Ushauri tafadhali; Mpenzi amebadilika na nashindwa kumuacha

Ushauri tafadhali; Mpenzi amebadilika na nashindwa kumuacha

Sasa kama unashindwa kumuacha,basi komaa tu mpaka siku akikufanyia kituko cha wewe kumuacha mwenyewe tena kwa hiari yako mwenyewe bila kushurutishwa.

Ujue watu mnachezaga sana na akili za watu humu jf,unatangaza kabisa unahsindwa kumuacha,ushaongea nae hakuelewi wala hasikii Ndio kwanza anaota mapembe sasa unataka ushauriwe kitu gani??
 
Habar wana jamii ....nashawishika kuandika yanayonisibu hapa kwani natambua tafakari na uzoefu unaopatikana kwenu waweza kuniweka mahala salama.

Ni miaka minne sasa tangu niwe nae kwenye mahusiano. Ni kipenzi cha nafasi yangu kiukweli. Ni mwanamke aliyenifanya niamini katika kupenda, kujali, & kuthamini. Mwanzo sikuwahi kuwa na fikira kuwa kuna udhati katika mapenzi ya wanaume na wanawake. Niliamini mapenzi ni sehemu ya kusukumana siku ziende kwa Yale yaliyowahi kunipata mara kadhaa na niliyoyaona kwa marafiki na watu wengine katika mazingira niliyokaa

Kwa takribani kipindi cha miaka mitatu tangu tufahamiane ningeweza kumuelea kwa maneno machache ( anajali, anathamini, ana mapenzi ya dhati).

Kwa sasa namuona kabadilika, so msikivu tena, amekuwa mtu wa kutukana, kufanya mambo kwa kukomoa. Kati yetu hakuna tena maelewano.
Kwa uwezo wangu nimejitahid kumwambia na kumueleza Kuhusu mabadiliko katika mwenendo wake bila mafanikio na sasa ni mwezi wa sita.

Napata kigugumizi juu yake kwani nampenda sana na niliamuamini kuliko, tukaahidiana kujenga familia pamoja.
Nimejaribu mara kadhaa kujitenga nae lkn limekuwa jambo hatar sana kwangu. Yaani nimeshindwa kumuacha na yeye kila siku kituko.
Na hashauriki sasa nikimshauri anakuwa wa kunitolea matusi, nikimuelekeza kitu yeye anafanya yake tofauti.

Nilipo sasa n mtu wa kuwaza, nervous sana naiona dunia inanizonga.
Nimeshindwa la kufanya naombeni mnisaidie nahsi nitaangamia

Uwezekano ni mkubwa kuwa ametoka nje kanogewa...
 
ondoa shaka huyo bado wako mkuu itakuwa hali ngumu ya uchumi kwa sasa ndio imesababisha awe hivyo
 
Tatizo ameshajua anapendwa na kumuacha huwezi ndo mana anakufanyia hayo yote, kitu pekee kitakachokusaidia kwasasa ni wewe kufanya maamuzi magumu nasema magumu kwasababu nahisi unampenda sana na swala la kumuacha kwako ni mtihahani lakini ili uweze kupata majibu ya maswali yako ni lazma uilazimishe nafsi yako kuachana nae, yani kuanzia sasahivi, usimtafute kwa namna yoyote, usipige simu, wala text, na akipiga yeye usipokee wala akitext usijibu, kama bado anakupenda zilikuwa mbwembwe tu za kupima penzi basi lazma atakutafuta muongee face to face hapo ndo itakuwa chance yako ya kumpa warning abadilishe mwenendo wako na last chance
 
kuna mahali umeteleza na kuna mjanja katumia upenyo huo kumla demu wako.. unatakiwa utumie akili sana kumrudisha.. anakolezwa huyo..!!!!
Nimejitahid kuitafuta hiyo sehemu siioni , nmejaribu kumuuliza majibu yake ni "usiniulize mimi kama huoni shauri yako"

Mwanzo maisha yetu ilikuwa ni uwazi mmoja akikosea anaambiwa Mapema yanajadiliwa na kusonga
 
Kaeni mbali kwa muda kupeana muda wa kuwaza mambo vizuri na kupata maamuzi yaliyo bora.
Nimekuwa nikijitahidi kukaa mbali lkn Sijawahi kufanikiwa mkuu ....inashindikana nitajikuta namtafuta
 
Tumia ile method ya ''The power of letting go''
Push her away,...
Hahaha hii ni njia tamu sana kama ukijua kuitumia, lazima aje kwa magoti
Nielekeze hiyo njia mkuu ....Naona kama itafika mda nishindwe kufanya maisha maana nasumbuka sana kichwani
 
Achana nae mkuu,tatizo ni akili yako haitaki kukubali kua unaweza kumuacha,jiulize maswali kama kwani nikimuacha ntakosa nini na usijiulize kwani umekosa nini hadi akuadhibu hivyo
Napotafakari hilo swali naona Giza kwangu
 
halafu toa huo msamiati " ETI HUWEZI KUMUACHA" futa huo msamiati mara moja halafu angalia dunia kwa namna nyingine watu wangapi wanakupenda kuanzia kwenye familia yako ? halafu mpe space kwanza amekuchoka, huna jipya kwake, tatu ukiingia nae kwenye ndoa sababu anajua unampenda sana atakutesa mpaka kaburini ....

jiulize lipi bora kumwacha kabla ya kwenda kifungoni au kuendelea mkaachane kwa sheria baadae huku mnaweza kuwa tayari na kiumbe mkitese? take time think big .

huo ni ubinafsi kulazimisha penzi ..
Ahsante.... Swali linakuja nafanyaje kufanikisha, ndo napofeli
 
Sasa kama unashindwa kumuacha,basi komaa tu mpaka siku akikufanyia kituko cha wewe kumuacha mwenyewe tena kwa hiari yako mwenyewe bila kushurutishwa.

Ujue watu mnachezaga sana na akili za watu humu jf,unatangaza kabisa unahsindwa kumuacha,ushaongea nae hakuelewi wala hasikii Ndio kwanza anaota mapembe sasa unataka ushauriwe kitu gani??
Shida niliyonayo n uwezo wa kufanya maamuzi...Naona naumia nimuache lkn nafanyaje hayo maamuzi nafsi inaona namhitaji....nipo njia panda
 
Tatizo ni namna ya kukaa nae mbali siyo rahisi kama inavyoandikwa
Nafahamu inategemea na mambo mengi, lakini kama hawasomi pamoja au kufanya kazi sehemu moja anaweza tafuta hata kahobi kwa sasa kama vile akajiunga na mafunzo yoyote ya mda ambao yupo huru (mda ambao alikuwa anatumia na mwenzie) Anaweza hata tafuta kozi ya lugha ya kigeni aipendayo akawa anajifunza kwa kipindi hicho, au ala za mziki n.k
 
Piga goti omba mkuu omba sana dunia imeoza bila maombi utaambulia ubatili mtupu
 
Back
Top Bottom