Ushauri: Ni sehemu gani nzuri ya kuishi kati ya Tukuyu ama Kyela?

Root root AE

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
207
345
Habari wakuu...

Niende moja kwa moja,ni hivi nataka kuhamia MBEYA na lengo langu ni kuishi moja kati ya sehemu nilizotaja hapo juu,"TUKUYU ama KYELA.

LENGO KUU

Kuishi sehemu ambayo sitatumia zaidi ya 2500/= kwa upande wa chakula,na nishibe vizuri tu.Niwe chimbo uko nidundulize walau nikirudi Dar es Salaam nifanye kitu cha maana.

Kwanini Mbeya?
Napenda sana mikoa yenye baridi lakini pia chakula cha kutosha.
Sehemu yenye baridi hakuna matumizi kama ya Feni,Jokofu(Fridge) n.k

Sasa kwanini Tukuyu na Kyela? na si kwingine?

🔹TUKUYU
Kwa utafiti mdogo nilioufanya naskia hii ndo sehemu ambayo huwa na baridi sana kuliko zote mbeya.
Lakini pia kwa mtu kama mimi ninayeenda kuanza maisha vyumba vya 10,000/= mpaka 20,000/= kwa mwezi napata.
Naskia pia kuna ndizi za kutosha.

🔸KYELA
Huku naskia mchele mzuri na mtamu kwa gharama nafuu ndo kwao,pia samaki wazuri watamu kwa gharama nzuri pia wapo wa kutosha.

Wakuu hizi zote ni mbinu za kivita kuona walau kama tunaweza kuyashinda mapambano ya kiuchumi.

Hivo naomba kama kuna anayekaa au aliwahi kuishi sehemu hizo mbili anisaidie uzoefu wake na taarifa kwa kina.

NB
Nataka nikaishi maisha ya hadhi ya chini tu(nipo tayari) ila yenye MALENGO.
Naamini baada ya miaka mitano sintakua mimi yule.

"Tough times never last,but tough people do".

[UPDATE]

Wakuu shukrani kwa michango yenu yote,na sehemu niliyoichagua ni TUKUYU(Mwakaleli,kijiji cha KANDETE).

Kitu cha mwisho ambacho naomba ushauri wenu ni namna ya kusafirisha vitu vyangu,Kitanda,jiko la gesi...nk

Ni magari yapi yanasafirisha vitu vya ndani kama nilivyo vi orodhesha hapo juu....gharama yake ni kiasi gani? yanapatikana wapi?

Natanguliza shukurani.
 
Habari wakuu...

Niende moja kwa moja,ni hivi nataka kuhamia MBEYA na lengo langu ni kuishi moja kati ya sehemu nilizotaja hapo juu,"TUKUYU ama KYELA.

LENGO KUU

Kuishi sehemu ambayo sitatumia zaidi ya 2500/= kwa upande wa chakula,na nishibe vizuri tu.Niwe chimbo uko nidundulize walau nikirudi Dar es Salaam nifanye kitu cha maana.

Kwanini Mbeya?
Napenda sana mikoa yenye baridi lakini pia chakula cha kutosha.
Sehemu yenye baridi hakuna matumizi kama ya Feni,Jokofu(Fridge) n.k

Sasa kwanini Tukuyu na Kyela? na si kwingine?

🔹TUKUYU
Kwa utafiti mdogo nilioufanya naskia hii ndo sehemu ambayo huwa na baridi sana kuliko zote mbeya.
Lakini pia kwa mtu kama mimi ninayeenda kuanza maisha vyumba vya 10,000/= mpaka 20,000/= kwa mwezi napata.
Naskia pia kuna ndizi za kutosha.

🔸KYELA
Huku naskia mchele mzuri na mtamu kwa gharama nafuu ndo kwao,pia samaki wazuri watamu kwa gharama nzuri pia wapo wa kutosha.

Wakuu hizi zote ni mbinu za kivita kuona walau kama tunaweza kuyashinda mapambano ya kiuchumi.

Hivo naomba kama kuna anayekaa au aliwahi kuishi sehemu hizo mbili anisaidie uzoefu wake na taarifa kwa kina.

NB
Nataka nikaishi maisha ya hadhi ya chini tu(nipo tayari) ila yenye MALENGO.
Naamini baada ya miaka mitano sintakua mimi yule.

"Tough times never last,but tough people do".
big up kwa 100% tukuyu ,ila inabidi kuoa kabisa ......
 
Umemaliza mkuu kyela ile ni boda muda wote ni mchakamchaka, maisha ya kyela ghari sana aisee kuanzia kula, kulala hadi kuvaa
Kwa kukushauri tu, ni vema ukachagua kuishi Tukuyu ila katika kijiji cha Kiwira kwani hapo ndiko yaliko hayo maisha uyatakayo. Nimeishi sehemu zote unazozitaja ila pazuri zaidi ni hapo nilipokwambia. Kyela kuna joto kali na maisha ni ghali kama Dar tu.
 
Kyela hakuna baridi ni joto kama la Dar tuu labda tofauti ni kidogo sana. Maisha ya Kyela ni magumu sana na hakuna hela hayana tofauti na Dar sema tuu kwamba hela mzunguko sio kama Dar.

Tukuyu ni sawa maisha angalao ni rahisi ndizi na maziwa utapata, changamoto la Tukuyu ni baridi lakini umeshasema wewe ndicho upendacho. Labda hapo utaweza kufanya biashara lete magimbi ndizi Dar maisha yatakuwa murua tuu.
 
blackberry mhaya st: 31804901 said:
Kwa kukushauri tu, ni vema ukachagua kuishi Tukuyu ila katika kijiji cha Kiwira kwani hapo ndiko yaliko hayo maisha uyatakayo. Nimeishi sehemu zote unazozitaja ila pazuri zaidi ni hapo nilipokwambia. Kyela kuna joto kali na maisha ni ghali kama Dar tu.
Nashukuru sana mkuu,haya ndo mambo ninayoyata.
Natamani na wengine mtiririke kama ndugu yangu hapa.
 
Back
Top Bottom