Ushauri Wangu Kwa Serikali Yangu ya Tanzania

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,448
6,312
Mimi kama Mtanzania Naomba kutoa ushauri mdogo Kwa Rais wangu na serikali Kwa ujumla

Kwanza mheshimiwa Rais anafanya kazi mzuri, anaonekana ana ndoto mzuri Kwa tanzania na vision mzuri ya kuleta maendeleo Kwa Sisi watanzania

Changamoto ambayo mm naiona na nataka kushauri ni kwenye upande wa viongozi ambao mheshimiwa Rais amewateua kumsaidia..

Viongozi wengi wamekuwa wazito kujitokeza hadharani na kutoa maelezo ya usahihi pale Jambo linapotokea

Mfano kuna Jambo la mambo ya tozo,
Kelele zimekuwa nyingi Sana, kila mtu anaongea Jambo lake, kwenye mitandao kila mtu anasema lake, kwenye daladala kila mtu anasema lake, mtaani kila mtu anaongea anachokijua yy,

Why mtu mmoja mwenye mamlaka kama ni waziri wa fedha au au katibu mkuu fedha asitoke hadharani akaongea?

Akatoa maelezo na mifano ya kueleweka? Akaulizwa maswali na akajibu? Watu wote wakaelewa faina na hasara?

Msemaji mkuu wa serikali alichokiongea hakijakata kiu ya watanzania yy ameongea kama anaongea na watu 20 Tu wa office yake

Yan mambo yamekuwa ni mengi and no majibu ya uhakika


Nauli za mabasi zimepanda, vifurushi vya simu vimepanda, vyakula vimepanda, Kodi za nyumba zimepanda na watanzania tukiuliza jibu ni vita vya Urusi khaaa! So mpaka vifurushi vya simu navyo ni Kwa ajili ya vita?

Tafadhari Sana mheshimiwa Rais, walazimishe wasaidizi wako kutoka na kuongea hadharani

Wajibu maswali ya watanzania, na sio wakija wanaanza oooh mama anaupiga mwingi, Sisi wote tunajua unaupiga mwingi


Thank you so much
 
Back
Top Bottom