Ushauri: Ni sehemu gani nzuri ya kuishi kati ya Tukuyu ama Kyela?

Nenda tukuyu huo mchele wa kyela unafika tukuyu kwa bei ile ile.
 
Tukuyu ila baridi lake sasa. Kule hakuna jua.
Napenda sana iyo hali.
Labda niwe muwazi tu,huwa nikiwa sehemu za joto Malaria inanionea sana,ila sehemu ya baridi mbu hakuna,hivo hakuna hata haja ya chandarua,maisha yanakua mepesi kiasi fulani.

Pia kwenye baridi hakuna ubishoo,unapigilia mkoti wako mwanzo mwisho....dah sjui ata nisemeje ila napenda sana maisha ya kwenye baridi
 
Kama Moscow vilee...raha sana.
Hali kama hii upo zako ndani unaangalia mpira ama movie, huku una uhakika wa chakula cha kutosha tena asilia(Natural).....Mungu akupe ninii
Maparachichi na ndizi za kuchoma/kukaanga,maziwa ya mgando lita sh1,000,samaki wa ziwa nyasa wanapatikana kwa wingi boda ya Kasumulu.
Ishi Kk au Kiwira. Kyela maisha ni magumu sana kuyaanza
 
kyela ndo mpango mzima,2500 kwa msosi mmoja we boss,kwanza utanawiri sana,samaki mbasa,mberere wali ndo nyumbani kwake,beach kama lote,,matema,itungi etc,hutarudi tena mjini.
 
Nenda Tukuyu. Green city.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…