Ushauri Usioombwa: Kuingilia Maisha Binafsi

Ushauri Usioombwa: Kuingilia Maisha Binafsi

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
960
Reaction score
808
Wale wachambuzi wa maisha ya watu, wanaopenda kuingilia maamuzi binafsi ya watu kwa ushauri usiohitajitaka wala kuombwa wanasema, “Kuwa na angalau kaulevi kamoja. Inasaidia.”

“Mtu gani unakuwa na maisha perfect and you have everything under control? Unaishije? Pombe zimekushinda. Kahawa nayo inakushindaje?”

Inashangaza sana namna taaluma ya kuingilia maisha ya watu inavyokosa kiasi.
 
Kwa bahati mbaya wabongo ndio tulivyo

Na ukiwa tofauti na maisha yao utaara kuitwa majina mabaya au kuzushiwa sifa ambazo hauna kwa sababu hauishi kama wanavyoishi.

"Huyu kama hanywi pombe atakuwa malaya sana"..

" Mtu gani hapendi kujichanganya na watu, itakuwa ni mchoyo, ana roho mbaya, ana matatizo ya akili, muoga wa watu, mchawi"
 
Wewe mbona unapenda kuingilia maisha ya wengine kwa uchawa wako uliopitiliza? Nenda Kizimkazi huko ukasaidie walioko kwenye Eda zilizofuatana!
 
Back
Top Bottom