Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

Wala sio jokes na mimi nilishajaribu inaachia mafua yaliyobana

Hata mie nilishajaribu na ndio tegemeo langu siku zote dawa hii. Tena kwa hupoma haraka peleka matone mengi uwezavyo hata ukimeza inaruhusiwa tu ni nzuri kwa kifua kinachosumbua kubanja. Inalainisha na kufanya makohozi mazito yatoke bila tabu. Wasiliana na Mama Victoria Seme (Mkuu wa shule wa zamani Tabora Girls pia aliwahi fundisha Loleza Girls huko Mbeya) kwa maelezo zaidi ya kitaalam juu ya maajabu ya tiba hii ya mkojo.
 
habar wana jf naombeni msaada wa tiba mbadala yapata wik 3 sasa nakohoa kikohozi kikavu na kichwa kinanigonga ile mbaya, nimetumia dawa mbali pasipo nafuu yoyote! km unamtu anajua tiba mbadala naomba anisaidie! Nateseka jamanI! Pls pls help me!!
 
Sina uhakika sana kama itakusaidia lakini mimi ninaposikia hali kama hiyo nakunywa sana maji yaani kuliko kawaida na imekuwa ikinisaidia sana kwa sababu sipendi kutumia dawa.
 
Pole sana mkuu.@ Nyukibaby Kwa hicho kikohozi mimi nitakupa dawa lakini kwa masharti. Ikiwa unavuta Sigara uache kuvuta hiyo sigara kikohozi chako kitapona fanya hivi: Dawa ya kikohozi na mwenye Pumu:

(1).Kikohozi na Pumu:
Paka mafuta ya Habba sauda juu ya kifua na maungo yote na unywe kijiko kimoja cha mafuta hayo mara tatu kwa siku, na tia vijiko viwili ya mafuta hayo na utie katika maji ya moto na uvute mvuke wake kwa puani na mdomoni.

(2)
Vicks inasaidia kuondoa kikohozi kwa watu walioijaribu kutumia.

Utumiaji wake ni wakati unapotaka kulala upakae miguuni vicks kisha uvae soksi ulale,baada ya muda kidogo kikohozi kinapotea. Tumia hizi dawa za Tiba Mbadala kisha uje hapa utupe feedback.
 
Katibii kanakunyemelea kaka, vp ni mdau wa pombe na sigara? Kama vp kapime mapafu.
 
Pamoja na vipimo vingine kama TB, n.k ,Kacheck minyoo, kuna ndugu yangu nae alikua na tatizo la kukohoa kwa muda mrefu kumbe ilikua ni minyoo, alikua na kikohozi kikavu kinachopalia. Kuna thead ya ndugu BAOSITA amezungumzia dawa ya minyoo na fungus sugu, unaweza ukaijaribu endapo uta comfirm kama una minyoo. pole.
 
Katika kipindi cha wiki moja au mbili kumezuka gonjwa la watu kukohoa kikohozi kikavu na pia mafua katika jiji la Dar es salaam. Watu wengi sana wamekumbwa na gonjwa hili. Je sababu kuu ni nini?? kuna baadhi wanasema ni mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo now. Sijui wenzangu mnasemaje kuhusu hili.
 
Nina rafiki yangu wa karibu, mtoto wake anasumbuliwa na mafua mara kwa mara, tangu akiwa mchanga na sasa ana mwaka na miezi 8. Tatizo hili huwa naliona hata kwa wakubwa, mafua hayaishi, au yakiisha baada ya siku kadhaa yanaanza tena.

Tatizo hili husababishwa na nini? Je, tatizo linazuilika? Na tiba yake ni nini? Msaada tafadhali.
 
Habari za saa hii wakubwa...

Jamani mimi mafua yakinishika huwa nahisi kama nakufa, naumia sana jamani. Kichwa kinaniuma sana, nahisi kizunguzungu, uchovu kwa sana na mpaka nikipiga chafya, basi hutoka na DAMU MDOMONI!

Nilishaenda hospitalini hapo kabla, wakaniambia kwamba ni allergy na wakanipa madawa kibao. Lakini cha kushangaza mpaka leo sijapona. Yanapoa tu na kurudi!

MSAADA WENU TAFADHALI!
 
Pole sana bhoke , tatizo ni kwamba hawakukwambia una allergy na kitu gani ,vumbi , vyakula ,harufu za maua au pafyumu ,au rangi iliopakwa kwenye nyumba unayoishi , unyevu , au manyoya ya wanyama , e,g, paka . Kama walikwambia ni vizuri ukaachana na vitu hvy ,
Kuhusu dawa zipo nyingi madukani utazipata baada ya kupata ushauri wa daktari .
 
bhoke mwita, mafua yako ya aina tatu, yapo yale ya allergy ( allergic rhinitis) na yapo yanayosababishwa na virusi (viral rhinitis au common cold or infectious rhinitis) na aina ya tatu ni yale yasiyosababishwa na allergy wala virusi (non allergic au vasomotor rhinitis).

Allergic rhinitis.
Matibabu

Hii ya allergy matibabu ni kuepuka vitu ambavyo vinakuletea allergy, kuvijua lazima ufanye allergic test (unaweza kwenda upanga Haemeda Clinic kwa Dr Mwandolela jengo la scout, wana mashine za kisasa za kuchunguza allergy). Ukiweza kuepuka vile vinavyoepukika (vingine kama vumbi utakutana navyo barabarani kwenye basi nk na hivyo kuwa vigumu kuviepuka).
Dawa zipo lakini ni kwa ajili ya kupunguza "inflammation" puani na hivyo kupunguza discharges na maumivu pia lakini haziwezi kukuzuia usipate mafua tena kama utakutana na kitu usichopatana nacho (allergen). Dawa ambazo zimeonyesha uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwenye allergic rhinitis ni steroid za kupulizia puani (nasal spray steroids) kama beclometasone, budesonide, flunisolide, fluticasone, mometasone na triamcinolone, ukifika pharmacy ulizia kama wana moja ya dawa hizi kwa ajili ya kupulizia puani na zitakusaidia.
Lakini hata steroids za kumeza (systemic steroids) kama prednisolone zaweza kukusaidia. Pia kuna dawa za jamii ya antihistamines kama cetrizine zaweza kukusaidia. Steroids unaweza kutumia pamoja na antihistamines. lakini usitumie steroids kwa wingi au kwa muda mrefu zaweza kushusha kinga yako ya mwili. Muone daktari wako akushauri namna ya kutumia. Pia unaweza kutumia dawa za maumivu kwani huambatana na maumivu ya kichwa.

Viral rhinitis/common cold
aina hii ya mafua husababishwa na vimelea aina ya virusi, virusi hivyo ni pamoja na familia ya rhinoviruses, coronavirus, adenovirus na respiratory syncytial virus.
Kwa sababu ya wingi na aina mbalimbali za virusi vinavyosababisha mafua, utengenezaji kinga umekuwa mgumu.
Matibabu ya magonjwa mengi ya virusi ni magumu na mafua ya virusi ni mojawapo pia. Zipo dawa ambazo ukitumia zinakusaidia kupata nafuu mapema lakini si kupona, kupona huja kwenyewe (self-limiting). Kunywa maji ya kutosha, pumzika kiasi cha kutosha, tumia antihistamines zitapunguza wingi wa kamasi, dawa zenye vitamic C zitakupa nafuu, zinc lozenges pia zaweza kusaidia.

Kujikinga na aina hii ya mafua ni kuepuka watu wenye ugonjwa (sio kuwanyanyapaa bali kujikinga usiambukizwe kwani maambukizo yake ni kwa kugusa mkono au tissue papers au kitambaa anachotumia mgonjwa wa mafua au kukutana na virusi kama mtu akipiga chafya bila kukinga pua yake).

Vasomotor rhinitis.
Aina hii ya mafua husababisha na irritation ya pua kutokana na moshi, harufu ya vyakula na baadhi ya dawa hasa za kuspray. Hii haiitwi allergic kwa sababu jinsi inavyotokea haifuati hatua zinazoendana na magonjwa ya allergy, ni irritation tu kwenye ngozi ya pua. Huwa mafua haya hayawi makali sana kama yale ya virusi au allergy.
Matibabu yake ni kuepuka hivitu vinavyokupa irritation, kama mafua makali unaweza ukatumia dawa za kupunguza maumivu ya kichwa au kupunguza wingi wa kamasi (antihistamines), yakizidi muone daktari wako.
 
Last edited by a moderator:
Mafua yako yanasababishwa na allergy. Kama ni vumbi basi hapa tz huwezi kuliepuka labda ukaishi peponi.
Je umewahi kutumia dawa iitwayo avamys nasal spray?

Kama bado nenda kanunue au tumia kadi yako ya bima kisha uwe unajipulizia puani kila siku asubuhi kabla hujaenda kwenye shughuli zako. Naamini itakusaidia endapo utafuata maelekezo vizuri na bahati nzuri wameidesign iweze kutumika muda mrefu bila madhara
 
Back
Top Bottom