Ushauri: Serikali ipeleke kikosi maalum Msumbiji kuokoa ndugu zetu

Kwann wewe usiuze bangi au madawa ya kulevya kama? maana na wewe unatafta rizki. Jitambue kwenye kuvunja sheria hatujalishi ulikua unatafta rizk au nn.. bali uwepo kihalali.
Mkuu,ndiyo maana tuna mahakama! Kuna mtu anaua mwenzake still yet mahakama inamuachia huru! Pia kuna mtu anafanya kosa mfano wizi,wewe ukamhukumu kwa kumchoma moto,utaingia hatiani! Hivyo,hata kama Watz walifanya kosa kule Msumbiji,siyo sawa wapigwe,kudhalilishwa kama hukumu! Kwa nini wasifikishwe kiutaratibu na kisheria kwenye vyombo husika? Ingekuwa ni wewe,ungeona halali kufanyiwa hivyo?
 
Kaka nimependa mawazo yako kwani mawazo yako ni mawazo ni ya watanzania wengi,mawazo kama haya ndio utaona tafauti ya wenzetu wenye akili na hapo utafahamu kwanini wanatuita nchi zetu ni nchi za duania ya tatu,kwani ni kweli tuko nyuma kama miaka 500 ki akili na kimawazo

Nitakupa mikasa miwili,mkasa mmoja ni wa mtanzania aliechukua uraia wa Norweg,lakini yule jamaa alivuka Norway na kuingia Denamark bila ya kibali chochote,kufika denmark yuke jamaa akaanza kuvuta unga,askari wakamkamata yule jamaa na unga,wakamuweka ndani, ubalozi wa Norway ukajuilisha cha kushangaza siku ya pili yake tu balozi akamtembelea jamaa akampelekea passport ya muda na akaondoka nae Norway

Mkasa wa pili ni mtanzania aliechukua uraia wa Marekani yeye alikamatwa Thailand na Unga,cha kushangaza serikali ya kimarekani ilifanya juu chini yule jamaa akatumikie kifungo chake Marekani, wamarekani waliondokana na jamaa wakenda nae USA

Hiyo mikasa miwili ni kuonyesha tu vipi serikali za dunia ya kwanza zinavyowalinda watu wake,hao watu wawili waliporudi katika hizo nchi hawakukaa zaidi ya miezi miwili jela

Maneno yako uliyoandika na manenoya raisi wetu aliyongea juzi kuhusu watu waliokamtwa na unga nchi za nje yanafanana,ni maneno ya watu wanaoishi dunia ya tatu,bado hatujui nini tunafanya,nini tufanye na kwanini tufanye au tusifanye,,,

Nitapenda kukwambia hivi hao watanzania walioko huko msumbiji kama wamekwenda kisheria au si kisheria,kama wamekwenda na passport au bila ya passport kama ni watanzania basi hao watu bado watabakia kama watanzania,ni jukumu la serikali ya Tanzania kuwasaidia..
Hata media kama magazeti hazilipi uzito jambo hili. Nimefuatilia magazeti ya jana Jumatatatu na leo Jumanne,hayajaripoti habari hii. Nilitaraji tupate data,wangapi wamerudi na walio bado ukizingatia mwisho ilikuwa Jumapili. Kama ulivyosema,kuna mahali hatuko sawa kama wenzetu nchi nyingine
 
kupeleka kikosi cha tanzania bila idhini ya serikali ya msumbiji "is gross violation of mozambique's territorial sovereignty" na ni "de facto declaration of war on mozambique"

viongozi wetu watumie busara sana kwa hili mihemuko ya dakika mbili isije tuingiza kwenye vita ya kijinga
 
Kwa habari niliyoisikia DW radio jana,nashauri hilo lifanyike. Kuna wenzetu wengi watakosa uwezo wa kurudi ukizingatia wamenyanganywa kila kitu! Mtanzania aliyeongea na DW,kama aliyosema wanavyonyanyaswa ni ya kweli,uchunguzi na upelekaji kikosi cha uokozi vyema vifanyike
Hii ni kazi ya Wizara ya mambo ya nje na Balozi yetu ya msumbiji kumbuka serikali imesema inafuatilia, tatizo mnadhani kila kitu ni rahisi rahisi tu.
 
Hii ni kazi ya Wizara ya mambo ya nje na Balozi yetu ya msumbiji kumbuka serikali imesema inafuatilia, tatizo mnadhani kila kitu ni rahisi rahisi tu.
Wewe ni Mtanzania? Kama ni ndiyo,elewa nchi yako!
 
kupeleka kikosi cha tanzania bila idhini ya serikali ya msumbiji "is gross violation of mozambique's territorial sovereignty" na ni "de facto declaration of war on mozambique"

viongozi wetu watumie busara sana kwa hili mihemuko ya dakika mbili isije tuingiza kwenye vita ya kijinga
Suppose you violate,and stabilize while altogether your relatives are saved!
 
Kama umeenda nchi ya wenzako bila kibali hamna namna acha wawajibishwe. Serikali isipoteza muda wake kwa watu waliovunja sheria. Kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya
Mambo mengine humu ndani unasoma unakosa lakusema unabaki kuguna tu jamani sis watanzania sijui tulirogwa na nani?
 
Wewe unafahamu diplomasia? kama siyo, heshimu kazi za wenzako.
Wewe unajua diplomasia,na ni kazi zako,tunakuheshimu. Lakini,sisi ndiyo tumekupa kazi hizo unapaswa utuheshimu pia !kama hujui hivyo,hata maana ya diplomasia utakuwa huielewi.
 
Kama umeenda nchi ya wenzako bila kibali hamna namna acha wawajibishwe. Serikali isipoteza muda wake kwa watu waliovunja sheria. Kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya

WEWE JAMAA HAUNA AKILI KABISA AISEE HUJUI HATA SITUATION ILIVYO UNA COMMENT UJINGA BAHATI YAKO NIMECHELEWA HUU UZI....... DONT TALK IF U DONT HAVE AMPLE INFO......
 
WEWE JAMAA HAUNA AKILI KABISA AISEE HUJUI HATA SITUATION ILIVYO UNA COMMENT UJINGA BAHATI YAKO NIMECHELEWA HUU UZI....... DONT TALK IF U DONT HAVE AMPLE INFO......
Tupe info unazojua wewe mwenye akili.. Bado hujachelewa uzi upo tiririka dada
 
Back
Top Bottom