Amani iwe nanyi wakuu:
Kama Mtanzania na mwanachama wa CCM, naomba kushauri kwa yanayoendelea nchini kwetu hasa suala la utekaji, ufisadi, na ukandamizaji wa haki za binadamu,
Ushauri kwa Vyombo vya ulinzi na usalama:
Ninyi mmeapa kuilinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya maadui wa nje na ndani wa JMT ikiwemo na kuishauri serikali dhidi ya mambo mbalimbali ya kiusalama, swali la kujiuliza mikataba mibovu wanayoingia viongozi, rushwa na tuhuma zingine zingi ikiwemo na utekaji na mauaji yanaendelea sio tishio la amani na usalama wa taifa letu?.
Ikumbukwe kwamba ustawi wa jamii ndio msingi wa taifa lolote jamii yenye maalamiko na migogoro jamii hiyo haina ustawi na usalama, kila lenye mwanzo halikosi mwisho leo hii wewe kama mtu uliyeapa kuilinda jamhuri kuna siku utastaafu na kuwaachia wengine swali la wewe kujiuliza unatenda haki kwenye jamii? Na je siku ukitoka madarakani utapenda utendewe haya mnayoyatenda sasa hivi mfano mzuri: Suala la Humphrey Polepole wakati ameshika madaraka alijitahidi sana kutetea, kama angejua baadhi ya sheria na ukandamizaji aliokuwa anautetea ungemtokea puani angeshauri serikali ya wakati ule vizuri, ishini vizuri na wananchi. Haipo sababu ya kulinda masilahi ya mtu badala ya Taifa kwa sasa ninyi mmegeuka kuwa wapambe wa viongozi mafisadi. Kumbukeni serikali inakuja na kuondoka ninyi mtakuwepo fanyeni yale yaliyochini ya viapo vyenu.
Kumbukeni hawa wananchi mnaowaona si lolote kuna siku wataunda jeshi lao watakaloliamini lendeni masilahi ya wananchi na sio viongozi wasio waadilifu.
Kwasasa mtumbwi unaenda mlama kama Taifa lazima atafutwe yona aliweze kutoswa baharini
Ushauri kwa viongozi wa serikali:
Mawazo mbadala hayapigwi rungu na siku zote huwezi kushindana na wakati hakuna aliyewahi kushindana na wakati akafaulu, wasikilizeni wananchi wanataka nini kaeni nchi jitafakalini na kama CCM tujitafakali kwa yanayoendelea kama ni suala la katiba wapeni wananchi katiba, tume huru tendeni haki fanyani kazi kwa masilahi ya wananchi sio ya kwenu. Tukubali tukatae nchi yetu sio ile tuliyoizoea kabla ya oct 2025.
Propaganda na kutumia machawa haitasaidia kamwe, tambue kwa sasa nchi yetu inawananchi wanaojielewa sana propaganda kama za Mwigulu, Kenani, Ali hapi, na viongozi wengine haitabadili chochote. Wananchi pamoja na wanaCCM hatufurahi yanayoendelea na namna viongozi mnayoyafanya. Kuteka na kuua watu wenye mawazo mbadala na ya kwetu haitasaidia.
Mwisho
Tanzania ni ya kwetu sote awe mpinzani, asiye na dini mwenye dini,mchungaji na shekhe wote ni Watanzania haina sababu ya kutekana na kuuana kwa sababu tu mtu kaongea ukweli au katoa maoni tofauti na kile unachotaka kusikia.
Kama serikali kwa nguvu inayotumia kuzuia maandamano, kutafuta wanaoikosoa na kuwachukulia hatua, nguvu hii ingeelekezwa kwenye kutatua migogoro ya wananchi na shida za wananchi taifa lingekuwa mbali badala yake tumeharibu reputation yetu kidunia kwa sababu ya kulinda masilahi ya watu wachache wenye uchu wa madaraka.
"Nitasema ukweli daima, uongo kwangu ni mwiko"