Ushauri tafadhali; Mpenzi amebadilika na nashindwa kumuacha

More problems

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
433
257
Habar wana jamii ....nashawishika kuandika yanayonisibu hapa kwani natambua tafakari na uzoefu unaopatikana kwenu waweza kuniweka mahala salama.

Ni miaka minne sasa tangu niwe nae kwenye mahusiano. Ni kipenzi cha nafasi yangu kiukweli. Ni mwanamke aliyenifanya niamini katika kupenda, kujali, & kuthamini. Mwanzo sikuwahi kuwa na fikira kuwa kuna udhati katika mapenzi ya wanaume na wanawake. Niliamini mapenzi ni sehemu ya kusukumana siku ziende kwa Yale yaliyowahi kunipata mara kadhaa na niliyoyaona kwa marafiki na watu wengine katika mazingira niliyokaa

Kwa takribani kipindi cha miaka mitatu tangu tufahamiane ningeweza kumuelea kwa maneno machache ( anajali, anathamini, ana mapenzi ya dhati).

Kwa sasa namuona kabadilika, so msikivu tena, amekuwa mtu wa kutukana, kufanya mambo kwa kukomoa. Kati yetu hakuna tena maelewano.
Kwa uwezo wangu nimejitahid kumwambia na kumueleza Kuhusu mabadiliko katika mwenendo wake bila mafanikio na sasa ni mwezi wa sita.

Napata kigugumizi juu yake kwani nampenda sana na niliamuamini kuliko, tukaahidiana kujenga familia pamoja.
Nimejaribu mara kadhaa kujitenga nae lkn limekuwa jambo hatar sana kwangu. Yaani nimeshindwa kumuacha na yeye kila siku kituko.
Na hashauriki sasa nikimshauri anakuwa wa kunitolea matusi, nikimuelekeza kitu yeye anafanya yake tofauti.

Nilipo sasa n mtu wa kuwaza, nervous sana naiona dunia inanizonga.
Nimeshindwa la kufanya naombeni mnisaidie nahsi nitaangamia
 
Achana nae mkuu,tatizo ni akili yako haitaki kukubali kua unaweza kumuacha,jiulize maswali kama kwani nikimuacha ntakosa nini na usijiulize kwani umekosa nini hadi akuadhibu hivyo
 
Kaeni mbali kwa muda kupeana muda wa kuwaza mambo vizuri na kupata maamuzi yaliyo bora.
 
Kaeni mbali kwa muda kupeana muda wa kuwaza mambo vizuri na kupata maamuzi yaliyo bora.
 
halafu toa huo msamiati " ETI HUWEZI KUMUACHA" futa huo msamiati mara moja halafu angalia dunia kwa namna nyingine watu wangapi wanakupenda kuanzia kwenye familia yako ? halafu mpe space kwanza amekuchoka, huna jipya kwake, tatu ukiingia nae kwenye ndoa sababu anajua unampenda sana atakutesa mpaka kaburini ....

jiulize lipi bora kumwacha kabla ya kwenda kifungoni au kuendelea mkaachane kwa sheria baadae huku mnaweza kuwa tayari na kiumbe mkitese? take time think big .

huo ni ubinafsi kulazimisha penzi ..
 
Mkimbie kwa .uda umuachie uhuru ...

Uone atafanya nini , mema au mabaya.
 
Mkuu umeandika kwa hisia sana as if unaonewa sana kwenye hii sector ya mahaba.

Ila umebulia sana kwa almost six months no mabadiliko mkuu umejitahidi sana.

Pia ningependa nifahamu huyo mchuchu umefunga naye ndoa au unagegeda tu?

Nikipata hilo jibu nitaweza kukushauri kulingana na jinsi mahusiano yenu yalivyo.
 
Back
Top Bottom