Ushauri: Rais Samia vunja TAKUKURU na iundwe upya

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,703
6,498
Mama kama unataka kudili na rushwa nchi hii anza na TAKUKURU hii haina kazi zaidi ya kutumia pesa za walipa kodi. Hizo pesa za kuwalipa hawa bora vijana wapewe mitaji tu.

Ni taasisi ambayo haina kazi na ina bajeti kubwa sana, Taasisi yenyewe imejaa wapigaji.

Ukiangalia Habari kila sehemu ni Rushwa ni Rushwa ni upigaji, lakini cha ajabu kuna offisi za TAKUKURU kila wilayaj je huwa wana kazi zipi sasa?

Hawa wana kazi zipi hasa? na whay wanaendelea kulipwa pesa kwa kazi wasizo zifanya?

Mheshimiwa Rais anapaswa kuvunja hii taasisi either ifutwe kabisa au isukwe upya make uwepo wake ni sawa na kuto kuwepo.

Katika Taasisi zinazo kula pesa bila kufanya kazi ni hii TAKUKURU.

Wakati wa Mwenda zake ilitumika sana kunyanyasa watu na kubambikia kesi, sasa baada ya Mwenda zake sasa hawana kazi tena za kufanya.
 
BEBDCA3D-99F0-422B-8C40-5F995CF52FCB.jpeg
 
Wao ndio wanaongoza kula rushwa. Wanasubiri viongozi wafanye ziara na kuwaagiza wachukue hatua
 
Bi Indira Ghanthi, aliyewahi kuwa waziri mkuu wa India yeye aliunda anti corruption 6, ya pili kuichunguza ya kwanza na ya tatu kuichunguza ya pili hadi ya sita lakini akazivunja zote baada ya kugundua zote ni corrupt.
 
Back
Top Bottom