Ushauri: Nanyanyaswa na mke wa baba yangu mdogo

Isaack Newton

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
619
Reaction score
371
Habari wakuu,

Mimii ni kijana wa miaka 23, nimemaliza kidato cha sita mwaka huu, tangu nianze masomo yangu kidato cha kwanza, mke wa baba yangu mdogo ananinyanyasa sana, na nilikua nasikiaga ndugu zangu wakisema yule mama ana roho mbaya sana, yeye hana mtoto hata mmoja, kama mnavofahamu kukosea kwa binadamu ni kawaida nikimaanisha kwamba ikitokea labda nimevunja glasi nikiwa naosha, yeye hatambui kuwa ni bahati mbaya yeye anajua moja kwa moja ni makusudi.

Huwa ananitishia kunifukuza kwake na hapa me sina baba na sijawahi kumuona machoni maana alishafariki mi nkiwa mdogo sana na nimelelewa na bibi na mama yangu hana uwezo. Siku zote anataka mi niwe nafanya kazi, kazi zenyewe hamna ila raha yake anataka uwe unashikashika hata madirisha ili aridhike, akiniona nimekaa anatafuta kisa anakuja anamwambia baba yangu mdogo kwamba simuheshimu.

Baba yangu mdogo nae ananijilia juu, nikikaa nje nasemwa, nikiangalia TV sebuleni nasemwa, nikikaa chumbani nasemwa. Jamani nifanyeje maisha haya maana nimevumilia sana jamani, mpaka marafiki zangu wananishangaa maana huyu mama hataki mimi niwatembelee marafiki zangu na hataki aone rafiki yoyote kwake.
Nishaurini maana nilikua na drop academically shuleni kwa sababu ya kukaa na mawazo mengi.

Jamani naombeni ushauri wenu

Nawasilisha jamani
 
Umekua wewe sasa ukapange. Una drop masomo gani na hali ushamaliza form six???

Mie nimeishi na tuvijana tunato jiona tumekuwa, tuvivuuu mno, kujidai maisha ya movie, rimoti inakuwa kama extensio ya mb.o zao.

Na nikiangalia umelelewa na 'bibi', nahisi wewe ni janga. Mwanamme haogopi kazi, tena zenyewe za kufuta madirisha? Ingekuwa kumwaga zege??
 
Maisha uliyopitia nimepitia hayo hayo , kwa story yako fupi hii tumeshare ving na kikubwa umri tumelingana

wanawake wakat mwngne n viumbe wabaya sana , Nilichoamua kufanya mm niliondoka home nikaenda kuanza maisha yangu , saiv naish kwangu sisumbuliw na mtu , huna sababu ya kunyanyasik ushakua mkubwa
 
Pole sana kwa hayo yote unayopitia mdogo wangu but kuwa na furaha na amani tele kwani yamekuja kwako ili uwe imara, uwe na mafanikio na kikubwa zaidi uwe mtu wa kujali ndugu na rafiki. I pray for you that you pass your ACSEE and join university education directly, thereafter you will have happy life as you will be able to lead your own life.
 
Miaka 23 umemaliza kidato cha 6 bado unakaa kwa wazazi.
 
Unanyanyaswa kwa kukubali kunyanyaswa
ignore her..fanya yako....
mchukulie mgonjwa wa akili
na acha mazoea ya kucheka nae wala kuzungumza nae akijichekesha
kunja sura tu kutwa ukimuona huku unaendelea na masomo yako.....
usiguse tv yake...
 
Umekua wewe sasa ukapange. Una drop masomo gani na hali ushamaliza form six???

Mie nimeishi na tuvijana tunato jiona tumekuwa, tuvivuuu mno, kujidai maisha ya movie, rimoti inakuwa kama extensio ya mb.o zao.

Na nikiangalia umelelewa na 'bibi', nahisi wewe ni janga. Mwanamme haogopi kazi, tena zenyewe za kufuta madirisha? Ingekuwa kumwaga zege??

kwa nini hukuwatimua sasa na wewe?
 
Maisha uliyopitia nimepitia hayo hayo , kwa story yako fupi hii tumeshare ving na kikubwa umri tumelingana

wanawake wakat mwngne n viumbe wabaya sana , Nilichoamua kufanya mm niliondoka home nikaenda kuanza maisha yangu , saiv naish kwangu sisumbuliw na mtu , huna sababu ya kunyanyasik ushakua mkubwa

Ndo kamaliza fom 6 .
Anaanzaje kupanga?
MPE mbinu
 
Umekua wewe sasa ukapange. Una drop masomo gani na hali ushamaliza form six???

Mie nimeishi na tuvijana tunato jiona tumekuwa, tuvivuuu mno, kujidai maisha ya movie, rimoti inakuwa kama extensio ya mb.o zao.

Na nikiangalia umelelewa na 'bibi', nahisi wewe ni janga. Mwanamme haogopi kazi, tena zenyewe za kufuta madirisha? Ingekuwa kumwaga zege??

samahani mkuu,naomba nikuulize swali moja la msingi, unanishauri nkapange, je ntapanga vip wakati sina kipato,na mbali na kipato jana nimetoka kuongea na baba yangu mdogo nikamwambia kwamba kwa kipindi hiki naomba nitafte kazi yyte ya kuniingizia kipato na kazi nilishapata kiwanda flani hivi, cha kusikitisha nikakataliwa, na mi sio kwamba nimvivu, napenda sana kazi iwe ya aina yoyote ambayo ni halali.
 
Huyo mwanamke ndo maana Hana mtoto,hicho ni kipimo Kama anashindwa kukulea wewe Mungu hawezi mpa
 
samahani mkuu,naomba nikuulize swali moja la msingi, unanishauri nkapange, je ntapanga vip wakati sina kipato,na mbali na kipato jana nimetoka kuongea na baba yangu mdogo nikamwambia kwamba kwa kipindi hiki naomba nitafte kazi yyte ya kuniingizia kipato na kazi nilishapata kiwanda flani hivi, cha kusikitisha nikakataliwa, na mi sio kwamba nimvivu, napenda sana kazi iwe ya aina yoyote ambayo ni halali.

Hutakiwi kumuomba ruhusa ya kuondoka , ulitakiwa KUMUAGA
 
Babako anakukataza kufanya kazi? Wee bado mdogo, acha wakuendeshe tu.

Siku ukikua hutaruhusu mtu akukataze kufanya kazi wala kupanga chumba, utajikuta tu umeshafanya maamuzi, babako mdogo unampa tu taarifa.

samahani mkuu,naomba nikuulize swali moja la msingi, unanishauri nkapange, je ntapanga vip wakati sina kipato,na mbali na kipato jana nimetoka kuongea na baba yangu mdogo nikamwambia kwamba kwa kipindi hiki naomba nitafte kazi yyte ya kuniingizia kipato na kazi nilishapata kiwanda flani hivi, cha kusikitisha nikakataliwa, na mi sio kwamba nimvivu, napenda sana kazi iwe ya aina yoyote ambayo ni halali.
 
Ať 23 unaweza kujimudu kabisa mzee, na hapo sio kwenu. Fanya mambo ama endelea kunyanyasika.

kujimudu naweza mkuu sema tatzo linakuja kwamba hawataki mi nianze kuchakalika na ukiangalia wenzangu niliomaliza nao sa hv wanahangaika me niliwaomba nianze kuhangaika na maisha nikakataliwa kata kata na mkuu mpk nimekuja kuomba ushauri kwenu ujue hayo yote uliyoyasema nishayajarbu lkn ndo vile.
 
Pole sana kwa hayo yote unayopitia mdogo wangu but kuwa na furaha na amani tele kwani yamekuja kwako ili uwe imara, uwe na mafanikio na kikubwa zaidi uwe mtu wa kujali ndugu na rafiki. I pray for you that you pass your ACSEE and join university education directly, thereafter you will have happy life as you will be able to lead your own life.

nashukuru sana mkuu wa ushauri wako.
 
kujimudu naweza mkuu sema tatzo linakuja kwamba hawataki mi nianze kuchakalika na ukiangalia wenzangu niliomaliza nao sa hv wanahangaika me niliwaomba nianze kuhangaika na maisha nikakataliwa kata kata na mkuu mpk nimekuja kuomba ushauri kwenu ujue hayo yote uliyoyasema nishayajarbu lkn ndo vile.
Tafute mishe halafu unaaga tu, wataelewa mbele ya safari. Leo wakikataa usiendelee shule na umepata nafasi sidhani km utakubali.
 
Back
Top Bottom