miss wa kinyaru
JF-Expert Member
- Aug 28, 2012
- 542
- 356
Kuna rafiki yangu aliwahi kuolewa baadae akashindana na mme wake wakaachana lakini walikuwa wamebahatika kupata watoto wawili, ni miaka nane sasa tangu watengane na mme wake, alikataa kabisa kuolewa tena, japo kuna wanaume mbali mbali walitaka wamuowe alikataa, ni wanaume wengi tu walimfuata wakiwa na nia ya kumuoa alikataa.
Kati yao kuna mmoja tangu mwaka 2010 anamfuatilia alishamtukana alishamjibu majibu yote ya sitaki lakini yule baba hakuacha kusistiza kwamba wewe ndo mke wangu najua ipo siku, huyo baba nae alishaachana na mke wake mwaka ule ule aliotengana na mme wake, kwa hiyo huyo baba nae ana miaka nane sasa yuko single, na yeye ana watoto wawili pia.
Kwenye mwezi wa sita akawa kwenye relationship na baba mmoja ambae nae alikuwa anamfuatilia siku nyingi pia nae alikuwa ameshaachana na mke wake na wakakubaliana hivi wawe pamoja wasomane ili ikiwezekana mwakani mwanzoni waowane, lakini rafiki yangu akaona tabia zao haziendani akamwambia hawezi kuendelea na uhusiano huo, japo huyo baba alilalamika sana.
Mwezi wa tisa akaamua amkubalie yule baba sasa yule baba yeye kila siku alikuwa anaomba aende kwao na rafiki yangu akajitambulishe then ampeleke kwao, yule dada anakataa anamwambia subiri kwanza, kama wiki 2 zimepita yule baba kampigia simu mama yake kwamba anataka kuoa amepata mchumba kwa hiyo siku yoyote atampeleka nyumbani awatambulishe.
Yule mama kafunga safari mpaka kwa kijana, akamwambia hakuna kuoa mwanamke mwingine mrudie aliyekuwa mkeo mimi huyo ndo namtambua maana kila nikipata matatizo huwa yuko na mimi bega kwa bega siwezi kupata mkwe mwingine kama huyo.
Mtoto nae hataki anasema yule dada alikuwa malaya alishamfumania mara kibao, mama anamtetea anasema atakuwa ameshajifunza kwa mda uliomuacha.
sasa huyo baba yuko njia panda lakini anasema hawezi kurudiana na huyo mwanamke yeye lazima amuowe rafiki yangu.
Sasa rafiki yangu alikuwa anaomba ushauri je akubali kuolewa japo mama mkwe hataki au aachane na huyo mwanaume?
japo huyo mwanaume anampenda sana rafiki yangu lakini itakuwaje kwa mama mkwe?