Ushauri: Nimeitwa Polisi

Ushauri: Nimeitwa Polisi

Dah
Hii inshu waweza uichukulie poa
Ila kusema ukweli kupigiwa simu ya kiofisi na police nakukuita kituoni ni shughuli nyingee

Mm walishawahi nipigia japo ile najiandaa niende wakaniambia samahani tumekosea una bahati sanaa.

Aloo nili haha sanaa
Niliwaza kila kitu lakn sioni nilipo na kosaa

Nilitrace miaka miwili nyuma sioni kosa ila naogopa.

Polisi wakikupigia simu tuu jua huna pakutokea wakiamua, labda km wanaona uhitaji wao kwako sio mkubwa sanaaa wakiona unawasumbua na huna msaada mkubwa wanakupotezea.

Tena washakuambia hao n watu wa Cyber

Amini usiamini, wanamawasiliamo ya watu angalau watano unaowasiliana nao mara kwa mara,
Kwenye hio kesi ya mshkaj wangu niliyosema hapo juu, nae walimuita akagoma
Wakanipigia mm, nikaongea na mshkaji akagoma,
Wakampigia baba yake, baba akampigia mwanae ndio mshkaji akaenda, tunafika wakamweka ndani kwa usumbufu.

Mkuu nakushauri sana nenda mzee nendaaa....
Wana angalau nusu ya details zako zote ndio maana wanajiamini kukupigia

Nenda mzeee

Ila twaweza ongea hapa kumbe una siri zako,
Kama una msala mzito mzee USIENDEEEEEE
Japo unazidi kuharibu ila sikushauri
Mm nikiwa na msala mkubwa haki nahama nchi
Kule mahali sipoooo

Kitu cha kwanza kikubwa achana na yote Ni TB.
Hii kitu asilimia kubwa wanaoenda selo wanatoka nayo

Ni hayo tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uzoefu wangu mdogo, hapo ishu sio wewe ila unaweza kusaidia kupata wanachotaka, kama unaweza na una nafasi nenda au kama una ofisi binafsi muelekeze aje ofisini onesha kujiamin ukianza kutetemeka bila kujua sababu watakutesa.
 
Kuna jambazi/mhalifu unawasiliana naye au mtu wako wa karibu?

Aliyekuita alijitambulisha vipi na wewe unamwamini vipi kuwa ni polisi na si tapeli au mwenye nia mbaya na wewe?

Kama upo ok chukua mtu wa kukusindikiza ambaye atakuwa nawe in case of anything. Ili ukatoe ushirikiano kwa kile unachokifahamu.chukua jina la askari husika na namba yake. Nenda kituoni uliza kama kuna mtu mwenye jina na namba hiyo.then waambie amekuita kwa simu unataka onana naye ukiwa na mtu amekusindikiza na umeoa taarifa kwa watu wa karibu.

Then waoneshe ushirikiano.

Kama unatembea na mke wa mtu na chats zenu zimeonekana ni issue ujue. Ombea mwenye mke asiwe karibu akakuona na jinsi ulivyokuwa ukitamba kwenye chats kwa kumkunja mkewe pasipo huruma.
Ushauri mzuri. Ila hili la kumkunja bila huruma, mkuu umebonyeza sana.
Aweza asiende akaogopa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama simtu wamisala na unauhakika uko clean kwenye engo zote, mtangulize Mungu mbele uende jumatatu. Zaidi yahapo utaishi kwa mateso na msongo wa mawazo utakumaliza ukijua siku yoyote utatiwa nguvuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani sheria inasemaje kuhusu summons za polisi?

Yaani inaingia simu out of nowhere eti mtu anadai ni polisi,utaamini vipi?
Vipi Kama simu akipokea mtoto,au houseboy utajuaje unahitajika?
Kwanini wasilete summons physically?
Kabisa, lakin makwambia mara mia uwasiliane kwa Kutumia WhatsApp tu
 
Sasa kama wanayo hiyo namba unayoongea nayo kwanini wasimpigie yeye?
Hapo inaonekana mnatafutwa wote na kwa binadamu kuna wengi wana ishi double life
Wewe unaweza kujua ni nani huyo bila hata kupima upepo hapa

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kuna jambazi/mhalifu unawasiliana naye au mtu wako wa karibu?

Aliyekuita alijitambulisha vipi na wewe unamwamini vipi kuwa ni polisi na si tapeli au mwenye nia mbaya na wewe?

Kama upo ok chukua mtu wa kukusindikiza ambaye atakuwa nawe in case of anything. Ili ukatoe ushirikiano kwa kile unachokifahamu.chukua jina la askari husika na namba yake. Nenda kituoni uliza kama kuna mtu mwenye jina na namba hiyo.then waambie amekuita kwa simu unataka onana naye ukiwa na mtu amekusindikiza na umeoa taarifa kwa watu wa karibu.

Then waoneshe ushirikiano.

Kama unatembea na mke wa mtu na chats zenu zimeonekana ni issue ujue. Ombea mwenye mke asiwe karibu akakuona na jinsi ulivyokuwa ukitamba kwenye chats kwa kumkunja mkewe pasipo huruma.
Polisi wana utaratibu wa kumuita mtu kituoni, huwa wana ku summon, Usiende polisi mpaka upate samass wao huuiita.

Tafuta wakili kIsha mtume akaulizse kama kuna jalada limefunguliwa kuku husu na kama halipo usiende.

Kazi ya upelelezi ni wajibu wa polisi wamtafute muhusika sio kukusumbua wewe.

Katika upelelezi polisi anaweza kukufuata ulipo, na mkazungumza au kama wewe ni suspect unaweza kupelekwa polisi kutoa maelezo yatakayosaidia upelelezi wao.

Usiende polisi na hilo sio kosa, unless wame ku summon halafu ukakataa kwenda.
 
Habari wakuu

Nimepokea simu kutoka kwa mtu anasema yuko central kitengo cha cyber na kuna namba inaonekana naongea nayo na wanataka kujua machache kuihusu
Nimewauliza ni ipi niwajibu? wamekataa wamesema niende central au niwaambie nilipo wanifate nimewajibu ntaenda kesho

Hasa hapa najiuliza niende au? maana polisi wetu hawaaminiki unaeza fika yakawa mengine

Ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiweza kupata wakili wa kuongozana naye, itakuwa ni jambo jema zaidi, na wao pia watakuwa waangalifu ktk utendaji kazi wao.
 
Kuna jambazi/mhalifu unawasiliana naye au mtu wako wa karibu?

Aliyekuita alijitambulisha vipi na wewe unamwamini vipi kuwa ni polisi na si tapeli au mwenye nia mbaya na wewe?

Kama upo ok chukua mtu wa kukusindikiza ambaye atakuwa nawe in case of anything. Ili ukatoe ushirikiano kwa kile unachokifahamu.chukua jina la askari husika na namba yake. Nenda kituoni uliza kama kuna mtu mwenye jina na namba hiyo.then waambie amekuita kwa simu unataka onana naye ukiwa na mtu amekusindikiza na umeoa taarifa kwa watu wa karibu.

Then waoneshe ushirikiano.

Kama unatembea na mke wa mtu na chats zenu zimeonekana ni issue ujue. Ombea mwenye mke asiwe karibu akakuona na jinsi ulivyokuwa ukitamba kwenye chats kwa kumkunja mkewe pasipo huruma.
Sawa kabisa, ila tutumie wanasheria wakuu, wako tele waliosajiliwa na kulipa ada zao, lawyers lawyers lawyers....
 
Mwambie akusinfikize lakini usimwambie kila kitu
Wakuu

Kuna ushauri ametoa TheSpam nadhani ni issue ya simu maana kuna mshkaji wangu mmoja tulienda nae kununua Tecno Cammon X kwenye madukavwanayouza simu used kipindi cha nyuma na ndo anayo mpaka sai

Na kweli huwa tunawasiliana sana maana ndo mshkaji wangu mno Asa kwa mantiki hii nafanyaje?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom