Ushauri Wangu Kwako Mama Samia Kuhusu Elimu

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,683
hali ya elimu kwa sasa ni mbaya, hilo halina mjadala!

1. Ushindani umegeukia kwenye kufaulisha wanafunzi wote na kufuta 'zero'. Kutokana na hilo, suala la kukutana na lundo la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika ni kawaida huku kwenye masekondari yetu ya kata. Kumkuta mwanafunzi anayeitwa Lamadhani badala ya Ramadhani au Asani badala ya Hasani ni kawaida (mipango hiyo). Sekondari sasa ufundishaji wa masomo ya mkakati (kufuta zero) unaojumlisha somo la kiswahili na elimu ya dini ili watoto wapate 'd' mbili na hivyo kupata cheti umeshika kasi. Ajabu ni kuwa udahili wa vyuoni hauhusishi kabisa somo lolote la dini (watu wanapata sifa za kufaulisha na kupeana zawadi huku future za watoto wetu zikiwa ktk sintofahamu km hivyo). Kinachoumiza zaidi ni kuwa wengi wanaomaliza form four huwa hapo kwenye daraja la nne, tena zile za 'd' mbili au tatu huku moja ikiwa ya dini.

2. Wimbi la watoto kutotaka shule kwa sababu ya 'kutoelewa/kutokuwa na akili' ni kubwa mno. Shule yangu ya kata niliyopo kwa mfano, walipokea wanafunzi 152 wa kidato 1.....taarifa ya juzi wameshaacha 24. Hapo sijazungumzia vidato vingine na miaka iliyopita. Hizi kauli kwamba wazazi wa watoto wakamatwe ni za kiuonevu na kinadharia zaidi na ni kujipa kazi isiyoleta ufanisi. Kiufupi watoto ndo kwanza wanafurahia hali hiyo kwani imewarahisishia uachaji wao wa shule. Watoto watukutu sana.

3. Matokeo na ufaulu sasa ni kizungumkuti tupu. Mtoto mwenye 'd' zake mbili za kiswahili na elimu ya dini eti amefaulu kwenda kidato cha tatu. Shida tupu walahi! Nendeni mkaone walichonacho kichwani hao watoto huko kidato cha tatu. Ukiacha hilo, fuatilieni wengi wa hao waliofaulu kwa division one zao....waambieni hata tu waandike barua kwa mhariri mjionee vituko.

Ushauri wangu:
1. Rudisha ule ufaulu wa wastani kwa kidato cha pili na darasa la saba waachane na upuuzi wa kuchagua tu maswali yote 45 isipokuwa matano tu katika masomo yote.

2. Nashauri darasa la saba wanaopata 'd', 'e' na 'f' pamoja na wale wanaofeli kidato cha pili na wale waliofaulu kwa ufaulu wa division four ya 27 hadi 33 wapelekwe veta wakajifunze ufundi. Au amuru kila mkoa utenge ekari za kutosha (zaidi ya 200) ili yaanzishwe madarasa ya ulimaji wa kisasa wa bustani (au zao lolote kulingana na jiografia ya mkoa husika) na wakapigishwe kambi ya miaka mitatu......nakuapia wakitoka huko utapatikana unafuu wa maisha na utapunguza wimbi kubwa la wakesha mitandaoni wakitukana na kujadili vitu ambavyo ni takataka.

3. Rekebisha huu utaratibu mbovu wa utoaji wa fedha za kujikimu za walimu wapya na hata wale wa zamani kuna haja ya kurekebisha kitu. Inakuaje mwalimu anayeenda kijijini (ambako wengi hawapendi kulingana na changamoto zake) anapata hela kidogo ya kujikimu huku yule wa mini (ambako bila kupewa chochote bado angeomba kubaki) anapewa hela nyingi?!!!! Huu ndo utaratibu sahihi na wa haki kweli wa kummotisha mwalimu huyu anayeelekea Kakonko ndani huko ambako ukilaza nyama asubuhi unakuta imegeuka kuwa maharage?

4. Wataalamu waachwe huru linapokuja suala la elimu......kwakuwa elimu ni maisha basi yapewe userious stahiki. Jiepushe na suala la watu kupika tu taarifa na kulazimisha kuinua ufaulu eti kisa uonekane tu kuwa umewapiku waliotangulia katika suala zima la elimu. Tumeliona sana suala hili hivi karibuni. Takwimu za kufaulu zinapanda tu ili mtu fulani aonekane ni wa kipekee huku ukweli ukiwa kinyume; hapana mama, usipende sifa hizi na acha utaalamu uongee hapa!

Mengine watasema wataalamu wengine lkn tafadhali fanya kitu kunusuru hii elimu......utaacha legacy itakayojipigania yenyewe na siyo ya kupiganiwa na watu!
 
Jipu kumbwa ni waziri wa elimu ndalichako ndo zero kabisa.....huyu mama chifu Hangaya amekua dhaifu kwa mda mfupi tu hata kuapanga safu ya mawaziri ameshindwa, elimu hapa Tz ni janga kubwa sanaa.
 
Nadhani wataalamu wa elimu pamoja na waratibu wa Elimu kuanzia Taifa, Mkoa, Wilaya hadi kata wanapaswa wafanyie kazi ushauri wako ili kuboresha elimu yetu zaidi.

wakuu wa Shule za Misingi na Sekondari pia wanapaswa watimize wajibu wao, kama ikitokea mwanafunzi hajiwezi arudishwe darasa.
 
Jipu kumbwa ni waziri wa elimu ndalichako ndo zero kabisa.....huyu mama chifu Hangaya amekua dhaifu kwa mda mfupi tu hata kuapanga safu ya mawaziri ameshindwa, elimu hapa Tz ni janga kubwa sanaa.
Mi pia hyyu nama ndalichako simulation kabisaaa
 
nadhani wataalamu wa elimu pamoja na waratibu wa Elimu kuanzia Taifa, Mkoa, Wilaya hadi kata wanapaswa wafanyie kazi ushauri wako ili kuboresha elimu yetu zaidi.
wakuu wa Shule za Misingi na Sekondari pia wanapaswa watimize wajibu wao, kama ikitokea mwanafunzi hajiwezi arudishwe darasa.
Kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom