Ushauri: Nini nifanye ili mwanangu aweze kuendelea na masomo mwaka huu?

Habarini wana jukwaa.

Naomba ushauri wenu tafadhali, nina mwanangu amehitimu mwaka huu kidato cha sita (Feza).

Amepata ufaulu wa daraja la kwanza point 7. ( Div I . 7) Science. Kidato cha nne alipata daraja la kwanza point 7 pia.

Anatamani sana kusoma course zifuatazo zinazohusiana na masuala ya anga (aviation).
  • Aerospace Engineering .
  • Aeronautical engineering.
  • Private Pilot.

Nilipata chuo nje ya nchi (Europe) nikalipia hadi tuition fee lakini bahati mbaya amekosa Visa.

Binafsi nimesikitika sana, amehuzunika sana pia, sihitaji huu mwaka upote bure.

Niko hapa mbele yenu kuomba ushauri, ni jinsi gani naweza kufanya kupata admission kwa muda uliobaki ndani ya mwaka huku, ili aendelee na masomo hasa kwa nchi za Europe (Poland, Cyprus na Scandinavian countries) na North America (Usa & Canada).

Nitashukuru sana kwa mchango wenu.
Nini sababu ya kukosa visa kama alipata shule?
 
Wasiliana na jamaa mmoja kwenye tiktok anajiita ebm scholars anaonekana ni mtaalamu wa marekani anaweza kukusaidia
 
Habarini wana jukwaa.

Naomba ushauri wenu tafadhali, nina mwanangu amehitimu mwaka huu kidato cha sita (Feza).

Amepata ufaulu wa daraja la kwanza point 7. ( Div I . 7) Science. Kidato cha nne alipata daraja la kwanza point 7 pia.

Anatamani sana kusoma course zifuatazo zinazohusiana na masuala ya anga (aviation).
  • Aerospace Engineering .
  • Aeronautical engineering.
  • Private Pilot.

Nilipata chuo nje ya nchi (Europe) nikalipia hadi tuition fee lakini bahati mbaya amekosa Visa.

Binafsi nimesikitika sana, amehuzunika sana pia, sihitaji huu mwaka upote bure.

Niko hapa mbele yenu kuomba ushauri, ni jinsi gani naweza kufanya kupata admission kwa muda uliobaki ndani ya mwaka huku, ili aendelee na masomo hasa kwa nchi za Europe (Poland, Cyprus na Scandinavian countries) na North America (Usa & Canada).

Nitashukuru sana kwa mchango wenu.
Usihuzunime wala kufikiria kipoteza pesa zako nje ya nchi. Pale Usagara, Missungwi, Mwanza njia ya kwenda Kivuko cha Kigongo (Daraja la Magufuli) kuna Chuo cha Urubani. Sema nikufanyie michongo maana Mkuu wa Chuo namjua.
 
Lakini Bado naamini katikati ya haya magugu utapata pia kitu Cha kusaidia. Kuna watu waungwana wataelewa na kukupa mwanga.

Bufa kama uko vizuri kwenye hili eneo muongozo tafadhali Kaka. Natanguliza shukrani na baraka pia.

Mkuu nilimshauri juu pale aangalie South Africa maana wengi ninaowajua wamesoma aviation SA.
 
Kuna jamaa alienda kusoma huko urusi mambo ya tourism akaradu akakutana na calculater ya TCU GPA ikashuka ikawa ndogo kazi kupata ikawa shida kwa hyo kama unampeleka huko akapambane sio anarudi anakua dj tena
 
Zingatia CANADA

MPELEKE CANADA

KUNA FAIDA NYINGI ZA KUSOMA CANADA NA HATA BAADA YA KUMALIZA MASOMO...

Hawezi kukosa kazi ya kufanya akiwa canada masomoni,

Pia ni rahisi ku gain international job experience.. maana baada ya kuhitimu atapewa tena visa ya kuishi huko sawa na muda aliosoma nchini humo..
Yani mfano aka.a amesoma miaka miwili basi atepewa miaka miwili mingine ...

Pia ni rahisi yeye kupata permanent residence..

AKIAPATA NA U.S pia safi !!
 
Habarini wana jukwaa.

Naomba ushauri wenu tafadhali, nina mwanangu amehitimu mwaka huu kidato cha sita (Feza).

Amepata ufaulu wa daraja la kwanza point 7. ( Div I . 7) Science. Kidato cha nne alipata daraja la kwanza point 7 pia.

Anatamani sana kusoma course zifuatazo zinazohusiana na masuala ya anga (aviation).
  • Aerospace Engineering .
  • Aeronautical engineering.
  • Private Pilot.

Nilipata chuo nje ya nchi (Europe) nikalipia hadi tuition fee lakini bahati mbaya amekosa Visa.

Binafsi nimesikitika sana, amehuzunika sana pia, sihitaji huu mwaka upote bure.

Niko hapa mbele yenu kuomba ushauri, ni jinsi gani naweza kufanya kupata admission kwa muda uliobaki ndani ya mwaka huku, ili aendelee na masomo hasa kwa nchi za Europe (Poland, Cyprus na Scandinavian countries) na North America (Usa & Canada).

Nitashukuru sana kwa mchango wenu.
Kuna Wakala yuko Uganda nikipata muda nitaiweka namba yake mwasiliane kwani ninaamini atakuvusha
 
Ila wewe mzazi aiseee! Mbona sikupatii picha? Unamaanisha nini unaposema nimelipia tuition fee lakini Visa amekosa? Yaani una joining instructions na umelipia halafu unakataliwa Visa? Walikwambia sababu ni nini? Hakuna ubaloxi Katili namna hiyo, isijekuwa umetapeliwa na dalali wewe!
LAbda kuna vigezo vingine alishindwa kuvifikia ndio maana kanyimwa
 
Kapteni, Crusaders yupo kwenye wakati mgumu na amekuja hapa apate muongozo. Kitu ambacho hata Mimi nilikua na shauku ya kujua kwanini kakosa Visa, amekieleza, mtoto akipata chuo uturuki na mipango yote ikaonekana inaenda vizuri Hadi pale dakika za mwisho mgogoro wa FEZA na serikali ya uturuki ulivyoharibu mchakato mzima wa Visa.

Sasa anachotafuta hapa ni namna Gani kijana atapata admission ili aanze masomo mwaka huu?

Nimeona wengi wanamshauri atafute South Africa, yeye shida yake ni chuo chochote Bora atakachoweza kupata admission wakati huu masomo yaanze ndani ya mwaka huu.
Admission nyingi za Europe zinaanza July mpaka December kwa international student. Yeye aanze application kwa ajili ya mwakani. Ufaulu wake na kuthibithisha kama unaweza kulipia ada kwa kipindi chote cha masomo itasaidia kupata admission.
 
Back
Top Bottom