Tanzania kuna wachambuzi wa michezo ila...

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,885
2,766
Ila zaidi ya redio hakuna majukwaa mengine ambapo unaweza kutembelea na kupata taarifa za kimichezo (hasa soka) kwa wakati na za kutosheleza.

Nakumbuka enzi hizo alianza Dr Leakey tukimsikiliza kipindi cha kombe la dunia - 1994 to 1998. Kipindi hicho ni yeye alitamba kwenye uchambuzoi wa soka tena la kimataifa kwa majina ya wachezaji, mchezo wenyewe, historia zao pamoja na masihara kibao. Alivuma sana. Miaka ya 2002 ndio wakaibuka kina Haji Manara na wengine na baada ya hapo yakatokea mafuriko ya wachambuzi wa soka la kitaifa na kimataifa. Leo hadi asubuhi unasikia kuna vipindi vya uchambuzi wa michezo redioni.

Ilitakiwa sambamba na hilo la mafuriko ya wachambuzi pangekuwepo na majukwaa mengine hasa ukichukulia kuna social media kwa sasa. Huwezi kupata taarifa za kimichezo kwa wakati na usahihi katika jukwaa moja na ukaridhika. Si Yanga, si Simba, wala si NBC Premier League wenye taarifa za kuridhisha za kimichezo. Hapo tumekwama sana.

Kupata tu taarifa za mchezo wa Yanga kesho Jumapili hadi uanze kuvizia redio. Hii ni challenge kwa wapenda michezo na wadau wa burudani kufanyia kazi. Wenzetu nje wako very active. Tazama EPL, Bundesliga, Serie a, La Liga, etc

Sijui hawa vijana wanakwama wapo wakati ukiwasikiliza ni kama wana taarifa zote vichwani mwao. SImu wanazo, intaneti wanayo (tena 4G, 5G), laptop wanazo. Wanafahamiana na developers kwa ajili ya kuwatengenezea aidha app nzuri au tovuti ambazo kazi yao ni ku update tu taarifa kama zinavyowafikia. Hili nalo hawaliwezi. Wanachotaka ni kuchukua taarifa kwa kudonoa toka mitandaoni na kukaa redioni kudadavua. Tunahitaji Sports Hub
 
Tembelea vijiwe vya kahawa, car wash (siyo zile zabki sure zenye mshine za kisasa au zenyepump, bali wanazotumia kitambaa na ndoo), tembelea feri (kama upo dar), tembelea masoko ya vyakula, nenda machinjioni vingunguti, garage za uswazi n.k
 
Usemacho ni kweli. Ila na wao huokoteza taarifa toka redio moja hadi nyingine. Sasa wakikutana ndio unapata hiyo "pakeji"
 
Mbona kuna blogs za michezo nyingi tu kama salehe jembe, bin zubeir sports online zipo miaka mingi tu. Poa online tvs kama mpenja nk? Sema wanaandika zaidi simba na yanga
 
Kwenye meza za wauza magazeti nako kuna wachambuzi wa soka utapenda. Hawa vijana wanaochambua soka redioni na tv lugha za kiingereza, kifaransa, kireno, kihispania, kitaliano, kijerumani na kirusi zinawakwamisha. Wanashindwa kutaja majina ya wachezaji ya lugha hizo
 
Radio sahv kuanzia asubuhi mpaka jioni ni uchambuzi wa michezo,wanazungumzia mambo ya wasanii na mambo ya udaku+kubet
Haya ndiyo mambo wanayoyapenda
Wabongo

Ova
 
Naona ni kama mkakati kuwaondoa vijana kwenye reli. Kijiwe chochote stori ni mpira tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom