Mkimuyangu
JF-Expert Member
- Oct 5, 2022
- 1,054
- 1,929
Yaani ukisikia inchi inayoongoza kwa vitu vya kipumbavu ni Tanzania, wanashindwa hata kuiga kwa KenyaKwa miaka 60 ya Taifa hili umuhimu wa Mbunge Viti Maalum ni mzigo:
1. Hana eneo analowakilisha( No area of jurisdiction)
2. Analipwa sawa na Mbunge mwenye jimbo ambapo yeye hana wananchi wanaomtegemea.
3. Ubunge wa Viti maalum huzalisha wanawake wanaojipendekeza kwa viongozi wa Chama zaidi kuliko Wananchi.
4. Wabunge hawa hawawajibiki kwa Wananchi. Hasara na mzigo
Mapendekezo:
Mabadiliko ya Katiba kufuta Wabunge wa Michongo, wengi wao ni Wake ama wapenzi wa Viongozi na Wanasiasa na baadhi yao ni nyumba ndogo. Katiba iweke mazingira sawa kwa jinsia zote kugombea na kupata ubunge wa majimbo.
Fedha wanazolipwa zingeweza kununua vifaa tiba kwenye vituo vya afya au hata kuajiri vijana walio mitaani kwa kutumia mamilioni ya bure wanaochukua Wabunge wa viti maalum wasio na majimbo.