Root root AE
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 207
- 345
Habari wakuu...
Niende moja kwa moja,ni hivi nataka kuhamia MBEYA na lengo langu ni kuishi moja kati ya sehemu nilizotaja hapo juu,"TUKUYU ama KYELA.
LENGO KUU
Kuishi sehemu ambayo sitatumia zaidi ya 2500/= kwa upande wa chakula,na nishibe vizuri tu.Niwe chimbo uko nidundulize walau nikirudi Dar es Salaam nifanye kitu cha maana.
Kwanini Mbeya?
Napenda sana mikoa yenye baridi lakini pia chakula cha kutosha.
Sehemu yenye baridi hakuna matumizi kama ya Feni,Jokofu(Fridge) n.k
Sasa kwanini Tukuyu na Kyela? na si kwingine?
🔹TUKUYU
Kwa utafiti mdogo nilioufanya naskia hii ndo sehemu ambayo huwa na baridi sana kuliko zote mbeya.
Lakini pia kwa mtu kama mimi ninayeenda kuanza maisha vyumba vya 10,000/= mpaka 20,000/= kwa mwezi napata.
Naskia pia kuna ndizi za kutosha.
🔸KYELA
Huku naskia mchele mzuri na mtamu kwa gharama nafuu ndo kwao,pia samaki wazuri watamu kwa gharama nzuri pia wapo wa kutosha.
Wakuu hizi zote ni mbinu za kivita kuona walau kama tunaweza kuyashinda mapambano ya kiuchumi.
Hivo naomba kama kuna anayekaa au aliwahi kuishi sehemu hizo mbili anisaidie uzoefu wake na taarifa kwa kina.
NB
Nataka nikaishi maisha ya hadhi ya chini tu(nipo tayari) ila yenye MALENGO.
Naamini baada ya miaka mitano sintakua mimi yule.
"Tough times never last,but tough people do".
[UPDATE]
Wakuu shukrani kwa michango yenu yote,na sehemu niliyoichagua ni TUKUYU(Mwakaleli,kijiji cha KANDETE).
Kitu cha mwisho ambacho naomba ushauri wenu ni namna ya kusafirisha vitu vyangu,Kitanda,jiko la gesi...nk
Ni magari yapi yanasafirisha vitu vya ndani kama nilivyo vi orodhesha hapo juu....gharama yake ni kiasi gani? yanapatikana wapi?
Natanguliza shukurani.