Ushauri wa bure: Msije Dodoma mnadanganywa sana

Ushauri wa bure: Msije Dodoma mnadanganywa sana

Kiranga mbona unatutisha wana iDodomya hilo ni linini tena Bonde la ufa?
basi hata Upanga litafika kumbe linasogea?
Karibuni Dodoma ingawa kwa Makao makuu naona km ndoto sasa hivi Miji mingi inamegewa mafungu
wale waelekezwa hawaji tena wamebaki watumishi tu, wanaoondoka Ijumaa na kurudi J3
Asante kunikaribisha mkuu, na wewe karibu visiwa vya Turks and Caicos.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kuhamia Dodoma ni moja kati ya mambo kibao yanayohitajika kufanywa, pia ni moja kati ya kitu ambacho ni lazima kufanywa.

Watanzania jifunzeni Kuwa na mtazamo chanya kuhusu maendeleo ya nchi acheni kuwa kama bendera fuata upepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Katika vipaumbele vyote inavyotakiwa kuwa navyo nchi ambayo ina matatizo mengi na haina pesa za kutosha, kwa nini habari ya kuhamisha mji mkuu iwekwe kuwa juu?

Tanzania isingehamisha mji mkuu kutoka Dar kwenda Dodoma ingepungukiwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii purukushani ya kuhamishia Wizara Dodoma imewaadhiri watu wengi sana.
Nyumba bado ni za shida, maji ya shida na changamoto nyingine lukuki.

Sasa sijui mambo yatakuwaje hapo mbeleni.
Wafanyakazi wengi wameziacha familia zao Dar es salaam.
Nimemhurumia sana jamaa yangu, analazimika kurudi Dar kila Ijumaa kwa ajili ya familia.

Wadau mlioko Dodoma kutoka Dar ni changamoto gani nyingine mnazokutana nazo Dodoma?

Poleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Maamuzi ya Mizuka na Kisiasa.
 
Wengine kabla hamjapata kazi Dar mlikuwa mnaishi kwenu huko vijijini gari mnaziona zikileta maiti leo mumepelekwa Dodoma mnalialia kama vipi acheni kazi mrudi kwenu vijijini mkalime mihogo hizi habari za kulialia na Dodoma kila siku zinachosha, Wanaume wanasemaga mara moja tu.
 
Katika vipaumbele vyote inavyotakiwa kuwa navyo nchi ambayo ina matatizo mengi na haina pesa za kutosha, kwa nini habari ya kuhamisha mji mkuu iwekwe kuwa juu?

Tanzania isingehamisha mji mkuu kutoka Dar kwenda Dodoma ingepungukiwa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafikiri ili tuelewane mimi na wewe unatakiwa uweke vipaumbele ambavyo nchi inatakiwa kuwa navyo ambavyo ni tofauti na kuhamia Dodoma.

Mimi nafikiri kuhamia Dodoma ni jambo zuri sababu nchi imekuwa na muunganiko mzuri wa kimaendeleo pia itarahisisha utekelezaji wa mipango ya kimaendeleo katika eneo la usimamiaji utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya nchi katika mikoa mbali mbali ukizingatia Dodoma ni kati Kati ya nchi.

Pia nafikiri watu mmekalili sentensi kuhamia Dodoma kama ni jambo lililogharimu Pesa nyingi, lakini kiuhalisia sijaona jambo kubwa lililofanyika Dodoma ambalo limegharimu Pesa kiasi kikubwa sababu kama Ikulu ya Chamwino, Bunge, ofisi ya waziri mkuu vyote vipo miaka mingi Kabla Magufuli ajawa Raisi ila jambo liligharimu Pesa ni la kuhamisha wizara zote, lakini kama umefika mji wa Kiserikali Dodoma uliopo eneo la Mtumba kwa Aina ya ramani ya zile Wizara na aina ya ujenzi uliofanyika utaamini ni Pesa kidogo sana imetumika katika ule ujenzi na ukizingatia wizara zote Zina Ramani inayofanana kila kitu ukitoa wizara ya Tamisemi yenye Jengo tofauti.
Ikumbukwe wizara zimejengwa na wanajeshi

Ni hivi, mini siongelei kuhamia Dodoma kama mtu ninayekusoma magazetini.

Nimeona bajeti zikipitishwa na kuliwa miaka nenda rudi. Nineona namba zikibadilishwa.

Walioongoza CDA ni watu nawajua kwa karibu sana. Nikiingea nao wananipa malalamiko yao.

Hapa sijui hata kama watu wanajua CDA ni nini.

Nchi zinazoendelea zinatakiwa kuwa na uchaguzi mzuri sana wa vipaumbele. Ili, zianze na miradi inayozalisha kwanza, ili pesa chache za kigeni kabla ya kuwekezwa kwenye projects zisizo na uzalishaji kama kuhamisha mji mkuu, ziwe zimezunguka kwenye uzalishaji.

Kuhamisha mji mkuu hakuna uzalishaji. Ni straight expenditure tu.

Tuanze na vitu vyenye Return On Investment. Kuhamisha mji mkuu hakuna ROI.

Serikali imeingilia biashara ya korosho, imeangusha mapato ya exports za agriculture kwa asilimia 55, kwa mwaka mmoja tu, halafu tunahamisha mji mkuu?

Unasema kuhamisha mji mkuu hakuna gharama, hao watu wanaotoka Dar kwenda Dodoma wanapaa kwa ungo?

Serikali inatakiwa kuweka mazingira mazuri ya biashara, kukusanya kodi, kusambaza huduma za jamii, kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

Serikali inadaiwa madeni kibao, haijalipa wastaafu, haina social benefit network ya kueleweka, haija exploit agri ultural potential to even half, haya yote yangewe,a kufanyika vizuri sana kwa hizi fedha zinazounguzwa kwa ujinga wa kuhamisha mji mkuu.

Mji mkuu ulikuwepo tayari Dar, ume develop kwa biashara, naturally.

Tumeamua kushindana na mji ulioibuka naturally, kwa sisi kutaka gharama nyingi za kujenga mji mkuu tofauti.

Bila ya sababu ya kueleweka.

Na watu wanafurahia.

Unasema kuhamia Dodoma hakujagharimu kwa sababu Bunge na Ikulu vipo Dodoma miaka mingi, hata huelewi kwamba mimi nakosoa hilo jengo la Bunge na Ikulu kujengwa Dodoma.

Hivi unaelewa ninachijadili hapa?

Au unarukia kuhamia Dodoma ndani ya awamu ya Magufuli tu?

Mimi naongelea idea nzima tangu enzi ya Nyerere ilikuwa ujinga mtupu!

Sasa utasemaje Ikulu na Bunge tayaribyapo Dodima? Kwani mwaka 1961 kulikuwa na Ikulu na Bunge Dodoma?

Watu ambao kodi zao zinatumika ku homa mafuta safari za Dodoma, kujenga majengo ambayo tayari yapo Dar.

Ni umasikini wa mawazo. Wa kujitakia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga, Hoja zako dhaifu sana ndugu, nimekuuliza jambo moja je vipaumbele vya nchi vinavyotakiwa ni vipi kwa Sasa ukiachana na kuhamia Dodoma ila haujanijibu?

Umeanza kuongelea Capital Development Authority - CDA ambayo siyo msingi wa Hoja na pia ilishavunjwa hiyo mamlaka.

Pia umesema nchi zinazoendelea zinatakiwa kuwa uchaguzi mzuri wa vipaumbele ili zianze na Miradi inayozalisha kwanza, je vipaumbele vipi vinavyotakiwa kufanywa na nchi Sasa ukiachana na jambo la kuhamia Dodoma?

Umesema unaongelea idea nzima ya kuhamia Dodoma tangu Enzi za nyerere ilikuwa ujinga mtupu, nafikiri wewe umetembea nchi kadhaa,
je unafahamu kwamba nchi zifuatazo zilibadilisha miji mikuu iliyorithi kutoka kwa wakoloni na lengo ilikuwa kurahisisha Utawala wa nchi, ulinzi , kuweka uwiano wa maendeleo ya maeneo ya nchi n.k.
nchi hizo ni Nigeria: Lagos to Abuja, Misri: Cairo to new Cairo, Brazil: Rio de Janeiro to Brasilia n.k

Unasema serikali imeamua kushindanisha dodoma na dar es salaam mji ulioibuka naturally, kwa kifupi hii Hoja yako Haina ukweli.

Nimeeleza kwa kifupi ili turudi kwenye msingi wa Hoja, ni kwamba jambo la kuhamia Dodoma serikali iko sahihi na faida zake ni nyingi sana kama nchi na sio kwa kuangalia mawazo ya wafanyakazi wachache wa serikali wasio taka kuhama dar es salaam sababu ya Mazoea.

Halafu kama bado una Hoja Jaribu kufata mtiririko wa Hoja sio kuruka ruka na maneno Bila mpangilio Mara CDA, Korosho, export za agriculture, exploit agriculture potential, social benefits na mengine kama hayo uliyoongea ambayo sio msingi wa Hoja ambavyo jibu la hayo yote ni kwamba serikali haiwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja.

Hoja ni kwamba kuhamia Dodoma Unasema ni gharama na Unasema serikali ifanye vipaumbele vingine,
Je gharama hizo za serikali kuhamia Dodoma ni zipi na je vipaumbele vingine ambavyo serikali inatakiwa kufanya ukiachana na kuhamia Dodoma ni vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom