Ushauri wa bure kwa Rich Mavoko

Uhai? Mkuu umelewa nini?
Hebu cheki hii feedback
View attachment 444270
Kidogo imeshinda best africa collaboration tizo za AELA
Mkuu ebu tupe mrejesho wa moyo mashine
Sasa kati ya mimi na wewe ni nani aliye lewa? Unaelewa maana ya uhai wewe au umekurupuka kujibu ili uonekana unafanya kazi yako vyema? Hicho ulichoweka hapo ndio uthibitisho wa uhai?
 
mavoko kaanza kuharibu toka asajiliwe huko mavoko alikua anaimba vitu vya maana Leo anaimba kokoro ?
 
Sasa kati ya mimi na wewe ni nani aliye lewa? Unaelewa maana ya uhai wewe au umekurupuka kujibu ili uonekana unafanya kazi yako vyema? Hicho ulichoweka hapo ndio uthibitisho wa uhai?
Lete wewe uthibitisho wa uhai mimi nimekuwekea mrejesho wa uhai wa wimbo
Ni kama umefuga kuku wa mayai mrejesho wa uhai wake ni mayai utakayovuna
 
Kokoro sio neno la Nigeria, nenda pande za pwani utakuta "kokoro" ni ile nyavu ambayo inavyutwa kwa kamba na wavuvi wengi uku wakiwa nchi kavu na nyavu ikiwa majini
 
Richard Mavoko ni mmoja wa waimbaji wazuri sana hapa bongo. Binafsi namkubali sana. Kaka nakushauri tuliza kichwa tunga wimbo mwingine mzuri, wapenzi wako hatujaridhika na wimbo wako wa Kokoro.

Mavoko una nyimbo nyingi nzuri ulizoimba mwenyewe na kushirikishwa ila huu wa sasa mmmmh.
Ni kweli Mavoko ana uwezo mzuri wa kutunga mashairi mazuri, ushahidi ni wimbo wake wa Ibaki Stori - Niwimbo wenye mashairi mengi sana.

- Lakini nyimbo za aina hiyo haziuzi ulimwenguni licha ya kupendwa hapa Tanzania, Mavoko tayari ana jina hapa bongo na anachokiangalia ni soko kubwa zaidi na kwa sababu huko hawaelewi unaimba nini - huwezi kuimba mashairi kibao kama kwenye Ibaki stori .Ndio maana unaona wameimba wenye mashairi mafupi mafupi tena ni wimbo wa burudani tu "Club Banger "

- Hata Diamond bado ana uwezo huo wa kutunga mashairi kama ya zamani ,ushaidi sikiliza matangazo aliyotengeneza yanavyokiki.

- Lakini kwasababu za kibiashara inatakiwa ubadilike badilike ili uuze maana muziki ni biashara huwezi kukommaa na kitu kwa sifa tu wakati huuzi.
 
Back
Top Bottom