Kama ningekuwa Muhitimu wa Kidato cha Sita Mwaka huu 2022. Ningefanya nini cha Tofauti??

MlekwaKik

Member
May 18, 2022
8
6
Kama ningeweza kurudisha muda nyuma ili nirudi kuwa muhitimu wa kidato cha sita mwaka 2022, basi ningefanya yafuatayo ili niandae vizuri kesho yangu:
  • Sitaomba Chuo Kikuu kwasababu tu nimemaliza kidato sita na nimefaulu kupata vigezo vya kuingia Chuo Kikuu.
  • Sitaingia Chuo Kikuu kwasababu tu muda na umri wangu wa kuingia Chuo Kikuu umefika.
  • Sitaingia Chuo Kikuu kwasababu Wazazi wanataka niingie Chuo Kikuu. (Japo kwa umri huu unakuwa hauna maamuzi na maisha yako hili ni gumu sana. Na linahitaji kuwa na Mzazi mwenye uelewa sana wa maisha)
  • Sitaingia Chuo Kikuu kwasababu tu nimepata udahili (admission) kwa kozi ninayoipenda.
  • Sitaingia Chuo Kikuu kwasababu tu rafiki zangu wote wameenda Vyuo Vikuu basi na mie itabidi niende.
Ila ningefanya vitu vifuatavyo kama ningepata fursa ya kurudisha muda nyuma:
  • Ningeenda Chuo Kikuu kusoma baada ya kulijua kusudi langu hasa hapa Duniani ni nini?? Nimeletwa na MUNGU hapa Duniani ili niwe nani au ili nifanye nini?? Na je hicho kitu kinahitaji elimu kiasi gani ili niweze kukifanya.
  • Ningeomba wazazi nikae nyumbani japo mwaka mmoja niingie mtaani kujaribu kufanya chochote kile hata kwa kujitolea tu kwanza, ili nijue kama ninachokipenda kweli naweza kukiishi baada ya miaka 4 ya Chuo.
  • Ningeenda Chuo Kikuu baada ya kuwa nimejifunza kitu mtaani na kuona changamoto fulani katika jamii na nimepata wazo la namna la kuitatua hiyo changamoto, ila ninahitaji kusomea kozi fulani ili kuweza kwenda kuitatua hiyo changamoto huko mtaani.
  • Kama hiyo Changamoto haihitaji utaalamu wowote mkubwa wa kusomea basi ningeanza na elimu ya kidato cha sita kufanya kile ambacho naweza kukifanya alafu nikaona kama wazo langu linawezekana au ni wazo la kitoto. Kama linawezekana na linaweza kufanyika basi ningeendelea na hilo wazo na kuanzisha biashara, baada biashara yangu kukaa muda fulani, sasa ningeangalia nahitaji utalaamu gani ili biashara iweze kukua zaidi. Hapo ningejiunga na Chuo Kikuu japo kusomea hata BBA tu.
  • Ningeingia Chuo Kikuu kama ingekuwa inawezekana kwenda kusomea kile ninachokihitaji kwenya biashara yangu. Hapa namaanisha kwa mfano sitaki Shahada ya Computer Science au IT ila nataka tu kujua kuwa Programmer na nisome kozi zile zinazo husiana na hicho ninachotaka tu. Au kama nataka kujua jambo fulani basi nisome yale masomo ambayo mie nataka kulingana na uhitaji wa biashara yangu, na wala sitahitaji kuwa na cheti cha kuhitimu masomo.
  • Kama ningekuwa napenda kitu chochote kinachohusiana na ufundi uashi au ufundi umeme au magari au ushonaji au ufundi simu au urembo au kilimo, hapo hata kama ningekuwa na DIV I ya Points 3 ningeingia VETA pale Chang'ombe. Ili kusomea hicho kitu na baada ya hapo ada ya Chuo Kikuu ningetumia kufungua ofisi yangu.
Najaribu kuwaza kwa sauti kama muda ungekuwa unarudi nyuma, ila pia najaribu kuwaonesha Vijana wa kidato cha Sita angalau wapate picha kamili ya maisha yalivyo.

Elimu ya Chuo Kikuu sio elimu ya lazima kila mtu kuwa nayo, ila ni elimu inayotafutwa pale kunapokuwa na uhitaji wa Elimu hiyo katika jambo fulani. Tubadirishe akili na mitazamo na mawazo (mindset) za watu wetu, waanze kuelewa hii kitu ili tuepukane na Vijana kwenda kupoteza pesa na muda bure huko Vyuoni. Na hili halihitaji hata ushahidi tayari tuna idadi kubwa ya watu wapo mtaani hawana ajira na wana elimu ya Vyuo Kikuu na hawajui hata waanzie wapi maisha.

Wanalaumiwa wao eti hawataki kujiajiri na wana chagua kazi, ila hauwezi kumuandaa mtu kwa miaka 17 kucheza basketball, alafu umlazimishe kwenda kucheza fainali za mpira wa miguu Kombe la Dunia na utegemee akacheze na Brazil alafu aifunge aje na kombe nyumbani. Haya ndo Vijana wanaambiwa wayafanye baada ya kurudi mtaani wakimaliza Vyuo Vikuu, sio haki wanaonewa hawa watoto. Hivi mtu kasoma miaka 7 elimu msigi, 4 sekondari, 3 A level alafu 3 au 5 Chuo Kikuu amerudi Mtaani ni Daktari, alafu unamwambia sasa nenda kafuge kuku ujikimu kimaisha. Sio sawa hii kitu. Na hauwezi kusema eti mtu yupo Muhimbili awe anasoma huku anajifunza kufuga kuku, na amalize akiwa biashara ya kuku na shahada ya Udaktari.

Vitu vingine havihitaji Serikali wala Rais wala Chama Cha Siasa wala Uamuzi wa Bunge au Mawaziri. Ni mtazamo wa wazazi na walezi na wanafunzi wenyewe, elimu hizi za mbadala (VETA na zingine) zipo nyingi sana hapa nchini na zina fursa nyingi sana. Ila ni elimu ambazo hakuna mtu anazipa kipaumbele zinaonekana ni elimu za wajinga, ila huko ndo pesa ilipo na watengeneza ajira wapo huko wengi sana. Kwani itakugharimu nini kuwa fundi muwashi kwa miaka mitatu alafu badae ukaenda kusoma Civil Engineering??? Lakini je unaweza ukawa Civil Engineer alafu ukaanza kazi kama kibarua wa fundi muwashi wa darasa la 7?? Hiyo haiwezekani ndo maana ni rahisi kwa Engineer kukaa mtaani bila kazi, huku darasa la 7 akipeleka watoto wake english medium.

Ni muda tuache kulia na Serikali na Mitaala ya Elimu kila siku, badala yake tuanze na kile tunaweza kufanya. Wakati Serikali wanaangalia mitaala, we jiongeze namna ya kumsaidia mwanao au kujisaidia mwenyewe, ili ukitoka Chuo usianze kuzagaa mtaani kutafuta namna ya kuwalipa HESLB mkopo wao.
 
Ni kweli

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo kwa mtazamo wako unatamani kama wanafunzi wote waliomaliza form 6 mwaka huu wakiuona huu uzi wako wasiende vyuoni bali waingie mtaani kujihangaisha kujifunza maisha.
Unasema hivyo kwa kuwa una hoja ya msingi au una wivu nyuma ya pazia wa kuchukia jinsi makundi ya vijana yanavyoelekea vyuoni hata wale ambao miaka michache nyuma wasingeweza kupata hiyo nafasi?
Kukosa kazi ukiwa na asie msomi kuna tofauti kwani pia namna Yao ya kufikiri ni tofauti.
Waache vijana wakachukue digrii zao mambo ya kupambania maisha yatakuja baadae wakati wao ukifika kwani maisha hayana formula,eti kwa vile yule alikuwa vile basi lazima huyu nae atakuwa kama yule,haiko hivyo.
 
We Jamaaa una akili sana.
Jitahidi kufanya Ibada Pepo Ina kuhusu
Amen. Asante sana sana hakuna Dua kubwa ya kumuombea binadamu zaidi ya hii ya kumuombea mtu Pepo. Kwa kuiwaza Pepo kuwa zawadi ya juu kabisa kwa Binadamu basi hata wewe pia Pepo inakuhusu maana ipo katika mazingatio yako ya maisha.
 
Kwa hiyo kwa mtazamo wako unatamani kama wanafunzi wote waliomaliza form 6 mwaka huu wakiuona huu uzi wako wasiende vyuoni bali waingie mtaani kujihangaisha kujifunza maisha.
Unasema hivyo kwa kuwa una hoja ya msingi au una wivu nyuma ya pazia wa kuchukia jinsi makundi ya vijana yanavyoelekea vyuoni hata wale ambao miaka michache nyuma wasingeweza kupata hiyo nafasi?
Kukosa kazi ukiwa na asie msomi kuna tofauti kwani pia namna Yao ya kufikiri ni tofauti.
Waache vijana wakachukue digrii zao mambo ya kupambania maisha yatakuja baadae wakati wao ukifika kwani maisha hayana formula,eti kwa vile yule alikuwa vile basi lazima huyu nae atakuwa kama yule,haiko hivyo.
Siwezi kuupinga mtazamo wako, upo sahihi pia na ninaheshimu sana mawazo yako Mkuu. Asante sana kwa mchango wako na kuisoma post yangu, umenipa heshima kubwa sana kwa kusoma na kutoa maoni yako. Mungu wa Mbinguni akubariki sana.
 
Maisha yapo tofauti Sana mtoto was maskini anabidi aende chuo apate exposure na boom ili apate startup kuliko kubaki mtaani bila future
 
:D:D:D:D:D:D:D upo sahihi mkuu kuna watu boom ndo mtaji wala hawana habari na masomo
 
Kwa hiyo kwa mtazamo wako unatamani kama wanafunzi wote waliomaliza form 6 mwaka huu wakiuona huu uzi wako wasiende vyuoni bali waingie mtaani kujihangaisha kujifunza maisha.
Unasema hivyo kwa kuwa una hoja ya msingi au una wivu nyuma ya pazia wa kuchukia jinsi makundi ya vijana yanavyoelekea vyuoni hata wale ambao miaka michache nyuma wasingeweza kupata hiyo nafasi?
Kukosa kazi ukiwa na asie msomi kuna tofauti kwani pia namna Yao ya kufikiri ni tofauti.
Waache vijana wakachukue digrii zao mambo ya kupambania maisha yatakuja baadae wakati wao ukifika kwani maisha hayana formula,eti kwa vile yule alikuwa vile basi lazima huyu nae atakuwa kama yule,haiko hivyo.
Umri sio Akili.
Umeandika madudu
 
Back
Top Bottom