Ushauri wangu kwa Lissu baada ya Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 kutangazwa

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Tundu Antiphas Lissu

Umeona yaliyotokea, kura Watanzania tumepiga ila matokeo yake ndIo hayo. Matokeo yanayotangazwa sio matokeo ya kura zilizopigwa ni matokeo ambao tayari NEC na CCM walikuwa nayo kabla hata ya uchaguzi. Kilichofanyika Jana ni kujaribu kuionesha dunia kuwa kuna uchaguzi wakati hakuna uchaguzi ila washindi walishaandaliwa.

Napenda kukushauri, Watanzania wa Bara sio watu wa kuanza. Ni watu wa kumuona mtu ana anza na wao wanamfuata nyuma. Watanzania wengi wanapenda kuona mfano kwanza then wao ndo hufuata.

Kwa Tanzania ya leo huwezi ku achieve jambo bila kulianzisha mwenyewe. Usione hivi, Watanzania wengi wameumia na huu uhuni uliofanywa na CCM, hao wanaokusema vibaya ni watu wachache sana ambao ndo wana Ccm wenyewe , wengine Tupo na wewe.

Napenda kukushauri jambo moja, kama ni kuaga, ageni familia zenu na ndugu zenu, then wote mtangaze mahali pa kuonana katika maandamano yenu, ifanyike kwenye mikoa yote na muwe serious kwenye hili.

Tangazeni, tarehe ya kufanya haya na muanze kweli. Hata mkianza 2 nawaambia kadri ya muda utakavyokuwa unaenda mtaona watu wanazidi kuongezeka. Najua pia hakuna dunia itakaa kimya ikiona mkifanyiwa unyama

UPDATES:

Hongereni sana Chadema na ACT kwa maamuzi haya ya kuwa na Maandamano yasiyo na ukomo kuanzia jumatatu. Naomba ushauri huu makini uzingatiwe na nguvu zote na tuwe serious kweli kwenye kutekeleza haya.

Viongozi wa upinzani kwenye majimbo na mikoa yote wahakikishe wanatekeleza haya kwa weredi mkubwa.

Tusiogope kabisa. Lolote watakalojaribu kutufanya dunia itawaona na haitowaacha. Wakitupiga na kutuua tutaomba kwa hatua za kijeshi za kimataifa kutulinda waaandamanaji wa amani.

Nazidi kutoa wito. Viongozi wote wa upinzani wakati ni sasa, hakunaga haki inayopewa mkononi, siku zote haki hudaiwa kwa nguvu mpaka inatoka. Tu waambie ndugu zetu na wake zetu, tunafanya haya kwa ajiri ya Tanzania, tunafanya haya kwa mstakabali wa vizazi elfu na elfu vijavyo. Na tunafanya haya kwa maslahi ya watanzania wote.

Tusipopinga kwa nguvu huu udhalimu, nawahakikishia, Ccm na magufuli watawachinja watanzania kama kuku kwenye hii miaka 5 ijayo.

Tutokeni wote kwa nguvu, tukafanye maandamano ya amani ya kupinga ukiukwaji huu wa maamuzi ya wananchi.

OMBI KWA POLISI NA JWTZ

Nyie ndo walinzi wa Watanzania, nyie ndo mnashika silaha kwa niaba ya watanzania. Nyie kama jamii ya watanzania na sehemu ya watanzania mmeona kilichotokea tarehe 28 ambapo kura zilipigwa ila watu wametangaza matokeo yao walioyandaa kabla hata ya uchaguzi. Nyie ni mashahidi na mmeona yote.

Nyie pia mnajua kuwa wapinzani ni watanzania, ni ndugu zenu na ni sehemu pia ya jamii yenu kama watanzania. Maisha ya kuwa magumu kwao ni yapo magumu na kwenu pia, bei ya sukari ilkipanda kwao imepanda na kwenu pia na hata watoto wao wakikosa elimu bora na mikopo au ajira ni watoto wenu pia yamewapata haya.

Ombi langu kwenu.
Vyama vya upinzani vimetangaza kufanya maandamano ya amani kuanzia jumatatu, tarehe 2. Ni maandamano ya haki, kudai kurudiwa kwa uchaguzi na tume huru kufanya uchaguzi huo.

Naomba nyie kama sehemu ya watanzania hawa nanyi muwe sehemu ya kudai haya mabadiliko. Msitekeleze amri zisizo halali na kuwapiga na kuwaumiza watu au hata kuua watu kwa sababu mabadiliko wanayoyadai hayatawanufaisha wao tu bali sehemu nzima ya watanzania na nyie mkiwepo pamoja na vizazi vyenu.

Naomba msikubali amri mbovu na muwalinde watanzania kudai haya mabadiliko kwa amani.

Mungu awabariki.




Asanteni.
 
Nilikwambia WEWE hapo mara nyingi sana humu kuwa Lissu hawezi kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ukanibishia. Ingia barabarani Sasa, Lissu kashatoa tamko mchana huu na video ipo YouTube naye anawasubiri nyie mlianzishe maana ndo mliotemewa mate usoni na tume ya uchaguzi kwa maelezo yake.

Sasa na wewe unamsubiria yeye alianzishe. Ninachojua watu hawana time, atajikuta yeye tu barabarani. Sisi tunawajua watanzania vizuri na tunaijua CCM vizuri mpaka kuwaambia vile na nyie mkashupaza shingo eti NI YEYE.
 
Lissu kishawaambia ingieni barabarani, nyie tena mnataka na yeye awepo? Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha mabavicha bana.

Si mlisema mnasubiri tamko la Lissu? Sasa tena nyie mnataka na yeye awepo?

Nimefurahi sanaaaaaa huku nilipo ni nderemo na vifijo tuuuuu watu wewe

IMG_20201029_150710.jpg
 
Mlisema mnaingia barabarani? Inakuwaje tena mnaogopa makamanda?

Nadhani ni mda wa kutumia vyombo vya nje inabidi tuichafue tanzania haswa tuwekewe vikwazo kama zimbabwe na nchi nyingine si tuna uwezo wa kujitegemea, afu naomba huyu mtu aongeze kodi mara dufu tuone hawa watanzia watalia lia kona zipi, mpaka hela za kununua ARVs zikosekane
 
Akili kama punje ya haradali, kwanza hata hizo kura alizopata amejitahidi sana. Kwa kueneza chuki badala ya sera, ni wapumbavu tu wamepoteza kura zao
Wewe zako kama mharo wa bata acha kuandika kama umebanwa na mavi hao unaowaita wapumbavu ulitaka uwalazimishe wakipigie kura Chama cha Mapinduzi kenge mjane wewe.
 
Tunasubiri tamko mimi mwanamke ila nitakuwa mstari wa mbele kabisa sipendi kuona manyanyaso kwa kweli
Tamko gani tena nyie?? Mbona Lissu kafanya press leo na katoa tamko kuwa muingie barabarani, hakuna kukubali
Au mnataka nani atoe tamko?

IMG_20201029_150710.jpg
 
Nadhani ni mda wa kutumia vyombo vya nje inabidi tuichafue tanzania haswa tuwekewe vikwazo kama zimbabwe na nchi nyingine si tuna uwezo wa kujitegemea, afu naomba huyu mtu aongeze kodi mara dufu tuone hawa watanzia watalia lia kona zipi, mpaka hela za kununua ARVs zikosekane
Wewe ni Mtanzania au mkenya? Kubomoa nyumbani kwako ni sifa?
 
Back
Top Bottom