Mgembe05
Member
- Oct 20, 2016
- 16
- 9
Habari za mchana, Mimi ni Kijana wa miaka 30 nimeoa miaka miwili iliyopita na nampenda sana mke wangu.
Nimejaribu kumpa mimba mke wangu kwa miaka 2 hiyo lakini imeshindikana, ilinibidi niende kwa doctor ktk Hosp moja hapa jijini lakini baada ya vipimo ilionekana sitoweza pata Mtoto maishani mwangu, nimeumizwa sana na hili tatizo.
Ninahitaji ushauri kama nimwambie mke wangu juu ya hili au nikae tu kimya? Ikumbukwe kwamba tupo mikoa tofauti kwa ajili ya majukumu ya kikazi na yeye kapania sana kupata Mtoto December hii kwamba kajiandaa kuchukua likizo ili abebe mimba atakapo kuja.
Naombeni mnishauri nifanye nn juu ya hili maana yeye hana tatizo lolote kwenye kuzazi chake ila Mimi ndio kwenye tatizo.
Nipo tayari kushauriwa hata kukejeliwa pia.
Kuna posibility kubwa ya ndoa kuvunjika baada ya kumueleza..! itategemea sana na hekma busara pia malezi anayotokea mkeo...lkn all in all kumwambia ni sahihi na akitaka kuvunjika kwa ndoa mruhusu aende kwsbb uking'ang'ania atakufanya uishi kwa shida kubwa kiasi kwamba utakosa na mengine katika maisha....! Na maisha c mke au mtoto peke yake...!