Ushauri: Serikali ipeleke kikosi maalum Msumbiji kuokoa ndugu zetu

Kwa habari niliyoisikia DW radio jana,nashauri hilo lifanyike. Kuna wenzetu wengi watakosa uwezo wa kurudi ukizingatia wamenyanganywa kila kitu! Mtanzania aliyeongea na DW,kama aliyosema wanavyonyanyaswa ni ya kweli,uchunguzi na upelekaji kikosi cha uokozi vyema vifanyike
Kama umeenda nchi ya wenzako bila kibali hamna namna acha wawajibishwe. Serikali isipoteza muda wake kwa watu waliovunja sheria. Kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya
 
Si ajabu ikatoka kauli "Walikwenda wenyewe watarudi wenyewe. Kwani si ccm wala Siri kali iliwapeleka huko ".
 
Kama umeenda nchi ya wenzako bila kibali hamna namna acha wawajibishwe. Serikali isipoteza muda wake kwa watu waliovunja sheria. Kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya
Kumbuka,nao Wamsumbiji wanakuja Tz kwa mtindo huohuo. Pia Wazambia,na Wamalawi ni wengi tu,wengine wameoa dada zetu. Tusiwaache hivi hivi japo wamekosea!
 
Kuna taratibu za kufuata kupeleka kikosi maalum! Kwani wao wanafukuzwa na kikosi gani,Sijasikia tamko la serikali ya msumbiji kwamba wanaunga mkono huo unyama wanaofanyiwa ndugu zetu au la.
 
Wanajeshi wetu wamekaa muda mrefu sana bila kufanya kazi...

Naunga mkono sasa kimefika kipindi wakafanye kazi yao...

Kama ile waliyomfanyia Idd Amin
 
Kuna taratibu za kufuata kupeleka kikosi maalum! Kwani wao wanafukuzwa na kikosi gani,Sijasikia tamko la serikali ya msumbiji kwamba wanaunga mkono huo unyama wanaofanyiwa ndugu zetu au la.
Mkuu,pitia media mbalimbali utapata ukweli!
 
Kupeleka kikosi ni kujaribu kuivamia Serikali ya Maputo sisi wana diplomasia wabobezi tunasema serikali isifanye kitendo hicho.
Wewe ulielewa ni kikosi cha jeshi? Pia kama wamenyanganywa kila kitu,wamedhalilishwa na kupigwa (Ref. DW redio) unafikiri nini kifanyike? Jua wameamriwa kuondoka haraka ina maana ni kwa gharama zao. Kuna uwezekano mkubwa baadhi wakakwamia huko.
 
Sasa kikosi gani mkuu? Unafikiri ni kikosi cha Mbuzi? Kupeleka Kikosi means military operation.
 
Back
Top Bottom