Ushauri: Nini nifanye ili mwanangu aweze kuendelea na masomo mwaka huu?

Crusaders

Senior Member
Jun 30, 2022
167
205
Habarini wana jukwaa.

Naomba ushauri wenu tafadhali, nina mwanangu amehitimu mwaka huu kidato cha sita (Feza).

Amepata ufaulu wa daraja la kwanza point 7. ( Div I . 7) Science. Kidato cha nne alipata daraja la kwanza point 7 pia.

Anatamani sana kusoma course zifuatazo zinazohusiana na masuala ya anga (aviation).
  • Aerospace Engineering .
  • Aeronautical engineering.
  • Private Pilot.

Nilipata chuo nje ya nchi (Europe) nikalipia hadi tuition fee lakini bahati mbaya amekosa Visa.

Binafsi nimesikitika sana, amehuzunika sana pia, sihitaji huu mwaka upote bure.

Niko hapa mbele yenu kuomba ushauri, ni jinsi gani naweza kufanya kupata admission kwa muda uliobaki ndani ya mwaka huku, ili aendelee na masomo hasa kwa nchi za Europe (Poland, Cyprus na Scandinavian countries) na North America (Usa & Canada).

Nitashukuru sana kwa mchango wenu.
 
Habarini wana jukwaa.

Naomba ushauri wenu tafadhali, nina mwanangu amehitimu mwaka huu kidato cha sita (International School).

Amepata ufaulu wa daraja la pili point 7. ( Div II . 7) Science. Kidato cha nne alipata daraja la kwanza point 7 pia.

Anatamani sana kusoma course zifuatazo zinazohusiana na masuala ya anga (aviation).

  • Aerospace Engineering .
  • Aeronautical engineering.
  • Private Pilot.

Nilipata chuo nje ya nchi (Europe) nikalipia hadi tuition fee lakini bahati mbaya amekosa Visa.

Binafsi nimesikitika sana, amehuzunika sana pia, sihitaji huu mwaka upote bure.

Niko hapa mbele yenu kuomba ushauri, ni jinsi gani naweza kufanya kupata admission kwa muda uliobaki ndani ya mwaka huku, ili aendelee na masomo hasa kwa nchi za Europe (Poland, Cyprus na Scandinavian countries) na North America ( Usa & Canada).

Nitashukuru sana kwa mchango wenu.
Alikuambia point 7 Ni division two?
Halafu akakuambia amekosa Visa baada ya kulipa fees?
Akikuambia kingine tujuze..
 
Alikuambia point 7 Ni division two?
Halafu akakuambia amekosa Visa baada ya kulipa fees?
Akikuambia kingine tujuze..
Mtu mwenye busara ha deal na makosa madogo katika uandishi, bali wazo la jumla (general content), hujawahi kukosea wewe katika uwasilishaji mawazo?

Ni mara yako ya kwanza kusikia mtu kalipa ada ila akakosa Visa, ni ajabu? umewahi kusafiri nje ya nchi au kusoma nje?
 
Habarini wana jukwaa.

Naomba ushauri wenu tafadhali, nina mwanangu amehitimu mwaka huu kidato cha sita (Feza).

Amepata ufaulu wa daraja la kwanza point 7. ( Div II . 7) Science. Kidato cha nne alipata daraja la kwanza point 7 pia.

Anatamani sana kusoma course zifuatazo zinazohusiana na masuala ya anga (aviation).

  • Aerospace Engineering .
  • Aeronautical engineering.
  • Private Pilot.

Nilipata chuo nje ya nchi (Europe) nikalipia hadi tuition fee lakini bahati mbaya amekosa Visa.

Binafsi nimesikitika sana, amehuzunika sana pia, sihitaji huu mwaka upote bure.

Niko hapa mbele yenu kuomba ushauri, ni jinsi gani naweza kufanya kupata admission kwa muda uliobaki ndani ya mwaka huku, ili aendelee na masomo hasa kwa nchi za Europe (Poland, Cyprus na Scandinavian countries) na North America ( Usa & Canada).

Nitashukuru sana kwa mchango wenu.

Mtafutie South Africa, wengi wanasoma aviation huko.
 
Yaani umelipa milion 100 au chini kidogo then umekosa visa, sio kweli, kila ubalozi unamaelekezo sahihi kwa wanaotaka kwenda kusoma, pesa yote hiyo haiwezi kupotea hivihivi labda kama hela uliiokota na wakaona hakuna uwezekano wa kupata nyingine kwahiyo lazima mwanafunzi atazamia tu.
 
Mtu mwenye busara ha deal na makosa madogo katika uandishi, bali wazo la jumla (general content), hujawahi kukosea wewe katika uwasilishaji mawazo?

Ni mara yako ya kwanza kusikia mtu kalipa ada ila akakosa Visa, ni ajabu? umewahi kusafiri nje ya nchi au kusoma nje?
Usije juu. Umelileta hapa public na hivyo ruhusu watu waulize na watoe maoni yao kwa uhuru kabisa.

Ina maana ulilipa fees kabla hajapata admission kwenye hicho chuo? Na kama alikuwa amepata admission ina maana chuo kilikuwa kimetuma forms zote zinazohitajika kwenda kuombea visa katika ubalozi wao. Sote tuliosoma Ulaya na Marekani huo ndiyo utaratibu.

Ukishapata admission wanakutumia forms zao ambazo kupata visa ni kama 99.99999%. Sasa yeye ilikuwaje akakosa visa wakati ameshapata admission na kupata nyaraka zote muhimu mpaka na fees mkalipa?

Kuna kitu hakiko sawa katika maelezo yako. Nitarudi baadaye ukishanyoosha maelezo.
 
Jomba elimu yetu sasa hivi iko vizuri; mwambie aombe vyuo vikuu vya hapa nchini, TCU wamefungua dirisha la mwisho la udahili.
 
Usije juu. Umelileta hapa public na hivyo ruhusu watu waulize na watoe maoni yao kwa uhuru kabisa.

Ina maana ulilipa fees kabla hajapata admission kwenye hicho chuo? Na kama alikuwa amepata admission ina maana chuo kilikuwa kimetuma forms zote zinazohitajika kwenda kuombea visa katika ubalozi wao. Sote tuliosoma Ulaya na Marekani huo ndiyo utaratibu. Ukishapata admission wanakutumia forms zao ambazo kupata visa ni kama 99.99999%. Sasa yeye ilikuwaje mkakosa visa wakati ameshapata admission na kupata nyaraka zote muhimu mpaka na fees mkalipa?

Kuna kitu hakiko sawa katika maelezo yako. Mimi ni mwalimu huko huko mtoto wako anakokwenda kusoma. Nitarudi baadaye ukishanyoosha maelezo.
Nimebaki kushangaa tu maelezo yake.
Haki nimeshangaa mno.
Mimi sijasoma huko lakini najua utaratibu ndo huo unaosema.
 
Nimebaki kushangaa tu maelezo yake.
Haki nimeshangaa mno.
Mimi sijasoma huko lakini najua utaratibu ndo huo unaosema.
Mzazi mwenzetu inaonekana makosa aliyoyafanya yeye ya kukosa elimu yasije yakajirudia kwa Mtoto wake! Bora mi ningeona atafute ndg au wakala mwenyewe kujua Mambo ya elimu amsaidie, maana Mzazi hajui hata muundo wa division uko je!? Huyu sizani hata kama alifika O level!!
 
Mkuu wayagute tassaaa nadhani wako Victoria jengo la tanzanite watakusaidia tatizo lako la visa na kukuunganisha na vyuo
 
Yaani umelipa milion 100 au chini kidogo then umekosa visa, sio kweli, kila ubalozi unamaelekezo sahihi kwa wanaotaka kwenda kusoma, pesa yote hiyo haiwezi kupotea hivihivi labda kama hela uliiokota na wakaona hakuna uwezekano wa kupata nyingine kwahiyo lazima mwanafunzi atazamia tu.
Ndivyo nilivyoandika hivyo kuwa nimelipa milioni 100 mbona unaandika yasiyoandikwa Mkuu?
 
Back
Top Bottom