Ushauri: Serikali idhibiti vipindi vya michezo kwenye redio na TV nchini

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,459
17,258
Naomba kumshauri waziri wa michezo na burudani aanze na kudhibiti vipindi vya michezo kwenye redio na TV.

Redio stations nyingi kama sio zote hapa nchini wanaanza vipindi vya michezo kuanzia sa 12 asubuhi hadi sa 7 mchana. Huu ni muda wa watu kufanya kazi nyingine za uzalishaji.

Hata Ulaya ukiachia zile stations ambazo ni sports perse kitu ambacho hakipo Tanzania, michezo inatangazwa baada ya masaa ya kazi, hasa jioni kwa ajili ya kuburudika.

Ndio maana kokote Duniani ukiacha siku maalum za michezo kama olimpiki ama World Cup michezo haianzi kuchezwa sa 12 asubuhi, ni jioni baada ya watu kufanya shughuli nyingine za uzalishaji.

Marekani, sports and entertainment inachangia 20% ya uchumi, the same na kwa nchi nyingi za ulaya. Maana yake hiyo 80% ambayo ndio msingi mkuu wa uchumi inatakiwa ndio ipewe attention zaidi.

Haiwezekani Muda wa watu kufanya kazi nyingine za uzalishaji wawe wanasikiliza kinachoitwa uchambuzi wa michezo masaa 8 ya siku tena masaa ambayo ni active ya mchana, haiwezekani.

Toka sa 12 asubuhi mtu anasikiliza uchambuzi tu wa mpira atafanya kazi saa ngapi? Mwisho wa siku hao hao tunaenda kuomba misaada kwa hao tunaoshinda kuchambua michezo yao huku wao wakiwa wanapiga kazi.

Serikali isimamie, vipindi vya michezo vianze saa 10 jioni hadi usiku mnene lakini sio kuanza saa 12 asubuhi hadi sa 8 mchana.

Ahsante.
 
Hauwezi kudeal na kila jambo katika ulimwengu huu, fanya yale yenye tija kwa upande wako mengine achana nayo au waachie wengine.
 
Sema washabiki wa mpira wa hapa kwetu wana mizuka ya kijinga na ushamba uliopituliza. Fuatilia hata aina ya ushabiki huko katika nchi ulizotaja, iko tofauti bro. Tuanze na kubadilika sisi kwanza TVs na Redio wataadjust muda wa kutusikilizisha.

Wewe kama kila saa kichwani mwako umejaza michezomichezo tuu, wakati wenzako wanaingiza fedha kwenye hiyo hiyo michezo unaeumia ni wewe.

Hata hivyo ukiona wewe unao muda mwingi sana wa kusikiliza na kufuatilia sports, ujue uko jobless. Hata wakibadilisha muda wa kipindi haitakusaidia kitu.
 
Shida ya kutaka kujipa umuhimu kwenye Maisha ya watu kwani umelazimshwa kusikiliza hizo redio?
 
Tatizo lako umejiangalia wewe tu unafkiri kila Mtu anafanya kazi mchana, umesahau kuwa kuna watu wengi sana wanafanya Kazi kwa shift wanaingia night mchana ndio muda wao wa kuburudika na hivyo vipindi.
 
Mkuu mtu anayejitambua hawezi kusikiliza vipindi vya michezo wakati anafanya kazi.

Kama huyo mtu yupo basi hajitambui au hana kazi ya kufanya au kazi anayofanya haiitaji kutumia focus kubwa maybe anauza duka.

Hivyo hapo hakuna tatizo lolote sababu sio lazima kusikiliza radio na sio kila mtu anafanya kazi unayofanya wewe.
 
Naomba kumshauri waziri wa michezo na burudani aanze na kudhibiti vipindi vya michezo kwenye redio na TV.

Redio stations nyingi kama sio zote hapa nchini wanaanza vipindi vya michezo kuanzia sa 12 asubuhi hadi sa 7 mchana. Huu ni muda wa watu kufanya kazi nyingine za uzalishaji.

Hata Ulaya ukiachia zile stations ambazo ni sports perse kitu ambacho hakipo Tanzania, michezo inatangazwa baada ya masaa ya kazi, hasa jioni kwa ajili ya kuburudika.

Ndio maana kokote Duniani ukiacha siku maalum za michezo kama olimpiki ama World Cup michezo haianzi kuchezwa sa 12 asubuhi, ni jioni baada ya watu kufanya shughuli nyingine za uzalishaji.

Marekani, sports and entertainment inachangia 20% ya uchumi, the same na kwa nchi nyingi za ulaya. Maana yake hiyo 80% ambayo ndio msingi mkuu wa uchumi inatakiwa ndio ipewe attention zaidi.

Haiwezekani Muda wa watu kufanya kazi nyingine za uzalishaji wawe wanasikiliza kinachoitwa uchambuzi wa michezo masaa 8 ya siku tena masaa ambayo ni active ya mchana, haiwezekani.

Toka sa 12 asubuhi mtu anasikiliza uchambuzi tu wampira atafanya kazi sa ngapi? Mwisho wa siku hao hao tunaenda kuomba misaada kwa hao tunaoshinda kuchambua michezo yao hulu wao wakiwa wanapiga kazi.

Serikali isimamie, vipindi vya michezo vianze sa 10 jioni hadi usiku mnene lakini sio kuanza saa 12 asubuhi hadi sa 8 mchana.

Ahsante.
Sorry mkuu, umewahi kuishi nje au kwenda?
Muda wa kazi ni upi kwani hasa huko nje, alot of jobs ni by shift day n night, sasa ina maana vipindi hivyo vipigwe marufuku?
 
Back
Top Bottom