bhoke mwita, mafua yako ya aina tatu, yapo yale ya allergy ( allergic rhinitis) na yapo yanayosababishwa na virusi (viral rhinitis au common cold or infectious rhinitis) na aina ya tatu ni yale yasiyosababishwa na allergy wala virusi (non allergic au vasomotor rhinitis).
Allergic rhinitis.
Matibabu
Hii ya allergy matibabu ni kuepuka vitu ambavyo vinakuletea allergy, kuvijua lazima ufanye allergic test (unaweza kwenda upanga Haemeda Clinic kwa Dr Mwandolela jengo la scout, wana mashine za kisasa za kuchunguza allergy). Ukiweza kuepuka vile vinavyoepukika (vingine kama vumbi utakutana navyo barabarani kwenye basi nk na hivyo kuwa vigumu kuviepuka).
Dawa zipo lakini ni kwa ajili ya kupunguza "inflammation" puani na hivyo kupunguza discharges na maumivu pia lakini haziwezi kukuzuia usipate mafua tena kama utakutana na kitu usichopatana nacho (allergen). Dawa ambazo zimeonyesha uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwenye allergic rhinitis ni steroid za kupulizia puani (nasal spray steroids) kama beclometasone, budesonide, flunisolide, fluticasone, mometasone na triamcinolone, ukifika pharmacy ulizia kama wana moja ya dawa hizi kwa ajili ya kupulizia puani na zitakusaidia.
Lakini hata steroids za kumeza (systemic steroids) kama prednisolone zaweza kukusaidia. Pia kuna dawa za jamii ya antihistamines kama cetrizine zaweza kukusaidia. Steroids unaweza kutumia pamoja na antihistamines. lakini usitumie steroids kwa wingi au kwa muda mrefu zaweza kushusha kinga yako ya mwili. Muone daktari wako akushauri namna ya kutumia. Pia unaweza kutumia dawa za maumivu kwani huambatana na maumivu ya kichwa.
Viral rhinitis/common cold
aina hii ya mafua husababishwa na vimelea aina ya virusi, virusi hivyo ni pamoja na familia ya rhinoviruses, coronavirus, adenovirus na respiratory syncytial virus.
Kwa sababu ya wingi na aina mbalimbali za virusi vinavyosababisha mafua, utengenezaji kinga umekuwa mgumu.
Matibabu ya magonjwa mengi ya virusi ni magumu na mafua ya virusi ni mojawapo pia. Zipo dawa ambazo ukitumia zinakusaidia kupata nafuu mapema lakini si kupona, kupona huja kwenyewe (self-limiting). Kunywa maji ya kutosha, pumzika kiasi cha kutosha, tumia antihistamines zitapunguza wingi wa kamasi, dawa zenye vitamic C zitakupa nafuu, zinc lozenges pia zaweza kusaidia.
Kujikinga na aina hii ya mafua ni kuepuka watu wenye ugonjwa (sio kuwanyanyapaa bali kujikinga usiambukizwe kwani maambukizo yake ni kwa kugusa mkono au tissue papers au kitambaa anachotumia mgonjwa wa mafua au kukutana na virusi kama mtu akipiga chafya bila kukinga pua yake).
Vasomotor rhinitis.
Aina hii ya mafua husababisha na irritation ya pua kutokana na moshi, harufu ya vyakula na baadhi ya dawa hasa za kuspray. Hii haiitwi allergic kwa sababu jinsi inavyotokea haifuati hatua zinazoendana na magonjwa ya allergy, ni irritation tu kwenye ngozi ya pua. Huwa mafua haya hayawi makali sana kama yale ya virusi au allergy.
Matibabu yake ni kuepuka hivitu vinavyokupa irritation, kama mafua makali unaweza ukatumia dawa za kupunguza maumivu ya kichwa au kupunguza wingi wa kamasi (antihistamines), yakizidi muone daktari wako.