusu kwenda kwake ananipigisha kalenda....so swali langu ni kwamba je kweli ananipenda kwa dhati kama anavyodai au kunakitu ananificha!na hana mpango na mimi??msaada wenu wanajamvi natumai ushauli na c kejeli.

Sorry, kwa mfano mkitaka kukutana faragha hua mnakutana wapi?
 
deprettyn aidha huyo mtu
  • hana pakukupeleka yaani hana kwake au
  • kwake hajaweka sawa yaani anaona aibu hata kukukaribisha isije kuwa analala kwenye kigodoro chini au
  • hana future na wewe anakutumia tu!!
  • Usisahau kuna asilimia 85% ya kwamba sio mkweli ...So cha kufanya ni ujaribu kuchunguza je ayasemayo ni kweli kuwa anasehemu ana ishi?Na kama anayo je kwanini hakupeleki?Kuna mtu anaishi nae?

Daah!asante kwa ushauli wako and ntaufanyiA kazi thankx
 
Last edited by a moderator:
Achana nae si mwaminifu huyo ilinikuta na pia kuna watu wawili nawajua pia yamewakuta
 
Anakupenda sana huyo ndo maana hakuoneshi kwake ila kwa mkweo mtarajiwa na mama watoto wake. mwaka 1 na nusu utatosha kupafahamu kwake.
 
Anakaa kwao hana kwake,subiri akiwa na kwake atakupeleka,wahenga wanasema subra yavuta kheri eti.
 
Heee! Kwa hiyo huwa mnafanyia "maongezi" wapi?

Miaka 3 hujui anapoishi!!!!!! Mh kweli tupo tofauti.

Vumilia nadhani kwa muda ulovumilia huo basi bado kama miaka 2 upajue kwake. Si unaona ulikotoka ni mbali kuliko unakoenda kuwa mvumilivu

mmh hapo pa "maongezi"!!!!
 
Hapo kuna mambo mengi.Moja,yawezekana kuna mwanaume mwingine anaewezesha mpango mzima wa hapo anapokaa huyo dada.Mbili,yawezekana ana wanaume kadhaa ambao wote anawafanyia mchakato ili hatimaye mmoja ndo apatikane kwa ajili ya ndoa.Kwa maana hiyo ni vigumu kumuonyesha mmoja wenu mahali anapokaa.
 
du! we dada are u serious kweli?miaka 3 hujui apapokaa mpenzi wako?ukiapata ujauzito au tatizo lingine utamtafutia wap? sasa ngoja nikufungue macho,huyo kaka ana mwanamke anaishi nae huko kwake amini usiamini!kama huamini peleleza kimya kimya anapokaa halafu umfanyie suprise uone kama hutomkuta mwanamke mwenzio anapika na kupakua!i halafu usisahau kutuletea mrejesho hapa jukwaani,kila la kheri.
 
ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha

miaka 3 bado unasubiri?

ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom