Ushauri: Nahisi mchumba wangu ana mahusiano na wanaume wengine

michael G

Member
Jul 28, 2018
21
19
Habari za Jumapili. Poleni kwa majukumu na pole kwa Mashabiki wenzangu wa SIMBA ila safarii bado.

Nina mpenzi wangu tupo kwenye mahusiano kwa miaka 5 sasa (2016-2021) ila shida inakuja kwenye Simu yakee, hataki niishike na nikiishika nakuwa natumia nguvu sana, na anasema hataki nimkague ila Simu yangu akija lazma aishike na aikague kila sehemu.

Juzi alikuja wakati yupo nje ananisaidia kufua, niliingia ndani nikashika mkoba wake nikakuta kuna simu ndogo mpya ila hajawahi kuniambia kuwa ana simu ndogo niliiwasha, nikakuta haina laini ila ina sms za mapenz mfano Bby, wife, mke wangu kwa namba 3 tofauti.

Nikaizima nikairudisha kwenye mkoba na sikumwambia kama nimeona simu hiyo ndogo, baada ya muda nikatumia akili binafsi kumuuliza kuhusu sms kwa sababu sikutaka ajue kuwa nimeona simu ndogo, akaniambia kuwa hao watu wanamtongoza tu ila hajawah kulala nao na hana mpango nao.

Nikachukua zile namba alivyoondoka nikazipiga ili nijue ukweli moja ya zile namba ilikua ni namba ya Daktari ambaye wanafanya wote kazi katika hospitali moja hapo Dar, akaniambia hana yeye hana lolote linaloendelea na huyo mpenzi wangu, japo huyu mpenzi wangu alishawahi kunielezea kuhusu huyo Dkt kuwa anamtongoza.

Sasa nawaza kwanini huyu mwanamke alinificha kuhusu hiyo simu ndogo?? Na mpaka leo hajaniambia.

Je hizo chating kwenye simu nizieleweje ni kweli wanamtongoza tu au kuna namnaa hapoo??

Na kwanini hataki nishike simu yake ili hali yangu anashika muda wowote?

NB; Baada ya kumpigia yule Dkt baada ya muda mpenzi wangu alinipigia na kuanza kunilaumu kwanini nimefanya vile na kuanza kunikejeli kuwa najidhalilisha na sijiamini, na kuongezea kuwa kama mimi ni rijali kwanini nafanya vilee??

Na tumepanga kutambulishana mwez wa 8 mwaka huu.

Ingekuwa wewe ungefanyajee?
 
Wanawake hawaeleweki mkuu , Wanafalisafa wengi duniani wameshindwa kung'amua Wanawake wanataka nn kina Albert, Isac Newton na Darwin pamoja na sayansi zao wameshindwa kuelewa wanawake wanataka nn sembuse we ?

Kuna Mwanafalisafa mmoja pekee aliegundua Wanawake wanataka nn na ushahidi wake ulionekana kukubalika na watu wengi alisema "Wanawake wanataka pesa ukiwa nayo watatulia" cha kushangaza sasa baada ya Bill gate na Melinda gate kuachana huyu Mwanafalisa ameenda Chaka saiv karud Tena kufanya research 😁 Cha msing ukijua kuishi na hawa viumbe hawatakupa shida we jilie mbususu tu mengine hayakuhusu wahuni Wana msemo wao kwamba Kama pisi inatokea location fresh ukiwa na haja zako unamaliza mishe zngne cjui anatoka na Nan haina Maana 😁😁😁
 
Tuanze, ulimuingiaje daktari?

Unajua kuna ile kumchana mwanaume mwenzako mpaka mwenyewe anakuambia ukweli kama anamla au la!. Kama ulienda kiupole au kiukali basi jibu lazima liwe silalani naye.

Ila ungeingia kiakili namna hii:
Mambo vipi bro? Asee huyu manzi X unamuonaje? Mimi ni demu wangu, najua na wewe unatafuna. Ila kama una malengo naye mpoteze. Kuna njemba nyingine ya pembeni inamkandamiza.. Hata mimi nilikuwa na mpango wa kuitambulisha home lakini Hapana. Tuendelee tu kuitumia kama chakula.

Au we bro unasemaje?

Angekuambia ukweli mtupu.
 
Wanawake hawaeleweki mkuu , Wanafalisafa wengi duniani wameshindwa kung'amua Wanawake wanataka nn kina Albert, Isac Newton na Darwin pamoja na sayansi zao wameshindwa kuelewa wanawake wanataka nn sembuse we ? Kuna Mwanafalisa mmoja pekee aliegundua Wanawake wanataka nn na ushahidi wake ulionekana kukubalika na watu wengi alisema "Wanawake wanataka pesa ukiwa nayo watatulia" cha kushangaza sasa baada ya Bill gate na Melinda gate kuachana huyu Mwanafalisa ameenda Chaka saiv karud Tena kufanya research Cha msing ukijua kuishi na hawa viumbe hawatakupa shida we jilie mbususu tu mengine hayakuhusu
daaah "pisi kama inatokea location fresh"
nimekuelewaa mkuu
 
Tuanze, ulimuingiaje daktari?

Unajua kuna ile kumchana mwanaume mwenzako mpaka mwenyewe anakuambia ukweli kama anamla au la!. Kama ulienda kiupole au kiukali basi jibu lazima liwe silalani naye.

Ila ungeingia kiakili namna hii:
Mambo vipi bro? Asee huyu manzi X unamuonaje? Mimi ni demu wangu, najua na wewe unatafuna. Ila kama una malengo naye mpoteze. Kuna njemba nyingine ya pembeni inamkandamiza.. Hata mimi nilikuwa na mpango wa kuitambulisha home lakini Hapana. Tuendelee tu kuitumia kama chakula.

Au we bro unasemaje?

Angekuambia ukweli mtupu.
Daktari anakulaa.
 
Ndugu yangu kama hujamuoa, hebu nakuomba ufikirie upya kuhusu maamuzi yako. Japo simu ya mtu binafsi lakini ni muhimu kutoweka mipaka kwenye simu za mke na mme, mfano kuna muda simu yangu inaisha chaji hivyo natumia ya mke wangu pale dharura. Pia ukiwa na mwanamke anaekuwa line ama simu ya kuficha mme wake huyo siyo mke sahihi wa kuoa bali hawa tunawatumia kukidhi haja zetu za mwili lakini siyo kuoa.

Mimi binafsi sipendelei ama kuwa mke mwenye simu yenye password zaidi ya 1, unakuta simu ya mwanamke kila sehemu kuna sms halafu unajisifu kuwa una mke, huyo ni danguro aliyejificha kwa jina la mke.

Jitahidi sana kufanya utafiti wa uhakika kama mwanaume ili uchukuwe maamuzi sahihi maana kufanya hivyo ni kuokoa maisha yako wewe mwenyewe na kizazi chako. Kama utaona hafai tafuta mke mwingine lakini usipendelee manesi japo siyo wote lakini walio wengi tabia zao siyo nzuri.
 
Tuanze, ulimuingiaje daktari?

Unajua kuna ile kumchana mwanaume mwenzako mpaka mwenyewe anakuambia ukweli kama anamla au la!. Kama ulienda kiupole au kiukali basi jibu lazima liwe silalani naye.

Ila ungeingia kiakili namna hii:
Mambo vipi bro? Asee huyu manzi X unamuonaje? Mimi ni demu wangu, najua na wewe unatafuna. Ila kama una malengo naye mpoteze. Kuna njemba nyingine ya pembeni inamkandamiza.. Hata mimi nilikuwa na mpango wa kuitambulisha home lakini Hapana. Tuendelee tu kuitumia kama chakula.

Au we bro unasemaje?

Angekuambia ukweli mtupu.
Sasa unapiga mkwara weeee ghafla mshkaji anakutumia video anamsulubisha then ana delete. Utakufa kwa preshs
 
Mkuu Ulitaka kumla bata hutakiwi kumchunguza sana.
Ninamaanisha nini, kuna vitu unatakiwa umuweke wazi kuwa unapenda na nini haukipendi kama anakuheshimu na anakuhitaji basi atabadilika ataonesha tabia njema.

1. Mimi iliwahi kutokea hivyo kwa Huyu mpenzi wangu nilie naye. Nilikaa nikamweleza aina ya mke ninayemtaka hivyo nikamtaka kwa lugha ya chini huku nikimbembeleza kwa hisia kuwa abadilike, ni kweli alibadilika na akaongeza na tabia nyingine nzuri.

2. Kitu kingine ambacho unatakiwa kufahamu kuna wanawake huwa hawataki kushauriwa vitu hivyo kuwa makini sana. Unatakiwa ucontrol akili yako iamini kuwa hana mpenzi mwingine zaidi yako (Mind manipulation) hii iko psychological zaidi ukiweza itakusaidia.

3. Achana kabisa na kuwaza kushika simu yake. Mkuu ukifanikiwa kuizuwia akili yako kuwaza kuhusu simu yake basi utakuwa umejiondolea mzigo wa panic, stress, na matatizo ya moyo.

4. Kama hamuishi wote mwambie akija nyumbani kwako au sehemu yoyote mnayokutana basi asiwe busy na simu hata kidogo.

Yangu ni hayo tu naomba kuwasilisha.

KIJISTORI KUNIHUSU MIMI.
Mimi nilibahatika kusoma mambo kidogo ya hacking huko mitandaoni, hivyo niliwahi kumhack mpenzi wangu lakini nilijuta, kadri siku zilivyozidi nilianza kupata mahasira hadi kazini, mtaani hadi kwenye daladala.
Nakumbuka siku moja nipo kwenye daladala konda aliuliza kituo
Konda: Nyegezi Kona wakushuka
Mimi: Konda acha u-s-e-n-g-e nipitilize gone(KWA SAUTI YA UKALI SANA).
Kwanza sijui kutumia maneno makali kama u-s-e-n-g-e, lakini niliyatumia ndani ya mwezi mzima.
Pili nilikuwa na hasira kwa sababu konda sikuwa nimemwambia awali kuwa ninashuka kituo alichokitaja konda.
Tatu wakati konda anauliza kituo kinachofuata nilikuwa bado hatujafika kwa wao uifahamu geographia ya jiji la Mwanza tulikuwa Bohari konda aliuliza Isenyi(hakuna aliyekuwa anashuka) kisha akauliza Nyegezi kona.

Kwa leo niishie hapo Lakini, usijaribu kujihusisha na simu ya mpenzi wako kabisa kama unampenda itakuumiza na kuvunja mahusiano yenu.
 
Back
Top Bottom